Naomba maoni kuhusu biashara ya nafaka Dar es Salaam

Mimi ni mzoefu wa nafaka na ninafanya biashara hii nipo mwananyamala.... kiufupi pesa yako ni ndogo bado ungekuwa na angalau milioni 20...
kodi frem laki 3 kwa mwezi,, mwaka ni milion 3.6.... leseni laki 2,, Tra laki 5.... mapareti pamoja na kibanda cha cashier laki 5... mzani laki 6 jumla 5,400,000 ukitoa milion 9 zako unabakia na milion 3 na laki 6 huwezi kununua nafaka kwa hela hiyo labda kwa mali kauli sio cash

fanya uongeze pesa angalau milion 20.
 
Jf ina watu yenyewe ndio kama hawa
 
Kwa staili hii watu hawawezi fanya biashara ya nafaka..acha kumtisha hiyo hela inatosha sana kwa biashara ya nafaka.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwa staili hii watu hawawezi fanya biashara ya nafaka..acha kumtisha hiyo hela inatosha sana kwa biashara ya nafaka.

#MaendeleoHayanaChama
Kanitisha hata Mimi wakati nasikia ukiwa na hata 1m tayari unaanza business.
 
mkuu hyo hele ni nyng asikudanganye mtu et ni ndogo, kwa mtaj huo ukiuwekeza vzr hutataman biashara nyngne bas tu sjui uko wap lkn una mtaj wa kutosha
 
usiwe mwoga huo ni mtaj wa kukuingizia ml1 had 1.5ml inategemea unafqnyia wap
 
Hao wa mali kauli wana vigezo gani na wanaweza kukupa mzigo hadi wa kiasi gani
 
Kibanda cha cashier cha nini ukifungua sokoni kuuzia mlaji wa mwisho
 
Kibanda cha cashier cha nini ukifungua sokoni kuuzia mlaji wa mwisho
sasa hela unataka uweke wapi na madaftari yako ya hesabu??? lazima uwe na kiofis kidogo kwenye frem yako!!
 
Kwani analazimika kulipia fremu kwa mwaka hiyo Tra kulipa laki 5 za kazi gan kodi baada ya makadilio kwa mwaka? Maana kwa uelewa wangu ufanyae biashara ndo mwenye uwezo wa kujikadilia mwenyewe kwann uweke makadilio makubwa wakati ndo kwanza unaanza hiyo biashara mfano unaweza kuweka makadilio ya kulipa laki 3 kwa mwaka yaani 75,000/- kila baada ya miezi 3 halaf sio lazima ulipe yote kwa mkupuo mmoja unao uwezo wa kulipa hiyo 75,000 kila baada ya miezi 3. Kwa mtaji wake wa milioni 9 hakika anaweza fanya ulivyoanza wewe sio lazima kila mtu aanza hivyo biashara ni uvumilivu, kujituma, nidhamu, kauli n.k.
 
Kaka tulisoma wote Cuba [emoji1083] eeh...! ? Maana hiz nondo ni zile zile tulizo jibia kwenye UE[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…