.
Hii ni basis ya cooling system ambayo inafanywa na thermostat.
.
Naelewa kuhusu heater ya engine block, na hii siyo magari yote yapo 'equipped'. Ni kwa magari yanayouzwa kwenye 'coldest regions' kama Alaska. Na hii unachomeka cable kutoka kwenye gari kwenda kwenye outlet ya garage (nyumbani) na ku 'heat engine block' kwa muda kabla ya kuiwasha gari. kama haupo karibu na 'electric outlet' kuwezi kufanya hivyo.
Ila usibishe ndugu, maji yanaganda yakifikia 'freezing point' majimaji yaliyoko kwenye radiator yanaganda joto la nje likifika 0°C. Na maji yakiganda yanatanuka (anomalous expansion of water). Kwahiyo raidator inaweza kupasuka pembeni (radiator nyingi zina plastic pembeni) kama maji yakiganda, ndiyo maana kwenye nchi za baridi coolant inashauriwa wakati wa winter.
.
Hii inategemea na engine design, kwa upande wa magari (4 stroke engine), 'coolant' hutumika zaidi (effectively) kupoza , ndiyo maana wakaiita COOL-ant (kipozeo), inayozungukakwenye 'waterjackets'. Hizi huwa zinajaa maji wakati wote ili 'ku transfer excess heat' (moja kwa moja) kutoka kwenye block kwenda kwenye maji.
Oil kazi yake kubwa ni kulainisha 'rod bearings' na 'crankshaft' kwasababu hapa ndo kuna 'maximum turning effect (torque)'. Ndiyo maana kama oil ni kidogo sana, utaanza kusikia 'rod knock'. Pia oil inalainisha 'camshaft' na lifters' kwenye 'cylinder head'.
Oil ni 'viscous' kuliko maji, haiwezi ika 'tranfer heat efficiently' kama maji.
Oil kweli inaweza inapoza engine lakini siyo kiivyo, njia inayopita oil ndani ya engine ni nyembamba kwahiyo ufanisi wake wa kupoza ni mdogo.
kuna magari yenye 'oil cooler', hii yanasaidia kupoza oil kwa kuitoa nje ya engine na kuipoza kwa 'heat exchanger' aidha kwa kutumia upepo (mbele ya gari) au kwa kutumia 'coolant' na kuirudisha kwenye engine ikiwa imepoa. kawaida hii ni kwa 'performance vehicles' (BMW) ambazo zina 'run at high temperatures' (105°C). Oil ikiwa kwenye joto kali huanza kupungua uwezo wake wa kulainisha (viscosity decrease with temperature).
Kwahiyo upozwaji wa oil siyo kwaajili ya kupoze engine bali kuhakikisha oil ina-'maintain it's molecular structure'.