Kwanza kabisa andaa barua na documents zote zinazohitajika kwenye maombi yako ya kazi mfano barua ya kuandika kwa mkono/kuprint, nakala ya cheti, namba ama kitambulisho cha NIDA na vinavyohitajika.
Vipange kwa kuanza na barua iwe juu kisha documents nyingine zinafata. Kama NIDA number umeiandika kwa kikaratasi inaweza wekwa kwajuu ya barua kisha inapendeza ukabana na pin.
Bahasha ni yoyote ila kwa barua inafaa ile ya kaki maana ni kubwa inatoshea barua na documents zote kukaa pasi na shaka, gharama ni Tsh 200 (inaweza kuwa tofauti maeneo mengine)
Mbele ya bahasha andika anuani ya inapoelekea kwa ufasaha kisha nunua stempu (zinapatikana posta sana sana) gharama yake yawezakuwa 2500-3500.
Kwa Dar es salaam unaweza kwenda posta ukapata hizo stempu na kutuma hapohapo. Stempu utabandika mbele juu kulia kisha utaambiwa sanduku la kutumbukiza maana kuna la zinazoenda nje ya nchi na sa ndani.
Kama haupafahamu Posta kwa sehemu uliopo unaweza sema ukaelekezwa.
(KAMA KUNA NILICHOKOSEA AMA KUSAHAU SAHIHI KUSAHIHISHWA AMA KUONGEZEA)