Naomba kuuliza: Hivi nchi ya Tanzania haina uongozi?

Naomba kuuliza: Hivi nchi ya Tanzania haina uongozi?

Ulishawai kuiona familia ambayo haina mzazi?
kila mtu ni kambale anafanya anachotaka!

nashangaa hizi siku kila mtu alipo anajiropokea tu, kila mtu anaongea anachojiskia,

Kuna chizi mmoja anajiita shekhe amehaidi kuwakata vichwa wote wataoandamana desemba9, tena akiwa mbele ya vyombo vya habari! yani mtu anaongea tu anavojiskia

Mara anahaidi wamejipanga mara watadili na shule za kikatoliki, wakati hili linaendelea mara MC pililipili kauliwa, yaani imekua vurugu mechi!

Hivi niwaulize vita ya kidini mnaiweza? mnafahanu civil war ni mbaya kuliko vita ya nchi na nchi?


Hivi amekosekana mtu mwenye namlaka kuzuia haya mambo?

Hakuna mtu mwenye sauti ya mwisho nchi hii?

Sawa tutaona mwisho wake ni nini nawaambia hata wanaojiona wapo salama hawatakua salama


View: https://www.facebook.com/share/v/17K1axiG3w/



Wakikatwa vichwa tayari tunamjua mkataji ni huyo jamaa
 
Cha ajabu huyu hata shitakiwa kwa kutangaza mauwaji na uvunjifu wa amani mbele ya vyombo vya habari
Alafu kuna binti anapambana na kesi ya uhaini kisa kucheza mziki wa samuya…my country people tutavuna tunachokipanda acha inyeshe tuone panapovuja
 
Back
Top Bottom