Naomba kuuliza kuhusu chimbo zuri la kununua mitumba balo za mitumba

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Na unakuwa ulichagua mwenyewe au walikuchagulia
Tumekaa nje mizigo inatolewa kwa order na kwa majina kadiri mlivyo lipa, unafika kwenye kufungua mzigo na wenzako wanao fungua mizigo yako mambo yanakua tofauti kabisa!

Sikukoma nikahama kijiwe nikahamia kisutu! Huko ndio ilikua balaa! Yule mhindi ilikua anataka tuwe wabia[emoji1787][emoji1787] nikabanga fremu flani sinza makaburini sokoni ilikua kubwa maana ilikua ni saloon ya kike hivyo akawa anakubali nachukua mizigo nakuja kui grade pale ila baada ya yeye kutoa 1st grade, yaani kila balo lililokua linakuja tulikua tunafungua anatoa nguo tano kila balo ambazo zimenyooka zingine anaacha[emoji23][emoji23][emoji23] sikujua kumbe nilikua naelekea 18 zake[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kuna watu wanaakili sana.

Nikapanga na fremu mabibo hostel kona ya kwanza kuingia chuo pale juu, baada ya mzigo kua mkubwa niliougrade kabla sijafungua duka, tukakutana na nane nane ilikua inaidhinishwa mtwara, ila mahesabu yake anigee mzigo wa mil16 malikauli niende nao 8 8 dodoma, bw'wee, nikaenda nikaandaa eneo nikaja nikafunga mzigo[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mzigo niliokuja kuufungasha sikuwahi kuuona na sikujua aliuongiza lini, kumbe kitaaambo alisha uingiza na alisha upekuwa vyakutosha, mimi sikuhangaika kuufungua maana ni balo nyingi sana na muda ulisha isha wa kwenda dodoma[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Kilichoenda kunikuta [emoji848][emoji16][emoji16] mpaka leo hii nawaonaga wanaofungua mitumba kama majini watu[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Fungua balo la kwanza la jinsi, zinatoka jinsi zile za zamani sana kama maraizoni haijulikani kama niza kike au za kiume, na nyingine ni matambara[emoji1787][emoji1787] duh

Fungua la pili sasa yakatoka mashati [emoji1787][emoji1787][emoji1787] makubwa hata pepekale havai na mengine kama mapazia sijui hata waliokua wanayavaa walikua ni watu wa aina gani na matambara ya kutosha

Kuendelea mwendo ukawa ni huo huo

Sikuumiza kichwa kwakua nilikua sijamlipa kitu pia mzigo alikua anaujua na aliuingiza akaupekua bila mimi kuwepo, ilikua vurugu ambayo sitamani kuikumbuka[emoji1787][emoji1787]

Labda siku hizi biashara hiyo itakua imetulia ila zamani ilikua mtihani sana
 
Dah nimecheka sana aisee,eti suruali kama malaizoni na mashati makubwa hata pepe kale havai[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Ndugu umenikumbusha beli yangu ya kwanza ya jinsi nilio agiza kenya, niliagiza men jeans, kaka imetoka jeans kama hizo ulizosema, yaani hazieleweki ni za Kiume au za kike, mpaka leo huo mzigo upo, hakuna mteja anasogelea hata uuze buku buku
 
Ndugu umenikumbusha beli yangu ya kwanza ya jinsi nilio agiza kenya, niliagiza men jeans, kaka imetoka jeans kama hizo ulizosema, yaani hazieleweki ni za Kiume au za kike, mpaka leo huo mzigo upo, hakuna mteja anasogelea hata uuze buku buku
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Umenichekesha hapo uliposema haziuziki kwa bukubuku,na wakati umezigharamia malaki ila binadamu sio watu kabisa
Kaka we acha tu, yani unakata beli ukidhani unaopoa, lakini cha ajabu nikakutana na suruali za ajabu, yaani zile fashen za zamani,. Unakuta suruali juu imebana afu chini imemwaga,.. Mbaya zani zina mifuko mifupi hata kiganja hakiingii, yaani ni nguo za kike ambazo ni toleo la zamani,.. Na huyo mshakaji alijua hilo bei kabugi kwahio akanibambikia mimi, laki tano mzee imepotea yoteeeee... Haa niuze buku akuna mteja anasogea, mpka leo ntaka tu nikazitupe au nikawape wabeba mizigo sokoni
 
Watu wana dhambi duniani hapa
 
Watu wana dhambi duniani hapa
We acha tu mkuu, yani mtu hafikirii mwenzie anakwenda kufanya biashara, anawaza faida zake tu,.. Alafu uyu jamaa ningekua nanunua kwake, ila kanivuruga nikamuacha
 
Pole mkuu ingawa nimecheka sana, why pepe kale lakini??
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] inasikitisha ila its funny
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] inasikitisha ila its funny
Yaani mpaka leo mfanya biashara wa nguo, unapaswa kumuomba mungu, mana hata uwe mjanja vipi mzee kuna mahali utapigwa tu
 
Pole mkuu ingawa nimecheka sana, why pepe kale lakini??
Balaa! Yana fanana na lile shati la lodi lofa akishuka kwenye gari yake ile sijui aina gani[emoji1787][emoji1787]
 
Umetisha kamanda
 
Mkuu un
Yaani mpaka leo mfanya biashara wa nguo, unapaswa kumuomba mungu, mana hata uwe mjanja vipi mzee kuna mahali utapigwa tu
Nimecheka kama mazuri wakati mtu alitoa hela.

Mkuu vipi kama utaamua kudeal na mashuka nayo unawez kubambikiwa?
 
Mkuu un
Nimecheka kama mazuri wakati mtu alitoa hela.

Mkuu vipi kama utaamua kudeal na mashuka nayo unawez kubambikiwa?
Kaka hakuna kizuri kwenye mtumba, labda uw3 unauza nguo mpya, ila sio mitumba kaka, hua wanaweka kwa ubora, na yale marobota ambayo yana ubora, hua yakishuka tu, kuna wateja wao maalum wanawaita ama kupeleka mapema sana, yaani zile grade one safi... Sasa ninyi mnaofata nyuma, kila mtu na bahati yake ndugu yangu, utakachokutana nacho mshukuru mungu

Nakupa ushauri, kamwe usijidanganye kuagiza mzigo mkuu, hio ndio hatari zaidi,.. Ogopa muuzaji mwenye Babalo ya bei zote,.. Yaani balo la laki 2 analo, laki 3 analo, laki 4 analo, mpaka laki 7 analo na nguo ni aina hio hio moja... Ogopa sana... Unalipia balo la laki 4 anakupa balo la laki 2,... Afu ogopa sana picha za mtandaoni.... Mana anapiga picha suruali zile grade one kaliiiiiiii..... Afu anakwambia hilo balo lake ni laki tatu... Wakati ukiiangalia, ni balo la laki 7...sasa jichanganye uagize,.. Kama hujapata kichaaa cha mbwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…