Naomba kujuzwa mazuri na mabaya ya Starlet

Naomba kujuzwa mazuri na mabaya ya Starlet

Mimi natumia Starlet kwa muda tu,na hii namba 4 umetudanganya..mimeshakua na Carina,Corolla,Rav4 old na hii Starlet..ni ka gari kagumu na kanakimbia vzr na matumizi siyo mabaya..engine yake ni imara maana ni kama inakaribiana na baadhi ya Carina engine.

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Ukubali ukatae injini yake sio vumilivu kama unachelwesha service, naongea hivyo sio kwa kubahatisha.

starlet ikizungusha biashara imeisha, tofaut na 1nz injin au 2nz, nilisha kuwa na starlet ilipo zungusha haikuweza kwenda umbali mrefu, ila 2nz ilizungusha bukoba baada ya kuweka oil fake, tukabadili oili na ikatembea had Dar, je starlet unadhan ingeweza kufanya hivyo.

Naongea hivyo kwa kuwa ni gar ambayo nimeishi nayo mkuu. Sasa kwa nn mtu ununue starlet ambayo inatumia mafuta mengi kuliko Allex au spacio new yenye cc 1496? Maana starlet nyingi ni 1330. Usiiteteee gari kwa kuwa unayo, starlet haiwezi lingana hata na vitz ya cc 1290

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nmeshakichukua wadau kazi yake kubwa kupeleka watoto shule na kurudi nyumbani, njia ni roughroad na lami,asanteni kwa ushauri....ila ntaitaji kuka pimp in pimp out,mpango wa kubwa na mpya hapo mbele mzee baba akilegeza noti...
IMG_20200528_183000.jpg

HOT
 
Dah mkuu unamenya sana basi. Hasa ukiwa mkoani ndio raha zaidi.

Natamani kama Corona iendelee ili mafuta yazidi kushuka kmmmk. [emoji23][emoji23][emoji23] yafike hata buku kwa litre wahuni tutambe juu ya mkeka.
Hivi hawa jamaa wanaouza mafuta wanatuona sisi mafala sana. Kwann mafuta yapo bei ambayo sio.... Me nilitaraji kwa sasa at least tungenunua petrol kwa 1500 hivi kwa lita ila wapo bado kwenye 1800
 
Hivi hawa jamaa wanaouza mafuta wanatuona sisi mafala sana. Kwann mafuta yapo bei ambayo sio.... Me nilitaraji kwa sasa at least tungenunua petrol kwa 1500 hivi kwa lita ila wapo bado kwenye 1800
Hahaha wanazingua ila huku nilipo Total ni 1700 msimamo.
 
Kwa kuanzia gari nzuri sana au kama una mishe za hapa na pale kwa mjini ni nzuri sana. Kumbuka hakuna stalert mayai, zote ni chuma.

Spea zake zinapatikana vizuri tu.
 
Ukubali ukatae injini yake sio vumilivu kama unachelwesha service, naongea hivyo sio kwa kubahatisha, starlet ikizungusha biashara imeisha, tofaut na 1nz injin au 2nz, nilisha kuwa na starlet ilipo zungusha haikuweza kwenda umbali mrefu, ila 2nz ilizungusha bukoba baada ya kuweka oil fake, tukabadili oili na ikatembea had Dar, je starlet unadhan ingeweza kufanya hvyo...
Naunga mkono hoja. Ist, vtz na spacio zina teknolojia mpya kuliko Starlet...
 
Hivi hawa jamaa wanaouza mafuta wanatuona sisi mafala sana. Kwann mafuta yapo bei ambayo sio.... Me nilitaraji kwa sasa at least tungenunua petrol kwa 1500 hivi kwa lita ila wapo bado kwenye 1800
Mkoa gani huo....?

Hapa nilipo lita ya petrol ni 1717...Jumatano ya kwanza ya mwezi huu wa sita lazima watapandiaha hawa.

Kesho inabidi tukakamue full tank..

I need my lawyer.
 
yan ata boda boda anakudharau fujo nying road jichange mkuu upate hata carina au crester old model.

Passo je? Au vitz. Najichanga nifikishe around 5 mil. nitafute Passo au Vitz. Unadhani Niko sahihi? Naomba unishauri. Ama namie nibakie kwenye starlet.

