Naomba kujua zaidi kuhusu Toyota Crown Majesta

Naomba kujua zaidi kuhusu Toyota Crown Majesta

Samahani naona ni mpenzi wa BMW lakini nikuombe unisaidie kuhusu hizi BMW 1 series 116i kwenye upande wa fuel consumption na matatizo yake makubwa ya kiufundi na upatikanaji wa vipuli kwa hapa Tanzania
Am BMW fan. Ila bila kua mnafiki BMW ni ghali sana ku-run especially ikija issue ya Maintenance.

Spare parts zake, vitu vya service kama Oil Brakes au tyres ni gharama sana ukicompare na Japanese cars.

Sikutishi, ila nakutaadharisha tu kwamba ukinunua BMW ni kama una m-date m-bongo movie. Shopping Mlimani city, lunch KFC, na vitu kama hivo.

Ukiwa na BMW ukitaka lidumu sana lazima ulpende. Tumia vipuri original, usiende garage za chini ya mwembe (nenda kwa authorized dealers mfano Noble Cars Tanzania), oil tumia recommended na even mafuta (petrol) itabidi utumie Premiums (Total mfano wanayo).

Haya turudi kwenye swali.
Sijui umeipendea nn 116i, ila ina engine ndogo sana 1.6L ingawa zipo kubwa zake ila hapa tuzungumzie base Model.
Pia, ni 4-inline valves ingawa zipo kubwa hadi 6 na turbo models zipo.

Kwa bei zetu najua utataka cheapest model E87 (hatchback). Sasa bro ukitaka nunua make sure ni kuanzia mwaka 2008 coz hii model BMW waliipa LCI (Life Circle Impulse) au kwa lugha nyepesi Facelift so kuna baadhi ya Updates zimefanyika. Kubwa ni replacement ya N45 engine na zikawekwa N43, pia exterior na interior na monitor uprades kadhaa. Usinunue F series zitakua bei chafu.

Bro natamani niongee hadi asubuhi ila jipe homework hii kabla hujaenda kununua hiyo ndinga:

1. Una mafundi/ dealer unapokaa?
2. Umejiandaa kutumia gharama kubwa kwenye vipuli na service? Hapa sikutishi. BMW ni very reliable ila zikizingua utatamani ubadirishane na Passo.
3. Kasome tofauti ya izo engine N43 na N45 ujue common problems na wewe ipi utaipenda.
Utakuta watu wengi wanakuambia epuka BMW engine zenye kuanza na N na zikiwa 4 cylinders.

Ila all in all karibu Ujerumani.
1280px-BMW_E87_front_20080719.jpg
1280px-BMW_E81_dashboard_20080719.jpg
 
Mad Max, Daa...kama haya yote ni kweli sioni sababu ya kununua European cars..
Kuna ndinga za mjapani ambazo bado zina heshima tu barabarani na ni reliable.

Anyway...kipenda roho hula nyama mbichi.
 
1lita =19km, hapa umetudanganya mzee baba [emoji848]
Chakushangaza unasema nimekudanganya wakati wewe unayejua inaenda l/km ngapi husemi halafu hizo km sijatoa kichwani mwangu mimi bali nimesoma kwa waliofanya review ya hio gari lakini Tatu Lita 1 inaweza kutembea Km 19 Kama unasafiri Kwenda umbali mrefu kama Mkoa hakuna kinachoshindikana.

Nne mmekalili kuwa Gari yenye cc kubwa inakula sana mafuta wakati sio hivyo Magari ya kuanzia mwaka 2005 kuendelea mfumo wake mwingi ni wa umeme kuliko mafuta kwasababu mafuta yanapounguzwa hutoa carbon emission ndio maana watengenezaji wa magari wanajitahidi sana kuendana na kasi ya teknolojia katika matumizi ya mafuta ili kupunguza hizo carbon emmission

na ndio maana magari mengi ya kisasa ulaji wake wa mafuta ni mdogo ukilinganisha na ya zamani kwasababu Hizo kwahio usikalili eti cc kubwa ndio ulaji mkubwa wa Mafuta Penda Kujifunza na unapopinga Pinga kwa data

@ Mavado Nenda google ukaisome hio gari vizuri ndio urudi kupinga na kusema nimekudanganya
 
Hii ndinga iko vizuri,ukiwa na mzunguko mzuri Wa chapaa si vibaya kuwa nayo.
 
