Naomba kujua ukweli kuhusu 'kiama'

Naomba kujua ukweli kuhusu 'kiama'

Kwakuwa umeuliza kwa imani zote nami nisemi kidogo. Katika uisilam kiama ni siku ngumu kuliko ugumu wowote ambao mwanadamu anaweza waza. Ni siku ya hukumu. Kabla ya kusimama kiama ni wazi kuwa viumbe wote watakafu(wakiwemo maaika wote mpaka mtoa roho-Izraeli).
Kisha watu watafufuliwa kutoka katika matumbo ya ardhi wakiwa katika hali tofauti tofauti.kulingana na matendo yao. Hata hivyo bado siku hiyo itakuwa ngumu sana isipokuwa tu kwa wale waliridhiwa na mola wao.
Hapo ndipo watu watahukumiwa kwa matendo yao. Kuna mchakato mrefu.sana siku hiyo. Hakuna kujuana hapo baba hatamjua mwana wala mwana hatamjua mama. Kila mtu nafsi yake itakuwa imeshughulishwa na mambo yake. Kisha watu watahukumiwa kwa kuulizwa juu ya.yale waloyatenda. Na pindi watakapo danganya,itafungwa midomo yao kisha kila kiungo kipekee kitatoa ushahidi wa kila ulichokifanya.
Kwa wale wanodhani ukifa ndio kiama chako,hakika hawapo sahihi hata.kidogo. Kufa ni katika kitendo cha kufika.mwisho.wa dumia.na mwanzo wa akhera. Kaburi watu watu wataanza kukutana na kheri zao ama shari zao kulingana na matendo yao. Hapo ni adhabu kwa makosa hadi itakapo fika kiama. Na adhanu hii haipunguzi.adhabu atakayoipata mwanadamu siku ya kiama baada ya kuhukumiwa.
Hakika kiama ni siku nzito na tunamuomba Molla wetu atufishe.ili hali yu radhi na sisi ili tuweze kuongoka adhabu zake. Amin.
Inshaallah Amin
 
Haya mambo ya kiroho kwa kiasi kikubwa yana utata sana. Tunaambiwa mtu yaani nafsi anapatikana kutokana na muunganiko wa mwili na roho (pumzi ya uhai) na kwamba mtu huyo anapokufa mwili uoza lakini roho ubaki ikisubiri siku ya kiama. Sasa swali ni kwamba kama kiama kinaanza muda au siku ile mtu anapokufa iweje adhabu iwe ni kwa roho tu na siyo kwa mwili pia wakati kipindi cha kutenda dhambi vilikuwa pamoja?

Na kama mateso yanaanza mara moja baada ya mtu kufa basi ni dhahiri kwamba wale wenzetu waliofariki karne nyingi zilizopita hadi siku ya kiama itakapofika watakuwa wamepata mateso makubwa zaidi (ya muda mrefu) kuliko wale watakao wamekufa miaka michache (mfano mwaka mmoja, miwili kumi n.k.) kabla ya hiyo siku ya kiama. Na kama wakianza kutumikia adhabu zao baada ya kiama hao waliokufa na kupata mateso karne nyingi zilizopita kuliko wengine watapunguziwa adhabu au la?!

Kingine mtu anazaliwa na kudumu duniani kwa dakika, masaa, siku au miaka michache tu lakini siku ya kiama anakuja kutumikia adhabu jehanamu milele! Daah...mimi hata sielewi bana.

Umeelezeaa, ulivomalizia ikabidi nicheke tu
 
Habari zenu wana JF,

Kuna kitu nimekiwaza na kukitafakari kwa muda wa kama siku 3 hivi lakini bado sijapata majibu yake. Basi nipo hapa kuomba msaada wa kueleweshwa kiundani kwa watu wenye uelewa wa mambo ya kidini awe muislam, mkristo budhaa na hata asiye na dini.

Suala kubwa linalonitatiza ni kuhusu ukweli wa siku ya kiama, jehanamu na pepo. Je kweli hivi vitu vipo kweli? Nikiri wazi kabisa kwamba mimi ni mkristo mkatoliki na nimekua nikifundishwa haya kama sio kukaririshwa toka nikiwa mdogo katika mafundisho ya komunio ya kwanza na kipaimara kwamba kuna hivyo vitu 3 nilivyovitaja.

Yafuatayo ni maswali ambayo najiuliza na ningefurah kama nitapata majibu ya kina na kuridhisha.

1. Je ni kweli kuna siku ya kiama?

2. Na kama kweli ipo kwanini MUNGU aliwaadhibu na kuviangamiza baadhi ya vizazi kwa matendo yao machafu na kutosubiri siku ya kiama?

3. Je hawa walioadhibiwa na kuangamizwa siku za nyuma walikuwa waovu kuliko sisi wa zama hizi?

4. Je hao walioangamizwa wataletwa tena mbele ya hukumu? Na nini hatima yao na ilihali walishaadhibiwa kwa kuangamizwa?


Baada ya kupata ufafanuzi wa kutosha wa maswali hayo nadhani suala la pepo na jehanamu nitaweza kulielewa kwa urahisi.

Inawezekana kabisa kuwa kuna mada kama hii imeshawahi kujadiliwa kama hamtojali naomba kuwekewa link yake.

NB: Nimetumia zama za nabii Nuhu na gharika kuu kuuliza maswali hayo.


Shukrani.
Mungu(ALLAH) ana sifa ya kukiambia kitu kua na kinakua na yeye ndio mfalme wa mbingu na ardhi,pia anaamua atakalo na wala hana mshirika.Mfano ameumba kifo na uhai ili atupime ni nani ni mwenye matendo mazuri kati yetu na wala haimaanishi kwamba hajui,ukisoma kisa cha nabii Adam katika Quran utaona sehemu ya utukufu wa mungu na jinsi anavyofanya mambo yake atakavyo na wala haitaji ushauri.Tatizo ndugu zetu injili mmeichakachua na mmendika mambo mengine kwa maslahi ya kidunia,hivi AGANO JIPYA ni kutoka kwa nani?Naomba ujiulize hivi mbona kila siku wenzetu mnapata manabii
 
Mimi naamini kiama ni kifo chako, kwa maana kama ipo hyo d-day kwanini wapo wanaotangulia kufa (toka enzi za adam na eve) mpka sasa dunia ni hii hii je huoni kuwa hakuna fair hapo? kama tutafufuliwa tena pamoja tutakuwa tumewaoneawenzetu wameteseka sana huko chini,
 
Kiama tutakitengeneza wenyewe baba!, siku ya mwisho ni pale Russia watakatoirushia Atomic yapata 100 America na Mchina akamrushia Mrussia, miUiran akamrushia mchina! amini nakwambia Dunia itabaki shamba na utakuwa ndo mwisho wa watu
 
Sasa Amenn kwa hiyo wale moto hautowahusu? Na vipi sasa walokufa kwa maji (enzi za nuhu) wengine kwa moto (sodoma na gomola) na vipi sisi kiama chetu na adhabu ya moto wa milele hauoni hapo kama kutakuwa hamna fair justice?
Mkuu wote waliokufa enzi nuhu (gharika ya maji) n.a. waliokufa enzi za Ibrahim kwa moto ( Sodoma n.a. gomora) wote wataletwa mbele ya kiti cha enzi Katika siku ya mwisho (final judgement). Soma kitabu cha ufunuo sura ya 21 na 22.
 
Back
Top Bottom