Kwanza anaitwa Babra Hassan sio Barbara.
Kwa mtazamo wangu kwa muda ambao nimekuwa namsikiliza napata picha ya mtu anayejali sana tabaka fulani la Watu na kupuuza jamii ya watu wa chini a.k.a Watu wa kawaida....ukisikia reference zake nyingi zinatia ukakasi....binafsi sivutiwi saaana na ujivuni wa hivyo....ana mengi ya kujifunza kutoka kwa kina Masood.....B twelve, Dahuu.
Kuhusu elimu...inategemea na mtazamo wako kwani kwa Wabongo Mtu ukijua kuongea kiingereza tu basi, utaonekana una hadhi ya kupelekwa USA ukarushe Rocket....ila kwa muda ambao nimekuwa namsikiliza namuona ni fundi wa kujibu maswali kama 'baby shower ni nini?' nje ya hapo ukamuuliza swali technical kidogo basi uwe na namba za flying doctors....coz atazima papo hapo.