Majibu yote hapo juu ni sahihi ila nitaongezea moja, ambalo ni kuwa na 'warped cylinder head'.
Hapo chini nimeambatanisha mchoro wa 'engine' iliyoharibika (warped cylinder head) kutokana na kuchemka (overheating).
View attachment 588801
Hili hutokea pale ambapo gari imekuwa ikichemka kwa muda mrefu sana (kutokana na sababu zilizotajwa na wenzanu hapo awali) na kusababisha 'cylinder head' kupinda. Matokeo yake maji (coolant) kuingia kwenye chemba na kuunguzwa na kusababisha mvuke mweupe.
kama kila ukiongeza maji kwenye 'cooling system' (radiator or expansion tank) na maji kupotea 'kimazingara' bila ya kujua yanapokwenda basi cylinder head imepinda. Na kadri 'engine' inapozunguka ndipo maji yanapojipenyeza kwenye chema na kuunguzwa. Hii hufanya engine kuzidi kuchemka, kwa kukosa maji ya kuipoza.
Tatizo hili unabidi ulitatue haraka (by removing and resurfacing heads) kwasababu siku moja gari itashindwa kuwaka kabisa kutokana na kupoteza 'compression'.
Hii chini ni 'cylinder head' niliyoitoa kwenye gari iliyokuwa ikichemka, nikiipina kwa kutumia rula (straight edge) kuangalia jinsi ilivyopinda . Utaona kichuma (feeler gauge) kikipenya chini ya rula kuonesha kuwa hii 'cylinder head' imepinda sana.
View attachment 588802
.
Huu ni mchoro wa 'Engine' ambayo haina matatizo ya kuchemsha.
View attachment 588805
Na hii ndiyo 'cylinder head' nzuri utaona kachuma (feeler gauge) hakawezi penya katikati ya 'cylinder head' na rula (straight edge).
View attachment 588810