Japo sikuambiwa hilo hospital, niliambiwa ni uric acid ipo juu.
Hata kama kesi ni hiyo mkuu, nitumie dawa zipi ndugu.
Habari ya leo wakuu, kama kichwa cha habari kinavyosema.
Ningependa nipate msaada wenu kwa kunifahamisha dawa au tiba ya Uric acid nyingi mwilini.
Natanguliza shukrani
Pole sana ndugu, hata miki milikuwa na hii shida ilinisumbua sana, zaidi ya mwaka mmoja nilitumia dawa sana lakini sikupata nafuu.
Hata hivyo nilimpata Dr. Mmoja alinipa somo vizuri sana.
Alinipa Dawa aina ya Allopurinol hii inapambana na uzalishaji wa Uric Acid mwilini nilipewa dawa ya kutumia wiki 8, pamoja na zankutuliza maumivu Ibuprofen na baadaye Indomethacin, Dawa hizi ziliniponya mpaka leo nipo vizuri kabisa.
Sambamba na Dawa hizo nilipewa masharti yafuatayo:-
1. Usinywe Pombe hasa Beer (Hapa ilikuwa mtihani sana ndiyo maana awali pamoja na kitumia dawa nilikuwa nakatiza doze sana
2. Nisitumie kabisa Nyama Nyekundu hasa maini, mapupu, moyo na damu ( Nilikuwa mtimiaji mzuri sana wa hizi organs za mbuzi tulikuwa tinachanganya na damu na nyama ya mbuzi naitwa Udee
3. Kunywa maji ya kutosha lita zisizopungia 3 kwa siku, kumbuka kunywa maji mengi wakati wa kumeza Dawa Allopurional
4. Fanya mazoezi angalau dk 15-20 daily au 30-60 weekend.
4. Epuka Njegere, ina kiasi kikubwa cha purine ambayo mdiyo mama wa kuzalisha Uric Acid.
5. Tumia zaidi matunda na mboga mboga
6. Epuka soda, Sukari na Juice yenye kuongezwa sulari kwa kiasi kidogo kunywa Soda aina ya Soda Water hii ina alcaline insaidia kupunguza acid kwa damu.
Ukifuata masharti haya yote na kutumia dawa kwa uangalifu nakuhakikishia utapona kabisa.
Utakuja kunishukuru na ulete na ushuhuda hapa.