Naomba kujua sababu ya gari kuchemsha (overheat)

Naomba kujua sababu ya gari kuchemsha (overheat)

Mkuu habari.
Nimechunguza pale nikifungua mfuniko wa Radiator kutu imejaa. Natumia maji ya bomba kwa muda mrefu.

Je inawezekana maji yote yakaondolewa na system nzima ikasafishwa kutu yote inaondoka? Nataka nianze kutumia Coolant ama nishachelewa/haiwezekan
Kuna "sabuni" ya kusafishia radiator kama hiyo, inaitwa "radiator-flush" kama hii
1605031842423.png

Mwaga maji yote, halafu maji haya kama lita mbili; usiwashe gari kwa kama saa moja hivi kususdi yale kutu yote, halafu washa injini kwa kama dakaika 20, kisha mwaga yote ndipo uweke coolant mpya.
 
Bado upo nje ya nchi?
Kuna gari kilikuu tata piston 2 inachemsha nimechek mfumo wa upozaji uko sawa nimechonga head na nimebadirisha gasket nimeweka namba2 bado inachemsha pump iko sawa timing iko sawa gari inawaka vizuri nipe mawazo yenu tatizo ni nini had bado inachemsha iyo engine ni overhead cam shaft
 
Unatumia maji ya Dawasco au coolant kwenye rejeta?
 
Mkuu kuna sababu nyingi zinazosababisha
injini ya gari kuchemsha.Mojawapo ni radiator/rejeta kama
unatumia maji ya uswahilini badala ya coolant huwa zinajaa kutu
kama matope na hivyo njia za maji kuziba.Pia kuna feni
inayopoza maji kwenye radiator kama haifanyi kazi
ni sababu. Pia kama injini yako imefanyiwa overhaul
na fundi akakosea kuset timing belt hii nayo ni sababu.

Pia kuna thermalstart ambazo hutumika
kuzuia maji kuzunguka kwenye injini mpaka
joto linalotakiwa kwenye injini lifikie,
hizi kuna kipindi zinakufa na kushindwa
kufungua hata joto la injini likifikia.
hizi mara nyingi mafundi wetu huzitoa
ili kuondoa tatizo hilo,check kama gari yako inayo.

Kuna kitu kingine rahisi ambacho wewe mwenyewe
unaweza kuangalia ni mfuniko wa radiator,kama rubber
yake imechoka huwa inapitisha maji kabla pressure
haijafikia kiwango cha kufungua mfuniko kwenda
kweny expansion tank na hivyo kusababisha maji
kuisha kwenye radiator.
Naamini na wengine wataongezea.
ukitumia maji ya kununua dukani hapo vipi??? coolant inauzwa sh ngapi dukani??
 
Kuna gari kilikuu tata piston 2 inachemsha nimechek mfumo wa upozaji uko sawa nimechonga head na nimebadirisha gasket nimeweka namba2 bado inachemsha pump iko sawa timing iko sawa gari inawaka vizuri nipe mawazo yenu tatizo ni nini had bado inachemsha iyo engine ni overhead cam shaft
Baada ya kuchonga (resurfacing) head gasket, ulifanya any pessure test kwenye hiyo cylinder head kuangalia kama kuna leakage kwenye hizo valves?

Ku-resurface head pekee haitoshi, kwasababu kama cylinder head ilikuwa warped (injini kuchemsha), valves huwa hazikai vizuri tena kwenye lile tundu la mduara (valve seat). Hizi valveseat zinabadilika kuwa na umbo la yai na hivyo kusababisha leakage (compression loss, overheating - kuchemsha kwa injini).
 
Mkuu mimi gari yangu inatabia ya kujizima kwenye foleni,au ikiwa silencer,nimejaribu kupandisha silnce lkn bado tatizo lipo?service naw kila kitu kipo vizuri,tatizo nini?
Badili camshaft position sensor
 
Samahan bro. .gari yangu voxy ghafla imeanza kupunguza maji ingawa nikidogo kila asubuhi yanaenda kwenye reseve bottle. Tatizo nini. Pia ikifika spidi 100 alaf ukaachia mafuta ikifka 80 inakuwa inakatakata mafuta na siyo misi
Badili mfuniko wa rejetor huo ndio unakuletea tatizo
 
Back
Top Bottom