ramadhan ndonja
New Member
- Aug 9, 2024
- 2
- 3
Nahitaji kufuga kuku wa kienyeji lakini nahitaji kujua changamoto ambazo huwa zinajitokeza na namna ya kuziepuka.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kiukweli hii biashara wengi huiponda, lakini nimefanya utafiti sana, inalipa lakini ukubali kufuga kisasa! Kwanza upate elimu, uwajue vizuri, mbinu za kuwazalisha kwa muda mfupi, magonjwa, chakula, changamoto yao kubwa hawa ni kukua, wanakua taratibu, so lazima ujue kubalance chakula, ili wakue haraka na wewe upate faida, so ujifunze chakula mbadala, Azola, funza, lakini pia kuna sehemu niliona, kuku wa siku moja, analishwa stata mpaka afike mwezi, analishwa usiku na mchana, kisha wanaanza kulishwa kawaida, lakini pia hawa kuku hawataki kufungiwa ndani hawa wanapenda huria, so unakuwa na wavu unazungushia ili wawe huria ndani ya uzio, chanjo, chanjo,chanjo! Hapo usipitishe hata moja tena! Chanjo wapewe kwa wakati! Vitamins na dawa za mafua ziwepo muda wote. Banda lizingatie vigezo vyote, ukubwa kulingana na kuku ulionaao, Soko lipo la kutosha tu.Nahitaji kufuga kuku wa kienyeji lakini nahitaji kujua changamoto ambazo huwa zinajitokeza na namna ya kuziepuka.
asante sana mkuuKuku wa kienyeji Hana magonjwa au ha athiriki sana na magonjwa kama Hawa wa kisasa
Cha kufanya zingatia chanjo zote na Kwa muda sahihi.
Wape chakula sahihi na chenye virutubisho.
Usafi Kila inapohitajika
Wafuge nusu huria na
Panda miti ya madawa yao ya kienyeji
Mfano usikose hii miti
Mipapai
Mwaribaini
Mlonge
Alobera
Pilipili kichaa hii itakusaidia wewe na kuku wako pia.
Mwisho Mungu awe nawe katika jitihada zako.
Zingatia 1.chanjo kwa wakatiNahitaji kufuga kuku wa kienyeji lakini nahitaji kujua changamoto ambazo huwa zinajitokeza na namna ya kuziepuka.
Zingatia 1.chanjo kwa wakati
2. Usafi wa mazingira unayofugia
3. Gharama(bora ukatengeneza formula yako mwnywe ya chakula na ukawalisha kuendana na idadi yao)