Naomba kujuzwa kuhusu gari aina ya Vauxhall

Mimi ni 'mtaalamu' wa gari za Euro especially UK nakwambia kifupi tu USINUNUE.
Mkuu unaweza ukashare na sisi hiyo elimu yako na kwamba kwanini asinunue? Maana umesema kuwa wewe ni expert wa European Cars ila sasa kwanini hii hapa umeipa big NO as opposed to Opel, Discovery na Audi ambazo huwa unazipa positive review.
MCHANGO WAKO TAFADHALI
 
1.Not reliable
2.Spares bongo hamna

Ikiharibika,ambalo ni jambo la kawaida, utapata wapi spares?
Nimeendesha hio gari UK brand new ya kampuni. Ilikuwa diesel engine gear sita manual. Inakimbia,iko stable. Ni moja ya cheap cars UK lakini ikishachoka itakupasua kichwa.

Nilioendesha iliuzwa ikiwa na 70,000miles maana ilishaanza kusumbua.
Katika gari za UK epuka Vauxhall, Rover na Freelander 1(98-2005).
 
Mkuu labda ununue ukakate skrepa bongo ukitaka gari nunua Toyota tu kwa kule kenya wao wanapenda Nissan sana
 

Nasubiria ufafanuzi kwenye SUZUKI
 
Achana na European cars utajuta
Acha akili za kimasikini mkuu.
Hivi european car unaweza fananisha na hizo asian car mkuu.ww mwenyewe sio kwamba hupendi kuendesha european car sema ndio hivyoo usawa hauruhusu tuu
 
Acha akili za kimasikini mkuu.
Hivi european car unaweza fananisha na hizo asian car mkuu.ww mwenyewe sio kwamba hupendi kuendesha european car sema ndio hivyoo usawa hauruhusu tuu

European cars ni nzuri, ila kwa mazingira ya kinyumbani ni shida. Hizi gari za kizungu VW, Peugeot, BMW, Citroen, Vauxhall na nyingine zinatengenezwa kwa namna ya hali ya hewa yao ilivyo. Pia zinakuwa na Life span. Nyingi zikishafikisha miles 70,000 basi. Wenyewe wana schemes zao wanarudisha kwa dealer wanapewa gari nyingine.

Ila Gari za Japan ambazo zipo ulaya ni Nzuri. Mfano Carina E, Avensis, Hilux etc.

Achana nao hiyo itakuumiza kichwa.
 
Toyota mkombozi was wanyonge
Sidhani kama ni kweli ukombozi huo sijajua ww wauzungumziaje??..mtu anaye kunyonya /kukula kila siku kidogo kidogo ndio mkombozi wa wanyonge??.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…