Naomba kuuliza ni vibali vingapi vinahitajika kuanza ujenzi wa nyumba

Naomba kuuliza ni vibali vingapi vinahitajika kuanza ujenzi wa nyumba

Mkuu rudia kusoma nilichoandika
ulichoandika si sahihi hata kidogo kwa maana si lazima eneo liwe limepimwa na wala hauhitajiki kurasimisha eneo ili uweze kupatiwa kibali cha ujenzi.

1. kwa eneo lililopimwa utapeleka set ya michoro iliyoidhinishwa ili taratibu za kibali zifanyike.

2. kwa eneo lisilopimwa unahitajika kupata coordinates za eneo husika pia ujaze fomu maalumu ya ushirikishwaji wa majirani wa pande nne, ipite kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa, mtendaji wa mtaa, mtendaji kata ndipo uipeleke halmashauri husika ili taratibu za kupatiwa kibali zifanyike.

note: urasimishaji wa eneo na uombaji wa kibali cha ujenzi ni vitu viwili tofauti, nazungumzia kwa uzoefu wa ujenzi kwenye maeneo yaliyopimwa (surveyed areas) pamoja na maeneo yasiyopimwa (unsurveyed areas).
 
Wataalamu naomba mnisaidie kunijuza kuhusu vibali vya ujenzi, binafsi nina kibali cha serikali za mitaa ila kuna mtendaji alikuja site akaanza kufokafoka nikamwambia kibali ninacho, sasa baada ya kumwambia kibali ninacho akaanza kuuliza vibali vya mkurugenzi mara engineer wa wilaya, aisee nilishangaa sana maana sijawahi kusikia hivo vitu, hii issue ya vibali ikoje?
Serikali ya mtaa haitoi kibali cha ujenzi , Bali wanakupatia barua ya utambulisho kuwa lile eneo ni Lako na halina mgogoro wowote
Ili ukienda manispaa au halmashauri ya wilaya usikilizwe na kupatiwa kibali cha ujenzi
 
Ww ulikua hujasoma depo huyo alikua anataka hela ya soda mbona tunaishi nao kihivyo tu.Hivi najenga fensi ama nachimba shimo eti nikachukue kibali ....nitawasubiri wakija nawapoza biashara imeisha.
 
Ww ulikua hujasoma depo huyo alikua anataka hela ya soda mbona tunaishi nao kihivyo tu.Hivi najenga fensi ama nachimba shimo eti nikachukue kibali ....nitawasubiri wakija nawapoza biashara imeisha.
kuna wakati kuwapoza ni gharama zaidi kuliko kuchukua kibali kwa kufuata utaratibu na wakijua huna kibali huwa wanakuja kwa kupishana.
 
Hivi vibali ni hadi kwetu tunaojenga nyumba vyumba vitatu huku mtaani? Maana mimi naendelea ila sina kibali chochote.
 
Back
Top Bottom