NB: Kumbuka sijawahi kumiliki gari. Nataka usafiri kuniwezesha root za UDSM, Kimara na Bunju tufanye.
 
😀Yaani huto tudude huko raod hata uheshimiki kuwa na ww una gari.
 
Naunga mkono hoja....Ist, vtz na spacio zina teknolojia mpya kuliko Starlet...

Kaka naomba unishauri. Najichanga nifikishe 5 mil. nitafute gari ndogo kati ya Passo, Vitz, Starlet (najua kupata IST kwa bei hiyo mtihan).

Je, naweza kupata kweli kwa bei hiyo? Halafu nataka hiyo milioni 5 ijumuishe hadi BIMA ya gari (sijui ndio mnaita licence).
Nitaweza kweli ama najidanganya niendelee kusugua malapa?

Kati ya gari hizo ndogo unanishauri nitafute ipi (ukizingatia sijawahi kumiliki gari)

Natafuta gari ya mizunguko hapa mjini Dar. Kwenda UDSM, kurudi nyumban, kwenda kuwasalimia dada zangu Bunju!
 
Kaka naomba unishauri. Najichanga nifikishe 5 mil. nitafute gari ndogo kati ya Passo, Vitz, Starlet (najua kupata IST kwa bei hiyo mtihan).

Je naweza kupata kweli kwa bei hiyo? Halafu nataka hiyo milioni 5 ijumuishe hadi BIMA ya gari (sijui ndio mnaita licence).

Kwa kuanzia gari nzuri sana.. au kama una mishe za hapa na pale kwa mjini ni nzuri sana. Kumbuka hakuna stalert mayai, zote ni chuma.

Spea zake zinapatikana vizuri tuu.

Dada (nimechek avatar yako), naomba unishauri. Najichanga nifikishe 5 mil. nitafute gari ndogo kati ya Passo, Vitz, Starlet (najua kupata IST kwa bei hiyo mtihan).

Je naweza kupata kweli kwa bei hiyo? Halafu nataka hiyo milioni 5 ijumuishe hadi BIMA ya gari (sijui ndio mnaita licence).
Nitaweza kweli ama najidanganya niendelee kusugua malapa?

Kati ya gari hizo ndogo unanishauri nitafute ipi (ukizingatia sijawahi kumiliki gari)

Natafuta gari ya mizunguko hapa mjini Dar. Kwenda UDSM, kurudi nyumban, kwenda kuwasalimia dada zangu Bunju!
 
Kaka naomba unishauri. Najichanga nifikishe 5 mil. nitafute gari ndogo kati ya Passo, Vitz, Starlet (najua kupata IST kwa bei hiyo mtihan).

Je naweza kupata kweli kwa bei hiyo?
Halafu nataka hiyo milioni 5 ijumuishe hadi BIMA ya gari (sijui ndio mnaita licence)
Kwa hiyo budget yako ya 5milioni ina maana unataka kununua gari (Starlet, Vitz, Passo) kutoka mkononi kwa mtu na sio uagize Japan au kutoka showroom.

Ushauri wangu kwako.
-Kama ndio mara yako ya kwanza kumiliki gari, basi usijaribu kununua za kutoka mikononi mwa watu hapa Tz. Unaweza kujuta.

-Kupata Starlet from Japan au kutoka showroom ni vigumu kwa sasa, na ukiipata bei inaweza kuwa juu au ikawa imechoka sana (Milleage imetembea sana).

-Ni vyema ukajichanga zaidi ukafika hata 7milioni ukaagiza Japan mojawapo katika ya Passo au Vitz (Binafsi ningekushauri ufikirie Passo kwa sababu kuu mbili tu, ni toleo jipya zaidi ya Vitz kwa hapa Tz na pia ina space ya kutosha zaidi ndani ukilinganisha na Vitz. Mambo mengine sijaona tofauti kubwa za maana).

-Mwisho wa yote fikiria kumiliki IST kuliko hizo zingine (Starlet, Vitz, Passo) kwa sababu ni more Durable, stylish, Stable and classic kwa miji mingi hapa Tz kwa standard za gari ndogo za fuel economy. Japokuwa bei yake iko juu zaidi kwa at least 30% more than those ones.
 
Back
Top Bottom