Naomba maoni yako: Mtindo gani wa maisha hapa ni hatari zaidi kwa changamoto ya uzito?

Naomba maoni yako: Mtindo gani wa maisha hapa ni hatari zaidi kwa changamoto ya uzito?

Neema ya BWANA

Senior Member
Joined
Jun 25, 2023
Posts
129
Reaction score
61
SWALI:

Je! Ni mtindo upi wa maisha (lifestyle) kati ya iliyoorodheshwa hapa chini ambao ni HATARI ZAIDI kwa changamoto ya Uzito Usio wa Kawaida (Under Weight, Over Weight or Obesity); lakini ukishughulikiwa ipasavyo na kwa usahihi unaweza kuleta suluhu kwa mitindo mingine ya maisha iliyosalia katika orodha hii?

A: Matumizi ya dawa ya muda mrefu kutokana na changamoto mbalimbali za afya, magonjwa, matumizi ya dawa za kulevya na pombe.

B: Ulaji wa chakula chenye kemikali, sumu, mafuta mengi, kisichokidhi mahitaji, kisicho safi na salama, kisichozingatia kanuni bora za mapishi na changamoto za ulaji kama vile kula chakula kingi sana wakati wote, kukosa hamu ya kula, changamoto kwenye mfumo wa chakula, n.k.

C: Kutofanya mazoezi ya mwili na kutokuwa 'active' katika kutembea, kusafiri, kutalii, kufanya kazi na kutoka sehemu moja kwenda nyingine

D: Kuishi maisha ya mawazo na msongo wa mawazo (stress), hofu na mashaka kwa sababu mbalimbali.
 
Back
Top Bottom