Mad Max, Mkuu kuhusu gari za Kijerumani aina ya VW Touran vipi? Kuna yenye CC 1980,1380 na 1580, je ipi inafaa? Je ina maintenance Cost za bei juu kama hao BMW?

Tafadhali kama una info za ubora,matatizo na the like,tunaomba utusaidie kutoa darsa huru ili iwe na faida kwa wote. Kuna jamaa yangu alinunua VW Touran ya CC 1980 huu mwaka wa 4 anadunda nayo,ila alinitahadharisha kuwa zile za cc 1580(1600) siyo nzuri, sikuelewa nadharia yake!
 
Mkuu kuhusu gari za Kijerumani aina ya VW Touran vipi? Kuna yenye CC 1980,1380 na 1580, je ipi inafaa? Je ina maintenance Cost za bei juu kama hao BMW? Tafadhali kama una info za ubora,matatizo na the like,tunaomba utusaidie kutoa darsa huru ili iwe na faida kwa wote. Kuna jamaa yangu alinunua VW Touran ya CC 1980 huu mwaka wa 4 anadunda nayo,ila alinitahadharisha kuwa zile za cc 1580(1600) siyo nzuri,sikuelewa nadharia yake!
Mkuu,
Sipo vizuri sana kwenye Volkswagen cars kabisa ni kwasababu sijawahi fikiria kuzimiliki ingawa zipo ninazo zitamani tu kwa macho ikipita.

Germany cars watu wanazipa marks za juu likiaga swala la reliability. Ila pia likija swala la running and maintenance costs, sana sana nchi zetu ambazo kuwapata dealers specialized inakua ngumu.

Japanese cars zipo easy ku run na maintain kwa sababu nyingi, ikiwemo idadi ya hizo gari, availability ya spare parts na mafundi.

Ila kama umeipenda VW mzee baba chukua tu najua spare na mafundi hautakosa. Chukua kitu roho inapenda kaka.
 
LJ BLOG,
Mzee baba umeona 19mpg we ukajua ni 19km/l,hii sio sahihi.

19mpg ukii convert maana yake ni 12.38L/100 km ambayo pia maana yake ni 1lt/8km kumbuka gari hio inakua tested under ideal condtions so ukiileta kwenye mazingira yetu halisi ulaji wa wese lazima uwe chini ya hapo.
 
Subaru ipi? Kama Forester ya mwaka 2009 na kuendelea yenye CC2500 hivi,ikiwa na 240kph,hiyo athlete yako itaachwa kama mtoto mdogo. Na hawa Fuji Heavy Industry ni kiboko,magari yao hupata nguvu ukikanyaga kidogo mafuta,wakati wewe unaitafuta 80kph ndani ya sekunde 3 mwenzako anatafuta 100kph. Ndo utofauti unaanzia hapo. Kwamba Subaru ya cc 1990 inapata speed kubwa ndani ya muda mfupi(acceleration) kwa muda mfupi though the same Speed at maximum wote gari ina 180kph.

hio forester ya 2009 yenye cc 2500 Turbo ina only 263 HP haiwezi kufuata moto wa hio majesta yenye 339 HP hata kidogo.

Labda hio forester iwe moded na makorokoro kibao lkn kama iko stock,itaachwa kama imesimama vile.
 
Kwa hapa Dar zipo chache sana hii nikutokana na CC kubwa na ulaji wa mafuta,anayemiliki hiyo ndinga ujue anajitambua kwenye pesa
Kuna majesta moja ipo pale kariakoo mtaa wa gerezani ni CC 4290 na kuhusu engine majesta nyingi ni cylinders 6
Rekebisha hapo kwenye 6. Majesta nyingi zina 3UZ-FE engine ambayo ni V8
 
LJ BLOG,
Majesta is just a crown on steroids...Chukua majesta kama mfuko waruhusu japo angalia model mpya
 
Back
Top Bottom