Naomba kujuzwa Mahitaji ya Vifaa kwa ajili ya 'Car Diagnosis'

Naomba kujuzwa Mahitaji ya Vifaa kwa ajili ya 'Car Diagnosis'

Mfano kama hiyo picha hapo.

15852445252331807118612450768534.png
 
Ninaweza kukupatia generic code reader OBD2 ambayo inasoma codes zote za matatizo ya injini kwa euro 100 toka EU

Nashukuru mzee tunaweza fanya biashara ila kwanza nahitaji kujua vifaa hitajika kwanza, je nikinunua hii ndio nimemaliza kila kitu!?
 
Nashukuru mzee tunaweza fanya biashara ila kwanza nahitaji kujua vifaa hitajika kwanza, je nikinunua hii ndio nimemaliza kila kitu!?
Kwa kuwa sijui nia yako siwezi kusema. Ila hako kamashine huku kanamuingizia mtu euro 20 kusoma code tu. Na kwa gari za sasa hiyo ni hatua tosha kutengeneza magonjwa ya miss, kuwaka kwa tabu kuzimaghafla n.k.
 
Nia yangu ni kama inavyojieleza, nimepata hili wazo halafu sijui a,b,c kuhusu hiki kitu, tushazoea gari zetu kutengeneza kwa kuhisia, nilikuwa kwa fundi, ndio nikapata wazo hili, msaada wa kwanza google nikacheki haraka “car diagnosis” nikasoma juu juu nikakuta vifaa vingi na kampuni tofauti kina Foxwell na wengineo

Nikaona nije na huku nitaambulia mawili ma3, nahitaji maelezo zaidi, ni kitu ambacho nimevutika kufanya ila sina a,b,c zake
Nahitaji kujua vifaa pia na maelezo yake.
 
Kwa kuwa sijui nia yako siwezi kusema. Ila hako kamashine huku kanamuingizia mtu euro 20 kusoma code tu. Na kwa gari za sasa hiyo ni hatua tosha kutengeneza magonjwa ya miss, kuwaka kwa tabu kuzimaghafla n.k.

Upo wapi mkuu!? Huko kwenye kuingiza euro 20!?
 
Upo wapi mkuu!? Huko kwenye kuingiza euro 20!?
Europe kaka huku kila kitu ni ghali, ndiyo maana kama ulishawahi kusikia tunatupa magari sababu ni hiyo. Ukipeleka gari garage ni eur 20 kusoma code tu, ukitaka watengeneze ni euro 100 kwa saa watakayofanya kazi.
 
Nashukuru mzee kwa ushirikiano wako, jf miyeyusho hainipi notifications tena.
 
Tukirudi kwenye mada, ukiwa na diagnostic car code reader mengine ni hivyo vifungulio( spana ) na vifaa vingine vya kazi za nguvu

Sawa mzee nimekusoma.

Sasa car code reader ipi ni best!

Nilipocheki nilikutana nazo nyingi
Tuchukulie mfano kampuni ya Foxwell nikakutana na tns 301, kuna 510 kuna mpaka 650 huko sijui zinatofautiana nini!?
Je ni wingi wa kusoma codes au ama kuna hizi za kusoma eneo fulani tu kuna hizi zinadeal na eneo fulani kiasi nikitaka kununua ninunue zaidi ya moja!?
 
Tukirudi kwenye mada, ukiwa na diagnostic car code reader mengine ni hivyo vifungulio( spana ) na vifaa vingine vya kazi za nguvu

Masuala ya spana, atakuwepo fundi, kiufupi mie siujui ufundi wa magari, kagari kangu zaidi ya kubadili oili na vidogo dogo sijui zaidi.

Hii kwangu niliona kama fursa, nikaona km nitakuwa nacho halafu nikatengemeza connection na mafundi wengi wa huku nikahisi km kuna uwezekano wa kupiga piga visenti! Mpaka sasa nimeongea na mafundi km wawili hivi.

Ndio maana wazo hili nikalisukuma hapa nipate mawili ma3, unaweza ukaona ninidea mpya kumbe wenzio waishafanya hapa mjini, ama wanafanya! Nikapata zaidi na zaidi.
 
makaveli10,
Kuna huko kuzidiana vitu kiasi lakini in general code reader zote ni standard zimetengenezwa kutakiwa kusoma OBD2 zote. Na hii ilitakiwa iwe kuanzia gari za 2001 hadi sasa. Hiyo ni kwa mikataba ya nchi zote kubwa wanazotengeneza magari.

EU waliweka sheria ili yeyote anayetaka kuuza gari lake Ulaya ni lazima akubali hivyo. Ila code readers hizi hazisaidii kuangalia mambo yaliyo nje ya engine ya gari hapo unabidi kupata software spacific ya gari husika.
 
Kuna huko kuzidiana vitu kiasi lakini in general code reader zote ni standard zimetengenezwa kutakiwa kusoma OBD2 zote. Na hii ilitakiwa iwe kuanzia gari za 2001 hadi sasa. Hiyo ni kwa mikataba ya nchi zote kubwa wanazotengeneza magari. EU waliweka sheria ili yeyote anayetaka kuuza gari lake Ulaya ni lazima akubali hivyo. Ila code readers hizi hazisaidii kuangalia mambo yaliyo nje ya engine ya gari hapo unabidi kupata software spacific ya gari husika.

Ewa! Umegusa sehemu nyeti nilikuwa na maswali mawili! Nimeona ona tu hii kitu OBD kuna OBD1 naona ipo na OBD2 sijui kama zipo nyingine ni nini hizi hasa!

Kuna kaswali kengine nilitaka kuuliza lakini naona kama umekajibu hapa kwamba”hizi mashine hazichagui gari za ulaya wala asia, ambazo hapa bongo ndio nyingi zaidi.”

Mambo yaliyo nje ya engine ya gari!!?
Je hakuna mfumo wa kuingiza gari sehemu, halafu huku gari inaonesha magonjwa yoote!?
 
Mfano kama hiyo picha hapo.

Hii model name yake ni ipi!? Na je hiyo euro ni mpaka inanifikia mie mkononi haluna gharama nyingine!? Functions zake ni zipi, ukiweza niorodheshea itakuwa rahisi.
 
Hii model name yake ni ipi!? Na je hiyo euro ni mpaka inanifikia mie mkononi haluna gharama nyingine!? Functions zake ni zipi, ukiweza niorodheshea itakuwa rahisi.
Ivi vidude nimewai shuhudia Kama vitatu tofauti tofauti na kila kimoja kilikua na changamoto yake

Na viliagizwa Ali Express

Chakushauri ndugu nu kufatilia kwakina kujua ni kampuni gani itakua bora na ya uhakika kwani vile vilikua vikichagua magari mara ya kwanza nilijaribu kwenye vitz ,alteza,na funcargo kika goma chapili nacho kilikua ivo ivo ila Cha tatu kilikubali kweny nisan extrail

Na vyote vilivo goma error ilikua nikwamba kinashindwa ku communicate na ECU

Jamaa mmoja akashauri tunu ue vele vikubwa ambavy vina had tablet Sasa sija pata uhakika Kama kweli ndo solution

Sent using Jamii Forums mobile app
 
i 37,
Nashukuru kwa mchango mzee

Hivyo vi3 vilikuwa vya kampuni zipi kaka?
Je zenye tablet ni zipi!?

Nilijaribu kutafuta vifaa bora mtandaoni, kuna vifaa kama vi5 hivi vimetokea mara nyingi zaidi katika matokeo tofauti tofauti.

Nadhani wadau wengi watatokea tutapata pata dondoo zaidi.
 
Back
Top Bottom