Naomba kujuzwa uimara na ubora wa Honda Crossroad

Naomba kujuzwa uimara na ubora wa Honda Crossroad

HONDA CROSS ROAD
Moja ya brand ambayo inavutia sana kuiona machoni kwa umbo lake limejaa kwa mbali unaweza kuifananisha na nissan xtrail au hammer ndogo ya msouth, gari hii inakuja na umbo ambalo ni SUV ,Inakuja na viti 7 na kwa ndani huku ikiwa na umbo moja ambalo ni zuri sana ,gari hii ilianza kutengenezwa na kampuni ya hondernamo mwaka 2007


Extras: Rear Camera
Safety Features: ABS, City Brake Active Sytem, Curtain Airbags, EBD with TCS, Rear Torque Distribution., SRS Airbags
Exterior Features: Alloy Rims, Fog Lights
Interior Features: Bluetooth Connectivity, Touch Screen Entertainment System, USB Charging

Gari hii inakuja na machaguo mawili ya injini ambayo ni

[emoji108]1800 cc injini hii inatumia teknolojia ya IVTEC ...na pia injini hii tumeiona katika gari honda civic injini hii inatoa 140 hp

[emoji108]2.0 IVTEC
Injini hii ni nzuri sana na imetumika pia katika gari ya honda CRV..Injini hii inatoa 150 hp

Katika gari hii inakuja na vifaa vya kiusalama maa

[emoji108]Driven ,passenger ,side air bag
[emoji108]Abs with electronic brake force
[emoji108]2x ISOFIX point
[emoji108]Traction control
[emoji108]Seat belt pretensioners

Gari hii unapoiendesha kwa kweli ipo comfort sana kwa sababu inakuja na

[emoji108]Steering wheel inakubali kuji adjust ..hii inasaitia kwa wafupi au warefu kuiset kulingana na uhitaji

[emoji108]Climate control inasaidia kubainai hali ya hewa mapema na kuendesha kulingana na hali ya hewa ilivyo

[emoji108]Inakuja na cruise control (optional) honda wanaiita IHCC..intelligent high way cruise control

[emoji108]Kuna sun roof hii ni ption kws baadhi ya grade katika model hii

Upande wa ndani
inakuja na mistari mitatu ya viti ,mbele kuna viti viwili ,mstri wa pili unakuja na viti vitatu na mstri wa tatu unakuja na viti vili ,pia katika gari hii kwenye milango yake kuna sehemu ya kuweka vitu mbalimbali ,lkn pia inakuja na cup holder mbili kwa sitinza mwisho mwili kwa ajili ya kuwekaea vinywaji pia inakuja na nanafasi kunws na ya kutosha ya kuweka miguu

Upande wa mafuta katika gari hii honda ukweli hawakuumiza sana vichws vyao inakuja na matumizi ya kawaida

[emoji108]1.8L inatumia km13.2 kwa lita 1

[emoji108]2.0 Linatumia km 11 kws lita 1

Kutokana na teknolojia iliyotumika hapa gari hii iliundwa kulenga soko la ndani ya japani na ulaya ....hivyo kwa soko lanulaya ipo yenye injini ya dizel ambayo ipo poa kuliko hizi za petrol

Upande wa acceleretion
[emoji108]1.8 L inatoka 0-100 km /h kwa 11 sec

[emoji108]2.0L inatoka 0-,100km/h kws 8.0 sec

Upande wa tank la mafuta ni lita 55

GROUND CLEARENCE
Gari hii upande wa uvungu inakuja na uvungu ambao upo juu sana na hivyo kuifanya ipite mjini au porini inakuja na 7.28 inch ...hivyo usiwe na shaka yaani ipo juu sana ndio maana ina muundo wa kibabe sana

Stability and handling
Honda cross road is a powerful car on the road with a 155 bhp and 190 Nm of torque. Additionally, it has superb refinement for a four-cylinder engine. The honda cross road is no lightweight but it doesn’t feel slow either. It has a great acceleration speed and keeps up well with other vehicles on the road. Handling is more akin to that of a sporty hatchback than an MPV. Body roll is controlled while lane-change agility is smooth and effortless. Generally, this is a great car to drive.

Upande wa 2WD na 4WD...nakushauri nunua lenye kutumia tairi mbili kusukuma gari yaani 2WD.... Maana lenye 4wD utumiaji wake wa mafuta upo juu sana linatumia wastani wa km 8 kwa lita 1 wabongo wengi hawezi

Changamoto katika gari hii ni za kawaida sana
[emoji91]Baadhi wameripot kutotumia mafuta kama ilivyokusudiwa tatizo hili linasababishwa na kutumia plug za kiwango cha chini pamoja na kutokusafisha air filter

[emoji91]Transmition failure ...hii inasababishws na kuchelewa kubadili oil katika gear box ,lkn pia uwekaji wa oili ATF ,unapelekea kuharibu gear box

[emoji91]Injini kuishiws nguvu hii inatoka tatizo la kimechanics hasa uchafu na kutosafishwa vizuri service kuwa chini ya kiwango

Gari hili kama unataka lidumu jitahidi sana upitie manual ya gari hili ....

