Naomba kumfahamu Reccep Tayyip Erdogan na Uturuki kwa ujumla

Naomba kumfahamu Reccep Tayyip Erdogan na Uturuki kwa ujumla

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Nilikuwa namchukulia mwepesi kwa wakubwa wa ulaya kama Romania au Estonia tu.

Ila naona kama inabidi nimtafakari mara mbili mbili;
  • Alipinduliwa na ghafla mapinduzi yakazimwa, walioshiriki wote wamesakwa jeshini na wameshakamatwa. Alifika mpaka tz huyu mtu, sijui alimwambia nn jpm lakini alitulia kimyaa baada ya msafara ule na sijui ilikuwa safari ya kheri ileee?
  • Kumbe nae ana vikosi Iraq, tena nasikia wamewahi kukipiga huko na urusi.
  • Alikoromeana vikali na ufaransa muda si mrefu, ugomvi ulifika hatuackubwa tu.
  • Kuna jengo la kihistoria (nimelisahau jina) alilibadilisha matumizi kibabe sana. Wakubwa walipinga sana lakini hakuwasikiliza.
  • Anawapatanisha Urusi na Ukraine, nasikia pia kuna vifaa vyake vimeonekana huko.
  • Sasa hivi anaziwekea ngumu Finland na Sweden kujiunga na nato, sijui atafika wapi katika hili lakini ujasiri wa kulianzisha tu, si haba.
Naomba kufahamu kidogo kuhusu huyu mtu na nchi yake kwa ujumla, mbona nahisi harufu ya ubabe ubabe hivi.

Karibuni mnaomfahamu na kuifahamu!
 
Huyu mwamba ni kama kapembe kanakochomoza kwa mbaali.

Inasemekana US alitaka kumpindua akatonywa na Putin jaribio lile haraka sana likazimwa.
Ni rais ambae hana rafiki wala adui. Muda wwte anakugeuka au kuungana na ww.

Huko Syria 🇸🇾 anang'ata na kupuliza.

Wajuzi wa mambo watakuja.
 
Ni dikteta aliyejificha kwenye dini anayecheza na Katiba ya Uturuki mara kwa mara ili atawale milele.
 
Back
Top Bottom