Naomba kuuliza kuhusu chimbo zuri la kununua mitumba balo za mitumba

Mi sio mtaalam lakini nimeona nitue nishee kidogo nnachojua.

Japo mitumba Iko tofauti tofauti.....nguo za watoto,za wakubwa, ...kariakoo mtaa wa narung'ombe...... Na mingine mnazi mmoja. Ila ukiweza kununulia mzigo wako godown usiende kwenye hayo maduka ni nafuu kidogo maana mizigo wanashusha godown na kuanza kusambaza kwenye maduka yao.
 
Somo zuri sana.Nilikuwa nataka kuanza biashara ya mitumba mwaka huu naomba kuuliza n sehemu gan wanapouza nguo za mtumba za kike grade A zinazoendana na fashion?naomba ushauri wako
 
Umeelezea vizuri hii bishara, mimi kuna siku nilipita eneo linauza viatu vya mtumba vimepangwa chini, nikaona raba mbili kali sana ikabidi nisogee, kuuliza bei jamaa akaniambia nimpe 12,000 tukaongea pale nikamuambia nachukua 2 kwa nusu bei ila akakaza sana tukafikia bei 7,500 kwa pea na vipo ktk condition nzuri kabisa.

Raba zilikuwa ni Air Jordan 1 Low na Yeezy Boost 350 V2 kwa ile bei sikutaka kuviacha kabisa.

Sasa ulivyoelezea hao mawinga ndiyo nimeelewa maana kuna jamaa ana frame yake huwa anauza mtumba na raba kama Air Jordan 1 ni kuanzia 40,000.



 
Haya kila kitu hadharani
 
safi sana kaka, mimi nipo karagwe mkoa wa kagera, baada ya kupata changamoto kwenye biashara ya vifaa vya simu na m-pesa Nimefikiria mwaka huu nifanye biashara ya mtumba kwa kuanza na Tshirt kufungua belo grade 1 pamoja na simple jacket , maana kwa huku naona biashara ya mtumba bado iko chini sana wengi wao wanaleta nguo ambazo hazina quality kabisa mf. mm binafsi ni mpenzi wa tshirt za mtumba ila huwa nanunua mwanza mlango mmoja au dar ilala au kama ni kampala huwa nanunua pale stendi ya Gisan maeneo ya Hyper market ila huwa nanunua za kuvaa tu.
1. wapi ntapata bero la Tshirt grade 1 ( korea)??
2. Je nianze kwa kufungua belo au nianze kwa kupoint kutoka mwanza mlango mmoja??
3. Nilikuwa nimepanga nitafute frem ili niwe nauzia hapo na zile za quality ya chini nampa kijana kwaajiri ya kutembeza
ushauri plz
 
Oke, kama una uzoef wa kupoint ni bora ufubgue la kwako mana huwezi point mzigo wa kutosha Kwa siku moja. Pia kama una plan ambayo itakupa muda na uwezo wa kuajiri watu wengine fungua Robota lako. Robota unaweza chukua mnazi mmoja pale Kwa jamaa angu anaitwa amiri. Atakuuzia bei nzur tu. Lakin pia unaweza kwenda bazaar kule Tazara karibu na tbc. Kama unaweza pia kupata hapo mwanza kachukue Robota. Uwe na plan ya zile zinazobakia utazipeleka wapi kama kwenye minada au wapi. Mm naona kuchukua Robota risk ni kubwa ila pia faida huwa nzuri. Lakin pia kama utakuwa na mapointa itapendeza zaidi
 
Mkuu naomba mawasiliano yako maana umelimit view katika profile yako πŸ™
 
Wakuu naomba mnisaidie mawasiliano ya simu ya muuzaji wa mitumba ya nguo za kike Dar.
Naomba mnitumie JF inbox au normal sms 0624573133
 
Mm niko kayanga hapa tuchekiane mkuu
 
Nguo kali za mitumba grade A, Cream kabisa, za kike na za kiume.

Wanawake.
1. Mashati ya ofisini.
2. Mashati casual.
3. Form 6.
4. Jeans mkataba.
5. Pensi.
7. Flana.
9. Cardet.
10. Suaruali za vitambaa.

Wanawake.
1. Magauni ya sherehe.
2. Madira.

Nicheki #0623123369 wasap nikuunge group au unaweza ukaingia moja kwa moja.

 
Only admins can send messages. Mnaficha nini huko mpaka mzuie watu wengine wasitume texts na ukizingatia ni kundi la biashara? P
 
Nimesha wahi pigwa ndoige moja zamani kwenye hii bznec sina hamu! Tunaenda nunua watu kama kumi hivi ila mimi nikifungua nakutana na matambara hamna cha maana 2M iliteketea
 
Only admins can send messages. Mnaficha nini huko mpaka mzuie watu wengine wasitume texts na ukizingatia ni kundi la biashara? P
Hamna mkuu, nilifunga kwa sababu kuna watu walikua wanashare mambo ya hovyo so nikalifunga kwa muda tu ila mostly group linakuwa wazi
 
Nimesha wahi pigwa ndoige moja zamani kwenye hii bznec sina hamu! Tunaenda nunua watu kama kumi hivi ila mimi nikifungua nakutana na matambara hamna cha maana 2M iliteketea
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Na unakuwa ulichagua mwenyewe au walikuchagulia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…