Naomba kujulishwa mfumo wa hedhi ulivyo

Naomba kujulishwa mfumo wa hedhi ulivyo

Baada ya kusumbuka sana kusaka mtoto nilienda hospital nikapewa muongozo huu
Ipo hivii

Siku ya kwanza mke/demu wako anapoingia hedhi unaihesabu kama 1, siku ya pili ni 2 mmpaka cku 10, hapo mwanamke hawez kupata mimba

Baada ya hapo kuanzia siku ya 11 tangu hedhi ianze mpaka siku ya 15 hapo ni khatari, ni mimba tu, ila siku ya 14 ndio PEAK,hapaongopi hapo (ovulation)

Kuanzia 16-mwisho atakapoanza tena ni hakuna mimba , cheki hiyo picha hapo chini kwa msaada zaidi

View attachment 436975
Mkuu hyo Dr wako alikuwa wa mwendo kasi, mrudie tena akafafanue juu ya danger zone, huwa ni nine days na so pungufu,... Hzo 14ni kama unataka kupata MTT Wa kiume na za mwisho ni Wa kike
 
Mkuu hyo Dr wako alikuwa wa mwendo kasi, mrudie tena akafafanue juu ya danger zone, huwa ni nine days na so pungufu,... Hzo 14ni kama unataka kupata MTT Wa kiume na za mwisho ni Wa kike
ni siku 8 mkuu ndio za danger zone
 
Muhimu kwanza ni kujua mke wako (au mwanamke wako sijui mkuu) ana mzunguko wa siku ngapi. Wapo wa siku 28, 35 etc. Kufahamu hasa hesabu kuanzia siku ya kwanza ya hedhi ya mwezi huu hadi siku ya kwanza ya hedhi ya mwezi ujao. Wengine hesabu zao ziko irregular, hapo ni mtihani kidogo. Wengine ni regular, yani mathalan, siku 28 kwa kila mwezi. Tutapigia mfano kuwa mtu wako ana mzunguko wa siku 28, siku ya kwanza ya mzunguko ikiwa ni siku ya kwanza kupata hedhi (na SI siku ya kwanza ya mwezi kwenye kalenda. Yani sio tarehe 1 Januari, au 1 Februari, ingawa labda ya mtu wako ikawa inaingiliana na tarehe za kalenda, hilo sifahamu). Sasa basi, kufahamu lini ni siku za hatari kwa mtu wako (siku za Ovulation...yani yai kutoka), chukua idadi za siku katika mzunguko wake, ambazo hapa tutaassume kuwa siku 28, toa siku 14 kutoka hapo (28-14=14). Jibu letu ni 14, hivyo siku ya 14 tangu aanze kupata hedhi ndiyo siku atakayo ovulate (yani kutoa yai). Ukikutana naye faragha katika siku hiyo kuna uwezekano mkubwa akabeba mimba. Aidha, wakati mwingine huwa mzunguko hauko sawa, hivyo kitaalamu unaongeza siku 2 mbele na unatoa siku 2 mbele, na kwa hivyo ukikutana naye siku ya 12, 13, 14, 15, 16 zote ni siku za hatari. Literature nyingine zinataka uongeze siku 3 mbele na siku 3 nyuma (iwe tarehe 11, 12, 13, 14, 15, 16, na 17). Na sababu nyingine kubwa ya kuongeza siku 2 (au 3) mbele na nyuma ni kuwa sperm (seli ya uzazi ya kiume) inao uwezo wa kukaa kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa siku 3 (masaa 72) ikiwa hai na ovum (seli ya uzazi ya mwanamke) inao uwezo wa kukaa hadi siku 2 (masaa 48) kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke ikiwa hai. Hivyo basi, unaweza kukutana faragha na mtu wako leo, mathalani ni siku ya 12 ya mzunguko wa mwanamke wako, sperms zako zikakaa siku 2 hadi 3 zikiwa hai, zikaja kuchavusha (kufertilize) ovum yake baada ya siku 2 na ukabaki unashangaa kwanini amepata ujauzito. Na kama kuongezea tu, mwanamke anapofikia kwenye siku ya kuovulate (kutoa yai) huwa ana mabadiliko fulani ya kifiziolojia yanayompata. Mfano, atakuwa na joto la mwili lililopanda kiasi, atakuwa ana hamu kubwa zaidi ya kukutana faragha na mwanaume n.k, kutokana na mabadiliko ya kihomoni anayoyapata mwilini mwake wakati huo. Natumai nimejibu swali lako ipasavyo mkuu.
 
Aidha, ili kuondoa confusion na kutoa faida kwa wengi wetu zaidi. Kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 35, siku ya hatari (ya Ovulation) itakuwa siku ya 35-14=21 (14 ni fixed). Hivyo ukiongeza siku 2 mbele na 2 nyuma inakuwa siku ya 19, 20, 21, 22, 23. Kama tukiongeza siku 3 mbele na 3 nyuma inakuwa siku za 18, 19, 20, 21, 22, 23 na 24.
 
1479669807219.jpg
 
Muhimu sana kujua hiyo binti, LNMP ( last normal menstrual period) ni swali ambalo ni muhimu kuulizwa kwa kila mgonjwa wa kike aliyevunja ungo anapofika hospitali kwa kuwa kuna magonjwa ya kike yana interaction na menstrual periods
i do agree with u lakini ndio dr itabidi anivumilie nianze kuvuta kumbukumbu
 
mimi ndo tarehe zimenishinda
sijui kuzihesabu kabisaaa.

mwezi wa 9 tarehe 10
wa 10 tarehe 30
huu wa 11 sijui ndo itatoka wa 12 katikati[emoji26][emoji26][emoji26]
 
Nimekuwa nikikutana na dem wangu kwenye siku zake za hatari lakin hakupata mimba, lakin uwezo wa kubeba mimba anao na mimi uwezo wa kufetilize ninao, sasa hapo tatizo linakuja wapi?
 
Baada ya kusumbuka sana kusaka mtoto nilienda hospital nikapewa muongozo huu
Ipo hivii

Siku ya kwanza mke/demu wako anapoingia hedhi unaihesabu kama 1, siku ya pili ni 2 mmpaka cku 10, hapo mwanamke hawez kupata mimba

Baada ya hapo kuanzia siku ya 11 tangu hedhi ianze mpaka siku ya 15 hapo ni khatari, ni mimba tu, ila siku ya 14 ndio PEAK,hapaongopi hapo (ovulation)

Kuanzia 16-mwisho atakapoanza tena ni hakuna mimba , cheki hiyo picha hapo chini kwa msaada zaidi

View attachment 436975
Yan kati ya formula zote nilizowahi kufundishwa hii ndo ilikua rahisi
 
Hiv wataalamu kuna uhusiano na wowote kama mama ananyonyesha kwa wakati mtoto unaweza kula mzigo na asishike mimba
 
Na mimi ngoja nipate msaada kupitia uzi huu mwezi huu nimeingia period tarehe2-6 siku zangu za kushika ujauzito zitakuwa lin nisaidieni ndugu
 
Back
Top Bottom