Jana nilitoa wito wa kuzitumia siku tatu za ibada za wiki(Ijumaa, Jumamosi na Jumapili) kwa ajili ya kukemea matendo maovu yanayofanywa Nchini na hasa mauaji ya watu. Kipindi kile cha mahubiri/hutba kitumike kufanya kazi hiyo.
Kesho ni siku ya Ijumaa ambapo wenzetu waislamu ndo siku ya Ibada kwao. Ni matumaini yangu kuwa watafanya hivyo.
Ikiwa Kiongozi yeyote wa Dini ataogopa kukemea vitendo vya mauaji waziwazi tena ndani ya Ibada, Je, ni dhambi gani zaidi atakuja kuikemea kwa uwazi?
Kwa hakika Kiongozi wa aina hiyo hataweza tena kukemea maovu yoyote chini ya jua ikiwa ataogopa kukemea mauaji ya watu, kwa sababu mauaji inaweza kuwa ni dhambi kubwa zaidi kuliko zote chini ya jua.