1. Malimbikizo ya mshahara, yataendelea kubaki kama deni. Kwa kuwa haya hulipwa kama mshahara na kwa kuwa baada ya kufukuzwa kazi mshahara umekoma, malimbikizo hayo yatakumbushwa kwa barua kwenda kwa mwajiri kama madai na yatapaswa kulipwa kama madai mengine yalivyo serikalini (kama fedha za kujikimu nk)Wasalaam, naomba kujuzwa haki za mtumishi wa Serikali ambaye amefukuzwa kazi huku akiwa na Malimbikizo ya Mshahara ambayo hakulipwa. Je utaratibu ni upi?
Na kipindi aliposimamishwa alikuwa akilipwa Nusu ya Mshahara je baada yabkufukuzwa analipwa kiasi cha nusu alichokuwa akikatwa wakati wa uchunguzi wa Shauri lake?
Maelezo muafaka.Nina swali la nyongeza:1. Malimbikizo ya mshahara, yataendelea kubaki kama deni. Kwa kuwa haya hulipwa kama mshahara na kwa kuwa baada ya kufukuzwa kazi mshahara umekoma, malimbikizo hayo yatakumbushwa kwa barua kwenda kwa mwajiri kama madai na yatapaswa kulipwa kama madai mengine yalivyo serikalini (kama fedha za kujikimu nk)
2. Kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi za Umma za mwaka 2003, Nusu ya mshahara iliyokuwa inabaki wakati wa kusimamishwa kazi hulipwa kwa mtumishi endapo tu makosa aliyotuhumiwa nayo yatashindwa kuthibitishwa. Anapokutwa na hatia na kufukuzwa kazi hastahili kulipwa ile nusu ya mshahara ambayo hakulipwa.
3. Haki nyingine ni kulipwa fedha za kusafirisha mizigo au kupewa usafiri utaosafirisha mizigo yake kwenda nyumbani kwake (domicile). Mizigo isiyozidi tani 3, kulipwa nauli ya kumsafirisha yeye, mwenza wake na watoto wake wasiozidi 4 (kama wapo) kwenda nyumbani kwao mtumishi
Ikiwa aliajiriwa kama mtumishi asiye afisa (digrii) anapewa michango yake yote, ila kama alikuwa ni afisa (digrii) anapata 1/3 kama sikosei ya michango yake na ikipita miaka 3 hajapata ajira atafikiriwa kupewa michango iliyobaki (yote au kiasi tu)Maelezo muafaka.Nina swali la nyongeza:
Kuhusu mchakato wa fedha za mfuko wa hifadhi ya jamii anapataje?I nakokotolewaje?