Naomba kujua sababu ya gari kuchemsha (overheat)

Naomba kujua sababu ya gari kuchemsha (overheat)

Mkuu kuna sababu nyingi zinazosababisha injini ya gari kuchemsha.Mojawapo ni radiator/rejeta kama
unatumia maji ya uswahilini badala ya coolant huwa zinajaa kutu kama matope na hivyo njia za maji kuziba.Pia kuna feni inayopoza maji kwenye radiator kama haifanyi kazi ni sababu. Pia kama injini yako imefanyiwa overhaul na fundi akakosea kuset timing belt hii nayo ni sababu.

Pia kuna thermalstart ambazo hutumika kuzuia maji kuzunguka kwenye injini mpaka joto linalotakiwa kwenye injini lifikie, hizi kuna kipindi zinakufa na kushindwa kufungua hata joto la injini likifikia. hizi mara nyingi mafundi wetu huzitoa ili kuondoa tatizo hilo,check kama gari yako inayo.

Kuna kitu kingine rahisi ambacho wewe mwenyewe unaweza kuangalia ni mfuniko wa radiator, kama rubber
yake imechoka huwa inapitisha maji kabla pressure haijafikia kiwango cha kufungua mfuniko kwenda kweny expansion tank na hivyo kusababisha maji kuisha kwenye radiator.

Naamini na wengine wataongezea.
 
Mkuu kuna sababu nyingi zinazosababisha injini ya gari kuchemsha.Mojawapo ni radiator/rejeta kama unatumia maji ya uswahilini badala ya coolant huwa zinajaa kutu kama matope na hivyo njia za maji kuziba...
Mfuniko upo sawa, feni inazunguka kama kawaida. Engine imefanyiwa overhaul na situumii coolant. Je tunawezaje kuondoa kutu ndani ya radiator? Na kuhusu timing belt naomba ufafanuzi zaidi
 
Mkuu kuna sababu nyingi zinazosababisha injini ya gari kuchemsha.Mojawapo ni radiator/rejeta kama unatumia maji ya uswahilini badala ya coolant huwa zinajaa kutu kama matope na hivyo njia za maji kuziba...
Na pia aangalie water pump kama iko imara. Kama inavujisha engine coolant.
 
Mfuniko upo sawa, feni inazunguka kama kawaida. Engine imefanyiwa overhaul na situumii coolant. Je tunawezaje kuondoa kutu ndani ya radiator? Na kuhusu timing belt naomba ufafanuzi zaidi
Kutu kwenye radiator inaondolewa kwa kuwapelekea mafundi wa radiator ili waisafishe.Lakini kama injini imefanyiwa overhaul mwone fundi wako aangalie upya timing, kama alitega vibaya lazima itasumbua kwa kuchemsha.Kuna kifaa kinatumika kupima usahihi wa timing kama sikosei ni "timing torch" ngoja nitafute nitarudi.
 
Nimerudi tena inaitwa "timing light" siyo "timing torch", mafundi wengi mtaani wanapofanya engine overhaul
hawatumii hiki kifaa na hivyo mara nyingi wanasababisha matatizo. Kuna kitu kinaitwa "timing angle" bila hiki kifaa uwezekano wa kupatia ni mdogo sana.
 
Hivi kutokuwepo ke maji au kulant kunaweza kusababisha kuchemsha?
Yap kunaweza kusababisha engine kuchemsha

Ngoja nikupe elimu kidogo

Maji hayapoozi engine moja kwa moja ila yanapooza kama ifuatavyo:-

Oil inakazi tatu nazo ni
1.kuleta mlainisho wa vyuma
2.kusafisha engine
3.kupooza engine

Hapo kwenye kupooza engine ipo ivi:-

Oil inapozunguka kwenye engine inakutana na joto na ukisoma theory ya tempature inasema iv:-
Joto husafiri kutoka sehem yenye joto kubwa kuelekea kwenye sehem au chombo chenye joto dogo(heat transfer)

Kwaiyo oil inagain heat kutoka kwenye engine

Oil hiyo hupoozwa na maji au coolant hali ambayo hupelekea kupungua kwa joto la engine kwasababu oil huingia katika engine ikiwa na joto kidogo na hutoka na joto jingi kitendo ambacho tunaweza kusema oil husafirisha joto kutoka kwenye engine.

Kwaiyo oil hiyo isipopoozwa vizuri jawabu lake ni engine kutopoozwa vizuri jambo ambalo hupelekea engine kupatwa na joto losilo la kawaida

Note. Maji hayaiingii kwenye engine moja kwa moja kwasababu ya tabia yake ya kuweza kusababisha kutu(corrosion) hivyo oil hutumika kama chambo tu

Kama hujaelewa uliza kipengele ambacho unahitaj maelezo zaid ili nikupatie
 
Yap kunaweza kusababisha engine kuchemsha

Ngoja nikupe elimu kidogo

Maji hayapoozi engine moja kwa moja ila yanapooza kama ifuatavyo:...
Nashukuru sana eng.,ni sahihi kuongeza maji ya uhai, badala ya kulant(kuchanganya kulant na maji)? Gar yangu ni noA
 
Back
Top Bottom