Naomba kujuzwa Mahitaji ya Vifaa kwa ajili ya 'Car Diagnosis'

Naomba kujuzwa Mahitaji ya Vifaa kwa ajili ya 'Car Diagnosis'

Kwa kawaida vile vya bei rahisi huwa havina uwezo mkubwa kama vyenye bei kubwa, swala siyo jina. Yaani ni sawa na simu mfano, simu zote tunaweza kutumia kupiga lakini yakija mambo mengine makubwa ktk matumizi ya simu, zile zenye bei juu ndiyo zinafanikisha kuliko za bei chee.
 
Hii model name yake ni ipi!? Na je hiyo euro ni mpaka inanifikia mie mkononi haluna gharama nyingine!? Functions zake ni zipi, ukiweza niorodheshea itakuwa rahisi.
Imaitwa Autophix OM129. Gharama hadi kisafirisha sijazifuatilia
 
Wazee wenzangu huku ninapokaa naona hakuna vifaa kwaajili ya Car Diagnosis. Je, nahitaji vifaa gani hasa nifungue ofisi ya hivi na itanigharimu kama kiasi gani?

Mshanajr RRONDO Bavaria
Wazo zuri mno... Jitahidi ulitimize. Magari ya sasa sio ya spana tena na kuna baadhi hata ukibadili tu betri inabidi kuchomeka mashine kuondoa errors
Mashine zipo kuanzia laki moja (online shopping) mpaka million mbili... Lakini kwa kuanzia unaweza kupata hata ya laki mbili sio mbaya

Jr[emoji769]
 
Hii inauzwa laki 5
7916842472107469886.jpeg
-408055166749287103.jpeg
-2086104778-1955959545.jpeg
28940211121606497.jpeg

Jr[emoji769]
 
Kwa kawaida vile vya bei rahisi huwa havina uwezo mkubwa kama vyenye bei kubwa, swala siyo jina. Yaani ni sawa na simu mfano, simu zote tunaweza kutumia kupiga lakini yakija mambo mengine makubwa ktk matumizi ya simu, zile zenye bei juu ndiyo zinafanikisha kuliko za bei chee.

Sahihi kabisa mkuu, nilitaka kujua bora zaidi, si unajua sitaki mambo ya kubahatisha mzee mwenzangu nataka nifanye vitu kiuhakika, sio nanunua dubwasha nakuja kupiga nalo picha tu huku.
 
Wazo zuri mno... Jitahidi ulitimize. Magari ya sasa sio ya spana tena na kuna baadhi hata ukibadili tu betri inabidi kuchomeka mashine kuondoa errors
Mashine zipo kuanzia laki moja (online shopping) mpaka million mbili... Lakini kwa kuanzia unaweza kupata hata ya laki mbili sio mbaya

Jr[emoji769]

Sawa mkuu.
 
#1 – BlueDriver Bluetooth Professional OBDII Scanner

#2 – Autel MaxiCOM MK808 OBD2 Scan Tool

#3 – Autel Maxisys Elite Professional Auto Diagnostic Tool

#4 – Autel Maxisys Pro MS908P

#5 – Foxwell NT510 BMW OBD1 & 2 Car Scanner and Code Reader

Wazee wenzangu Coolhigh Mshanajr

Katika kuhangaika nikakutana na hii list

Nimeona technician mmoja amesema hiyo namba 1 ni bora zaidi, bado naendelea kuifatilia.

Ila kuna jambo limenishitua kuna moja hapo imeandikwa 2 years free update!? Ina maana hizi machine inabidi uapdate mara kwa mara, je kama hizo hapo mlizonionesha zinahitaji updates!?
 
makaveli10,
Hizi mashine zipo za aina mbili au zaidi. Kuna ambazo unachomeka kwenye gari halafu inatumia bluetooth kuwasiliana na simu/ laptop, ambapo humo unapakua software yake ndipo ifanye kazi.

Aina hizo huwa zinakuwa na updates kwa kuwa zinasoma kutokea kwenye servers za hao wenye huo mfumo. Aina ya pili ni ya hand held device ambayo imekamilishwa kuwasiliana na OBD/ gari na kukupa jibu, hizo hazihitaji update.
 
Labda maeneo unayokaa fuatilia magari gani sana ndio yapo mengi,au unataka kubase na magari yapi.

maana vifaa vya diagnosis vinatofautiana bei kutokana na aina za magari,uwezo wa kifaa,na functions(mf😛rogramming,adaptations,reset)

Ila kwa ushauri kama uko hapa bongo tena labda ni nje ya mji,nunua basic ambazo zinapima magari mengi hasa ya kijapan.

