Baada ya Kuendelea kuitafiti Toyota Crown Majesta hususani Uzao wa Nne toleo la Mwaka 2004 ambayo ina engine code 3UZS-FE V8 kiukweli nimetokea kuikubali kutokana na vitu vingi baada ya kuona ni gari yenye Airbags 9 nadhani inaweza kuwa moja kati ya gari chache za TOYOTA kuwa na AIRBAGS nyingi maana nyingi zina airbags mbili.
Lakini Seat zake nimezipenda kutokana na kuwa za umeme lakini pia na heater kupelekea Dereva na abiria kuwa more comfortable pale wanapohitaji heater kwenye seat zao. Lakini pia Kuwa na Air Purify nayo imekuwa kigezo kizuri sana kwenye gari hii, Lakini pia Kuwa na DUAL A/C dereva au abiria akitaka kipupwe kikali anajichagulia huku dereva akichagua kiwango chake cha kipupwe bila kuathiriana na abiria.
Lakini mfumo wa sunspension zake nimeupenda pia kutokana na Kuwa na Option za High, Height na Normal lakini pia sunspension zake ni za umeme ambapo zina option mbili za SPORT na Normal lakini Pia taa zake za mbele ni Directional ambapo zinamulika pale ambapo unaelekea pindi ukikata kona zinamulika upande unaokata kona. Pia ni Gari yenye Cooler Box kwenye Seat za nyuma za abiria
Kutokana na Kuwa na Nguvu, Speed na Comfortability Hii gari inazalisha nguvu ya 253 kW (339 hp; 344 PS). Hapa sasa nadhani Wale wapenda mbio, Basi hili linawafaa kwasababu hata ground clearance yake ni nzuri pia. Kibongo Bongo ukiamua kuiagiza inaweza kukugharimu kiasi cha Shilingi za Kitanzania Mil 16
Kuhusu Mafuta sidhani kama inaweza kuwa tishio kihivyo kwasababu kwa mujibu wa taarifa zao wanasema kuwa Lita Moja inaenda mpaka KM 18 - 19 . Tukiogopa sana Mafuta Tutashindwa kumiliki Magari mazuri aisee
Kwenye mbio nadhani mnyama huyu anaweza kuchuana na Land Cruiser V8 na aina nyingine za SUV lakini hizi sedan nyingi tu zitakuwa zinasoma namba kwa huyu Mnyama Aisee
View attachment 861020
View attachment 861021
View attachment 861022
View attachment 861023