Naomba kujuzwa zaidi kuhusu biashara ya nyumba (AirBnB)

Labda abuni bnb ya kitanzania kwa kuanzia
 
Mkuu sina uhakika sababu Marangu kuna mtu ana nyumba ya kawaida sana kila msimu anapata wazungu kwa njia ya mtandao bila shaka ndio hii kitu...
 
Zingatia ushauri wa wadau uzio wa kutosha , fanya land scaping, panda palm tree za tofauti tofauti paving kiasi hapo tutakuwa tunazungumza lugha nyingine
 
Mkuu hongera Sana.Fungua app ya Telegram,kuna channel na group la AirBnb Tanzania,Kocha Mkuu dada Jacqueline Mwanri,hapo ndani utajifunza mengi.Yaani haupo mbali na kupiga hela.Bagamoyo,Dar,ZNz na Arusha ndiyo Maeneo AirBnB yanafanya vizuri.Kaza but Mkuu
 
Nimechelewa ila kama bado hujaifanya airbnb jitahidi weka uzio. Kisha weka pavements, ukoka na maua ndani bila kusahau miti ya matunda na kivuli. Weka tank la maji na emergency generator. Ungeweza zaidi weka na swiming pool. Pia samani za ndani ziwe nzuri na uweke TV kubwa, taa za kisasa nzuri. Si lazima ufanye vyote kwa pamoja ila hakikisha mwisho wa siku vyote nilivyotaja vinakuwepo, baadae Mungu akibariki unaweza jikuta ndio biashara yako hii unakuwa na apartments kadhaa.

After that una uhakika wa kupata wateja wa hela nzuri. Alafu usiseme wazungu tu, ukifanya hivyo wateja wako 90% wanakuwa wabongo wanaofanya retreat nyumbani kwao na wanaotaka faragha. Na hauitangazi airbnb peke yake hata Instagram unakuwa na wateja wengi.

All the best. Ningependa kujua ulijenga kwa gharama gani na ilikuwa mwaka gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…