Naomba kujuzwa kuhusu Uchumi wa Tanzania

Watanzania ndiyo njisi tulivyo, baadala ya kuchangia maada unapost mawazo mgado kabsa
hapo nikija na thread ya mapenzi, watu wangetoa point.

maskin nchi yangu iliyojaa vijana wavivu...
Mkuu usipende kuletewa ulitakiwa ufanye research yako binafsi.
Najua akili yako imewaza mambo mengi sana na yenye maana ila kinachokuangusha ni uvivu.

Hivi unafikir akina newton,karl marx na wengineo wangekuwa na uvivu kama wako hii dunia ingekuwaje?

Jaribu kujijengea hali ya kuwa mtafit utafika mbali sana.
Ukitegemea mawazo ya akina Bull dog na Mgirik tutakudanganya bure na utaamin kitu cha uwongo
 
Last edited by a moderator:

shukurani sana ndgu yangu kwa kutuonya vijana wavivu kama mimi, lakn tunapenda kuendelea,!!

kuleta huu uzi hapa nina uelewa wa kwamba jf,, ina watu wanaoitwa great thinker,
kwa maana hiyo mategemeo yangu nitatoka na point kubwa sana humu jf na kuweza kukamilisha research kamili,

pia kupitia uzi huu watu watapata namna ya kujadili na kuuelewa vizuri uchumi wa taifa letu..

asante!!!
 
Last edited by a moderator:
Uchumi wa tanzania umeongezeka kwa kasi sana kwa asilimia 7.5 hivyo umeufanya tanzania kuwa kifua mbele miongoni mwa nchi nyingi sana!

Mkuu unaweza ukanielezea ni sababu zipi? zilozosababisha kupanda kwa uchumi wa tz 7.5
 
1,Naomba kufahamishwa, ni wilaya ngani hapa Dar es salaam ambayo inachangia pato kubwa kwa taifa letu na ni kwa nini?

Ilala, viwanda, biashara, bandari ...

2,kati ya waafanyabiashara, wakulima, wafanyakazi mbalimbali na wajiriwa ni kundi ngani la watu kati ya hao wanachangia pato kubwa kwa taifa na ni kwa nini?

Wakulima, mchango wao kwa nchi maskini kama Tanzania haupungui 35% GDP.

3,ukiachana na Dar es salaam ni mkoa ngani mwigine unachangia pato kubwa kwa taifa. je? vipi miundo mbinu imeimarishwa katka mkoa huo

wilaya nafkr tunduma, mkoa sina uhakika ila utakuwa mwanza.

4,Ni kwa nini? wakulima wadogodogo hawaruhusiwi kwenda kutafuta soko nchi za nje,? ili hali wafanya biashara wakubwa wanaruhusiwa.

Rukhsa imetolewa, wiki hii, uwezo wako beba kabichi zako ukauze kongo.

Ila inakuwa hivyo kwa usalama wa nchi ni rahisi kuthibiti wafanyabiashara wakubwa.
Nchi masikini yenye upungufu wa chakula ni kama mtu mzima kukosa nguo maungoni ukiwa ukweni.

5,Ni mkoa gani wenye madini na maliasili nyingi sana,? na maendeleo yao,, yakoje katika huo mkoa...?

Swali hili haliwezekani kujibika mpaka lirekebishwe, umahususi wake ujulikane. Madini na maliasili na maendeleo vyote vina mapana kimaana hivyo uvipanga, seti unayopata ni isiyoisha.

Chuma na makaa ya mawe ludewa inaweza kuwa na wingi kuliko Tanzanite lakini chini kwa thamani.

Mtwara isingekuwa Mh. Mkapa labda kusingekuwa na barabara mpaka leo, tungejenga bomba tu. Geita tunajenga zahanati kutuliza kelele na barabara kidogo.
Ludewa barabara lazima sasa tutatoaje makaa na chuma...

Miundombinu yawezekana kuwa ni chaguo, lazima au kipaumbele.

6 Ni kwa nini ofisi nyingi za umma ziko Dar es salaam,??

Mji wa kibiashara (serikali nayo inafanya biashara!), idadi ya watu wanaohitaji huduma ni kubwa, na ni mji wenye miundombinu zaidi kuliko iliyobakia.

7,Ni asilimia ngapi? ya pato la taifa linalotokana na utalii

2013 umeshapewa.

"Hivi kuna tofauti ya kuwakilisha na kuwasilisha?"
 
...

2,kati ya waafanyabiashara, wakulima, wafanyakazi mbalimbali.., wajiriwa na wasomi ni kundi ngani la watu kati ya hao wanachangia pato kubwa kwa taifa na ni kwa nini?

Wakulima, mchango wao kwa nchi maskini kama Tanzania haupungui 35% GDP.