Kama launch,autel, ambazo za uhakika kuanzia laki 9 hadi juu,
Za bei ya chini nzuri kama za laki 2(~usd100) au chini ya hapo ni code reader mfano za check engine tu,abs,service reset.

Note: kama unatumia wewe au unawauzia watu,jua kwamba hakuna machine ya kupima gari zote kama zinavyoandikwa kwenye matangazo ila zinajitahidi kwenye magari mengi.

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Sahihi kabisa mkuu, nilitaka kujua bora zaidi, si unajua sitaki mambo ya kubahatisha mzee mwenzangu nataka nifanye vitu kiuhakika, sio nanunua dubwasha nakuja kupiga nalo picha tu huku.
Unajua, wafanyabiashara wote duniani wanataka kujiongezea faida na faida. Hivyo hata watengeneza magari, walipoanzisha huu mtindo wa computer kwenye gari (USA), idea ilikuwa mwenye gari lazima alipeleke kutengenezea kwa mtengenezaji hata kwa kitu kidogo. Ndiyo EU wakaona kuwa siyo haki kumfanyia mtumiaji na kuweka hii sheria ambayo ilipelekea kuanzishwa kwa hiyo generic OBD 2 system ambayo watengeneza magari wote walitakiwa kuitumia.

Sasa, bado wanafanya uhuni kubania baadhi ya vitu ndiyo maana kuna baadhi ya readers zinaweza kukosa kusoma baadhi ya gari. Vilevile, niliweka bandiko awali hili lilifanywa hususan kwa gari zilizotakiwa kuuzwa ndani ya EU.

Kumbuka, kuna magari mengine yanatengenezwa kwa ajili ya masoko ya ndani tu, hasa wajapani, Korea, na USA. Aina hizo za magari huwa hazibanwi na hii sheria kwa hiyo kama injini yake haijatumika kwenye magari yaliyouzwa EU, most likely hizi readers hazitofanya kazi.
 
Hizi mashine zipo za aina mbili au zaidi. Kuna ambazo unachomeka kwenye gari halafu inatumia bluetooth kuwasiliana na simu/ laptop, ambapo humo unapakua software yake ndipo ifanye kazi. Aina hizo huwa zinakuwa na updates kwa kuwa zinasoma kutokea kwenye servers za hao wenye huo mfumo. Aina ya pili ni ya hand held device ambayo imekamilishwa kuwasiliana na OBD/ gari na kukupa jibu, hizo hazihitaji update.

Zipi nzuri zaidi mkuu

Je hiyo mashine yako ushajaribu katika gari ngapi tofauti tofauti!? Na matokeo yake je!?
 
fundibenz,

Mkuu, wewe ni fundi?

Maeneo ninayokaa gari zake nyingi ndio hizi za watz. Za kijapani nyingi kushinda za magharibi.

Hapa kwenye functions hapa nahitaji kujua kiundani zaidi.

Nipo bongo mkuu, sipo nje ya mji kiviiile, nipo hapa wilaya ya kigamboni tu mkuu.
Katika maelezo yako umeonesha kuna launch,autel n.k hizi zinapima magari, kuna mashine nyingine ni code reader, unaweza ukanielezea zaidi kuhusu hii kauli. Kupima gari na code reader.

Nataka nitumie mimi, lakini kama biashara, kwahiyo ikiwezekana, bajeri ikiruhusu ninunue hata 2 ama 3 ili nipate uwanja mpana.
 
makaveli10,
Mimi ni fundi,na nime base kwenye diagnosis na programming tu.kwa european cars,
Nina muda mrefu kwenye hii kazi,ukipata nafasi fika ofisini kwangu, naweza kukushauri na kukuelekeza zaidi na kukuonesha baadhi ya tools ambazo natumia.

Hakuna gharama,na ukifanikiwa kununua naweza kukuelekeza jinsi ya kutumia.
Karibu sana.

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Mkuu nitahitaji mawasiliano yako
Mimi ni fundi,na nime base kwenye diagnosis na programming tu.kwa european cars,
Nina muda mrefu kwenye hii kazi,ukipata nafasi fika ofisini kwangu,naweza kukushauri na kukuelekeza zaidi na kukuonesha baadhi ya tools ambazo natumia.

Ahsante kaka.

J3 inshaallah panapo uzima nitakuja mzee.
 
Back
Top Bottom