[emoji91]Upande wa kuagiza usiagize la kutoka singapore unaweza kuja kujuta japo bei ipo chini sana ,kutokana na magari yanayouzwa katika soko la singapore ni magari ambayo yaliundwa kws ajili ya soko la ulaya sio africa agiza kutoka japana ndio zuri zaidi ufurahie na vipuli vyake vipi

Upande wa teknolojia
Kuna teknolojia ipo katika gari ambayo ni nzuri katika injini yake ambayo ina maboresho makubwa japo hawakutaka kuumiza kichwa upande wa kuiberesha katika wese .....inakuja na teknolojia kama ya climate control ...gari inaset kulingana na hali ya hewa ilivyo ....lakini pia kwa toleo la sport unaweza kuiswitch ikanyanyuka juu au ikabonyea ikashuka chini na ikaaanza kutambaa

Upande wa mwaka nakushauri nunua gaki ya mwaka 2009-2010 ili uokoe fedha na kiac cha kodi kipungue ...utakavyo nunua la miaka ya karibuni ndivyo hela itaongezeka ya kulinunua gari hili

Upande wa matengenezo ....nakushauri gari hili linapokuwa na shida yoyote ni vyema kwanza ukatumia dignosisi mashine ...kubaini tatizo ndipo uweze kulishughulikia

Upande wa vifaa
Vifaaa vipo vingi sana ninwewe tu na hela ya yako na baadhi ya spare zinaingilia na hondar civic

Ukitaka kulipa muonekano mzuri gari hili nakushauri weka sport limu aisee ukipita mtaaani lazima watu wajue ni top manyota kapita ...kumbe wapi

Mwisho
Karibu katika ulimwengu wa honda cross dude tamu samu hii ukilinunua huwezi kujutia halafu bei ya kawaida sana .....!! Vijana sasa hizi ndio gari za kununu sasa kama unataka heshima fanya makeke
Kaka wewe huwenda ni mwalimu mzuri sana nimekukubali kwa kutoa maelezo mazuri..na sehemu gani naweza enda kuipimp ikawa kama hammer..maana meziona ambazo zimepimpiwa aiseh zinamuonekano flani wa kinyamwezi sana..samahani lakin
 
Hii customization nimeikubali. Kitu kama mdogoake na Hammer
FB_IMG_1616331011865.jpg
FB_IMG_1616331160285.jpg
FB_IMG_1616330987682.jpg
 
Daaaa hakika mkuu umetisha sn aiseee yan umemaliza kila kitu na hakika umesaidia wengi sn....tunashukur sn mkuuu kwa mchango wako huu murua mana umetufungua wengi...naona honda kila siku gari zao nyingi saiz zinakimbiliwa sn na watu wengi na naona gari kama honda hr-v old model zimeuzwa sn na hata ukifatilia kwenye mitandao ya magari utakubaliana nami...

Pia kuna honda cv r nazo naona zinatoka sana na sasa kuna hii kitu ya honda crossroad yan ni gari moja la kinyama sn kuanzia muonekano hadi vitu vyake vya ndan kama ulivoeleza .....tunashukur sn kaka hopely utaendelea kutupa zaid dondoo hasa kwa haya magar ya honda mana naona ni gari ambazo ziko vizyr sn

Sema ni jembamba mnabanana kinoma humo ndani labda mkae 1 X 1 akiongezeka wa tatu ni hatari
 
Blake inaingiliana na alteza, Z link inaingiliana na Subaru, engine mount zinafanana na tako la nyani, hiyo chombo ina collabo la kutosha

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mplange unaingiliana na nini
 
Nimefuatilia hii gari iliatengenezwa ikilenga soko la Japan halafu ililenga vijana wenye miaka 20-30 na wanandoa wachanga wenye watoto wadogo. Nimejaribu kuangalia kwenye calculator ya TRA ushuru wake ni 6M tu.
Haya magari hawayatengenezi tena....sijui ukinunua vipuri vyake inakuaje
 
Nimefuatilia hii gari iliatengenezwa ikilenga soko la Japan halafu ililenga vijana wenye miaka 20-30 na wanandoa wachanga wenye watoto wadogo. Nimejaribu kuangalia kwenye calculator ya TRA ushuru wake ni 6M tu.
Haya magari hawayatengenezi tena....sijui ukinunua vipuri vyake inakuaje

Hapo ndio changamoto sijui wajuzi wanasemaje
 
Wadau nahitaji kununua gari aina ya Honda CrossRoad naomba ushauri kwa watalamu hasa kujua uimara, vifaa na utumiaji wa Mafuta.

IMG-20221013-WA0021.jpg
 
Back
Top Bottom