Labda maeneo unayokaa fuatilia magari gani sana ndio yapo mengi,au unataka kubase na magari yapi.
maana vifaa vya diagnosis vinatofautiana bei kutokana na aina za magari,uwezo wa kifaa,na functions(mf😛rogramming,adaptations,reset)
Ila kwa ushauri kama uko hapa bongo tena labda ni nje ya mji,nunua basic ambazo zinapima magari mengi hasa ya kijapan.
Kama launch,autel, ambazo za uhakika kuanzia laki 9 hadi juu,
Za bei ya chini nzuri kama za laki 2(~usd100) au chini ya hapo ni code reader mfano za check engine tu,abs,service reset.
Note: kama unatumia wewe au unawauzia watu,jua kwamba hakuna machine ya kupima gari zote kama zinavyoandikwa kwenye matangazo ila zinajitahidi kwenye magari mengi.
Sent from my iPhone using Tapatalk