Naomba kujuzwa mbinu za kutumia ili kupata mafao yako haraka baada ya kustaafu

Naomba kujuzwa mbinu za kutumia ili kupata mafao yako haraka baada ya kustaafu

Covid-19

Senior Member
Joined
Mar 2, 2020
Posts
162
Reaction score
365
Habari zenu wakuu?

Naomba tusaidiane namna bora ya mtu kupata mafao yake kwa haraka maana kuna mzee wangu amestaafu ualimu tangu January mwaka jana na mpaka leo anafuatulia mafao yake bila mafanikio.

Kila akienda mkoani hapo Kibaha anapigwa sound file halijatoka, mara Email haijasomwa yaani ni mizengwe mitupu. Naomba msaada wenu nawezaje kumsaidia kwani licha ya financial support tunayompa amekua amekosa amani ya Moyo kiasi kuzorotesha afya yake.

Natanguliza shukran, hata msaada wa PM unakaribishwa kuokoa Afya ya mzee wetu.
 
Serikali yetu ni ya hovyo sana. Mstaafu anahanya kupata mafao yake utafikiri siyo haki yake.

Ndo maana wazee wakishapata hizi hela wanatumia hovyo hazikai make wanakuwa na hofu utafikiri si haki yao.
 
Serikali yetu ni ya hovyo sana. Mstaafu anahanya kupata mafao yake utafikiri siyo haki yake.

Ndo maana wazee wakishapata hizi hela wanatumia hovyo hazikai make wanakuwa na hofu utafikiri si haki yao.
Ukiangalia wao wanavyogawana mabilioni halafu hawa viumbe wa million 70 miaka 60 wanavyowatesa ndio unaona kabisa hakuna mwanasiasa wa kuiona pepo.
 
Ana wenzake wana miaka 4 hawajapewa mafao yao.Awe mpole tu.
 
Back
Top Bottom