Naomba kujua Soko la dhahabu na Rubby Dar es Salaam

Wolle Melkas Fernando

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2016
Posts
253
Reaction score
360
Ndugu wafanyabiashara, wajasiriamali na wabobezi wa masuala ya uchumi wasalaam!

Mimi huwa najishughulisha na uchimbaji wa madini ya Rubby na Dhahabu, sasa naomba kwa mwenye uzoefu wa soko zuri la rubby na dhahabu anielekeze ni wapi kuna bei nzuri au bei ina-range kuanzia kiasi gani kwa gram ya dhahabu?

Kabla ya hapo nilikuwa nauza kwa walanguzi tu, lakini kwa sasa nahitaji kupata soko la uhakika.

NB: Vibali vyote ninavyo.
 
Bei ni kuanzia milioni 60 gram 3 au 5 zinalipa vizuri.
Hiyo ruby ya moro, tanga au msumbiji?
Sasa nenda tunduru pale. Dsm uwongo mwingi. Nenda pale kwa wa srilanka umalize presha hiyo..
Utanitumiapo hapo hata kasenti tu. Ka maji.
 
We usisubiri kukutwa na uhujumu uchumi. Kama una madini na vibali vyote, nenda soko la madini Dar es salaam, lipo mkabala na extelecom mtaa wa Samora posta.
 
Bei ni kuanzia milioni 60 gram 3 au 5 zinalipa vizuri.
Hiyo ruby ya moro, tanga au msumbiji?
Sasa nenda tunduru pale. Dsm uwongo mwingi. Nenda pale kwa wa srilanka umalize presha hiyo..
Utanitumiapo hapo hata kasenti tu. Ka maji.
Shukrani sana mkuu! Rubby inatokea Dodoma.
 
Mbona soko la dhahabu liko wazi sana,kama uko dar nenda mtaa wa msikiti huko utapata wanunuz unauza dhahabu kama nyanya...

Naona bei ya dhahabu sahv imedrop tena ila twende kazi

Ova
 
Hongera kwa kupata vibali, Sasa ni wakati wa kutengeneza pesa, all the best
 
Mbona soko la dhahabu liko wazi sana,kama uko dar nenda mtaa wa msikiti huko utapata wanunuz unauza dhahabu kama nyanya...

Naona bei ya dhahabu sahv imedrop tena ila twende kazi

Ova
Mtaa wa msikiti gani? Msikiti wa wapi mkuu?
 
Ndugu wafanyabiashara, wajasiriamali na wabobezi wa masuala ya uchumi wasalaam!

Mimi huwa najishughulisha na uchimbaji wa madini ya Rubby na Dhahabu, sasa naomba kwa mwenye uzoefu wa soko zuri la rubby na dhahabu anielekeze ni wapi kuna bei nzuri au bei ina-range kuanzia kiasi gani kwa gram ya dhahabu?

Kabla ya hapo nilikuwa nauza kwa walanguzi tu, lakini kwa sasa nahitaji kupata soko la uhakika.

NB: Vibali vyote ninavyo.
upo wap Mkuu,na je una rubby nzuri na dhahabu ,wanunuzi ninao
 
Bei ni kuanzia milioni 60 gram 3 au 5 zinalipa vizuri.
Hiyo ruby ya moro, tanga au msumbiji?
Sasa nenda tunduru pale. Dsm uwongo mwingi. Nenda pale kwa wa srilanka umalize presha hiyo..
Utanitumiapo hapo hata kasenti tu. Ka maji.
Vipi mkuu hawa jamaa bado wapo???
 
Natafuta wanunuzi wa silver pure apa Dar es salaam,ambao wananunua kwa bei nzuri kilingana na soko
 
Back
Top Bottom