Naomba kujuzwa tiba ya Uric Acid nyingi mwilini

Naomba kujuzwa tiba ya Uric Acid nyingi mwilini

Mimi sio dokta .
Ila naamini bamia zinaweza kukusaidia.
Sijawahi kulalamika maumivu ya viungo hata siku moja.
Kila siku nakula bamia zaidi ya 5 kwenye chakula changu
Sina hakika lakini, kuna kipindi nilikuwa nafanya mazoezi ghafla nikaacha. Then maumivu kwa maungio......nilikwenda hospital tofauti tofauti nilikuwa napewa dawa za kumeza.. ..huo mwaka nilimeza dawa nyingi haijawahi tokea maishan mwangu.
Nitashukuru endapo utanipa ushauri au msaada wowote mkuu
 
Pole sana ndugu, hata miki milikuwa na hii shida ilinisumbua sana, zaidi ya mwaka mmoja nilitumia dawa sana lakini sikupata nafuu.

Hata hivyo nilimpata Dr. Mmoja alinipa somo vizuri sana.

Alinipa Dawa aina ya Allopurinol hii inapambana na uzalishaji wa Uric Acid mwilini nilipewa dawa ya kutumia wiki 8, pamoja na zankutuliza maumivu Ibuprofen na baadaye Indomethacin, Dawa hizi ziliniponya mpaka leo nipo vizuri kabisa.

Sambamba na Dawa hizo nilipewa masharti yafuatayo:-

1. Usinywe Pombe hasa Beer (Hapa ilikuwa mtihani sana ndiyo maana awali pamoja na kitumia dawa nilikuwa nakatiza doze sana

2. Nisitumie kabisa Nyama Nyekundu hasa maini, mapupu, moyo na damu ( Nilikuwa mtimiaji mzuri sana wa hizi organs za mbuzi tulikuwa tinachanganya na damu na nyama ya mbuzi naitwa Udee

3. Kunywa maji ya kutosha lita zisizopungia 3 kwa siku, kumbuka kunywa maji mengi wakati wa kumeza Dawa Allopurional

4. Fanya mazoezi angalau dk 15-20 daily au 30-60 weekend.

4. Epuka Njegere, ina kiasi kikubwa cha purine ambayo mdiyo mama wa kuzalisha Uric Acid.

5. Tumia zaidi matunda na mboga mboga

6. Epuka soda, Sukari na Juice yenye kuongezwa sulari kwa kiasi kidogo kunywa Soda aina ya Soda Water hii ina alcaline insaidia kupunguza acid kwa damu.

Ukifuata masharti haya yote na kutumia dawa kwa uangalifu nakuhakikishia utapona kabisa.

Utakuja kunishukuru na ulete na ushuhuda hapa.
Mkuu mimi nimepewa allupurinol,na meloxicam,na diclofenac kwa siku tano,kabla ya dozi hii nilishapewa tena hizi hizi kwa siku 5,siponi ila napata nafuu ya muda tu
 
Pole Mkuu jaribu kutumia Blackseeds oil..
Habari ya leo wakuu, kama kichwa cha habari kinavyosema.

Ningependa nipate msaada wenu kwa kunifahamisha dawa au tiba ya Uric acid nyingi mwilini.

Natanguliza shukrani
 
Fafanua kidogo mpenzi upo siku nyingi sana
Nipo mpendwa...majani ya mlonge yaliyokaushwa ndani na kusagwa yakawa unga..yanatumika kwenye maji vugu kikombe Cha chai na kijiko cha chai kimoja.. matumizi mara mbili kwa siku asubuhi na jioni
 
Mkuu mimi nimepewa allupurinol,na meloxicam,na diclofenac kwa siku tano,kabla ya dozi hii nilishapewa tena hizi hizi kwa siku 5,siponi ila napata nafuu ya muda tu
Mkuu jaribu kutumia kwa week 8 kama alivyoshaur mdau
 
Habari ya leo wakuu, kama kichwa cha habari kinavyosema.

Ningependa nipate msaada wenu kwa kunifahamisha dawa au tiba ya Uric acid nyingi mwilini.

Natanguliza shukrani
Uric acid is a normal body waste product. It forms when chemicals called purines break down. Purines are a natural substance found in the body. They are also found in many foods such as liver, shellfish, and alcohol. They can also be formed in the body when DNA is broken down.
When purines are broken down to uric acid in the blood, the body gets rid of it when you urinate or have a bowel movement. But if your body makes too much uric acid, or if your kidneys aren't working well, uric acid can build up in the blood. Uric acid levels can also increase when you eat too many high-purine foods or take medicines like diuretics, aspirin, and niacin. Then crystals of uric acid can form and collect in the joints. This causes painful inflammation. This condition is called gout. It can also lead to kidney stone.

Kwa msaada na Ushauri zaidi wasiliana Basi Gombeyehealthcare.
Call/ WhatsApp number
0678211747.
 
Mkuu mimi nimepewa allupurinol,na meloxicam,na diclofenac kwa siku tano,kabla ya dozi hii nilishapewa tena hizi hizi kwa siku 5,siponi ila napata nafuu ya muda tu
Mkuu kwa siku tano mi chache inatakiwa wiki 6 mpaka 8 ndio utapona na kufuata hayo masharti
 
Habari ya leo wakuu, kama kichwa cha habari kinavyosema.

Ningependa nipate msaada wenu kwa kunifahamisha dawa au tiba ya Uric acid nyingi mwilini.

Natanguliza shukrani

Kama upo dar Tuwasiliane ili kesho uje upate mafunzo juu ya magonjwa haya na tiba yake
 
Back
Top Bottom