Nakushukuru sana kwa msaada na upeo wako wa hali ya juu!! kuhusiana na uchumi wa nchi yetu.

umenifanya nitoe machozi kabisa kuhusiana na jibu lako hapo kwenye red,

pamoja na kwamba wakulima huchangia pato kubwa sana kwa taifa letu,!!,,
je? mkulima anaruhusiwa kuchukua mkopo serikalini ili kuendesha shughuli zake.?
maana wasomi ambao hawana msaada wowote katika pato la taifa kila siku wanapewa mikopo,!!

na kama mkopo upo utaratibu wake ukoje? ili kuupata.
 
1,Naomba kufahamishwa, ni wilaya ngani hapa Dar es salaam ambayo inachangia pato kubwa kwa taifa letu na ni kwa nini?
Ilala, viwanda, biashara.na bandari

kama nitakosea
wadau naomba mnisaidie kwa ufahamu wangu mimi bandari najua iko katika wilaya ya TEMEKE.

3,ukiachana na Dar es salaam ni mkoa ngani mwigine unachangia pato kubwa kwa taifa. je? vipi miundo mbinu imeimarishwa katka mkoa huo

wilaya nafikiri tunduma, mkoa sina uhakika ila utakuwa mwanza.

tunduma ina vitu ngan? vinavyoifanya kuchangia pato kubwa kwa taifa,?

kama ni Mwanza,
tukiachana na Geita ambayo kwa sasa ni mkoa,. MWANZA ina vitenga uchumi vipi? ambavyo huchangia pato kubwa kwa taifa

ASANTE SANA
 

Naomba wakuu mwenye uelewa wotote na hili swali anijuze,
 

mkulima ni mpangaji kwenye ardhi inayomilikiwa na serikali.
Hivyo ukiwa umepanga kwenye nyumba huwezi kuiwekea rehani, si yako.

Ni suala mtambuko, linaloendana na historia ya siasa na sera zinazoongoza uchumi.

Kiufupi nyuma ya 90 dar ardhi za bure zilikuwepo km 40 toka katikati ya jiji, kwa kuwa ardhi haikuwa na thamani.
Kwa wakati huo ukiwa na ardhi ukataka kukopa ununue bito ni sawa na sasa kuweka rehani pasi ukakope ununue vitz.

Sera zimebadilika ardhi inaingizwa kwenye mfumo unaoipa thamani, ukiwa na hati kwenye miji unapata mkopo, shamba bado ni changamoto mpaka liwe na mazao ya kudumu ya muda mrefu sema kama miti ya mbao n.k.

Pinga ukinia mambo mema kwa ujio wa benki ya wakulima, ila usitegemee sana kwa kuwa wakikiuka misingi ya uchumi benki itakufa kama crdb, thb ...
 

Asante sana mkuu, lakn ushauri wako ingekuwa vyema sana kama ungekuwa jukwaa la lugha
 
Asante sana mkuu, lakn ushauri wako ingekuwa vyema sana kama ungekuwa jukwaa la lugha

Samahani sana kuna mtu alichangia mwishoni akaomba ajuzwe tofauti ya kuwakilisha na kuwasilisha...lakini naona nilipomnukuu ili nimjibu naona kama amefuta ile post yake ....pole sana kwa usumbufu.
 

pleo asante umetusaidia wengi nilikuwa sielewi kwanini hatukopesheki. Kwa majibu yako inaonekana ili mkulima wa mazao alime kibiashara na kutanuka ni sharti awe na biashara nyingine au mfanyakazi ili kuongeza mtaji wake au kukopa benki. Kwa maneno mengine ukulima kama pekee hautambuliki kama kazi. Kwa mantiki hii hatushangai kuwa na wachuuzi tu, vi fremu kila mtaa, ikipanuka anahamia Kkoo, ilala nk. Wote ni mpesa, chipsi mayai, duka vyakula, mama lishe, salon, bodaboda. Ndio maana watoto wa kulima wanauza ardhi waje tubanane uku. Cha kusikitisha benki inazitambua hizi ingawa si ajira zenye tija na ndio stanbic ilipolizwa Kkoo. Taifa hili uchumi ungekua sana wakulima wakiwezeshwa.
 

Mama joe. ni jambo la kusikitisha kweli, mr pleo amesema wakulima ndiyo wanachangia pato kubwa kwa taifa kupita, hata wasomi, na waafanyabiashara.


lakn cha kusononesha serikali yetu inatunyanyara sana.
 
Umewaambia ukweli. Ndio tabia yao.
 
Mama joe. ni jambo la kusikitisha kweli, mr pleo amesema wakulima ndiyo wanachangia pato kubwa kwa taifa kupita, hata wasomi, na waafanyabiashara.


lakn cha kusononesha serikali yetu inatunyanyara sana.

yeah haitutambui mchango wetu ila mdogo mdogo tutafika tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…