Samahani naona ni mpenzi wa BMW lakini nikuombe unisaidie kuhusu hizi BMW 1 series 116i kwenye upande wa fuel consumption na matatizo yake makubwa ya kiufundi na upatikanaji wa vipuli kwa hapa Tanzania
Am BMW fan. Ila bila kua mnafiki BMW ni ghali sana ku-run especially ikija issue ya Maintenance.
Spare parts zake, vitu vya service kama Oil Brakes au tyres ni gharama sana ukicompare na Japanese cars.
Sikutishi, ila nakutaadharisha tu kwamba ukinunua BMW ni kama una m-date m-bongo movie. Shopping Mlimani city, lunch KFC, na vitu kama hivo.
Ukiwa na BMW ukitaka lidumu sana lazima ulpende. Tumia vipuri original, usiende garage za chini ya mwembe (nenda kwa authorized dealers mfano Noble Cars Tanzania), oil tumia recommended na even mafuta (petrol) itabidi utumie Premiums (Total mfano wanayo).
Haya turudi kwenye swali.
Sijui umeipendea nn 116i, ila ina engine ndogo sana 1.6L ingawa zipo kubwa zake ila hapa tuzungumzie base Model.
Pia, ni 4-inline valves ingawa zipo kubwa hadi 6 na turbo models zipo.
Kwa bei zetu najua utataka cheapest model E87 (hatchback). Sasa bro ukitaka nunua make sure ni kuanzia mwaka 2008 coz hii model BMW waliipa LCI (Life Circle Impulse) au kwa lugha nyepesi Facelift so kuna baadhi ya Updates zimefanyika. Kubwa ni replacement ya N45 engine na zikawekwa N43, pia exterior na interior na monitor uprades kadhaa. Usinunue F series zitakua bei chafu.
Bro natamani niongee hadi asubuhi ila jipe homework hii kabla hujaenda kununua hiyo ndinga:
1. Una mafundi/ dealer unapokaa?
2. Umejiandaa kutumia gharama kubwa kwenye vipuli na service? Hapa sikutishi. BMW ni very reliable ila zikizingua utatamani ubadirishane na Passo.
3. Kasome tofauti ya izo engine N43 na N45 ujue common problems na wewe ipi utaipenda.
Utakuta watu wengi wanakuambia epuka BMW engine zenye kuanza na N na zikiwa 4 cylinders.
Ila all in all karibu Ujerumani.