Naomba mawazo ya biashara ya viazi

Naomba mawazo ya biashara ya viazi

hp4510

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
7,235
Reaction score
7,392
Wakuu salaam

Kuna ndugu yangu anataka kuanzisha biashara ya kununua FUSO zima la viazi vya chips / viazi ulaya/ viazi mviringo, Njombe na kuja kuuza Dodoma

Naomba Kwa mtu mwenye uzoefu au amewahi kufanya hii biashara atoe uzoefu wake

Hasa kwenye mambo ya soko kwenye kununua na kuuza
 
Hii akikaa vizuri atatoboa mapema tuu

Apeleke Dodoma kahama mtwara au masasi
 
Wakuu salaam

Kuna ndugu yangu anataka kuanzisha biashara ya kununua FUSO zima la viazi vya chips / viazi ulaya/ viazi mviringo, Njombe na kuja kuuza Dodoma

Naomba Kwa mtu mwenye uzoefu au amewahi kufanya hii biashara atoe uzoefu wake

Hasa kwenye mambo ya soko kwenye kununua na kuuza
Masoko mengi yameshikwa na madalali huwezi kuingiza tu sokoni ukapata wateja lazma ukajichanganye sokoni kwanza ujue system ya pale.... mfano soko zote zilizo tajwa hapo ni masoko mazuri sema wengi wao wana taka mali kauli yani ufike uwape mzigo baada ya siku kadhaa ndipo uwekewe pesa kwenye acount je? Wew umejipanga vipi ......
 
Mimi hata Kwa hivyo ni Sawa Tu as long as tunaweka terms vizuri
 
Wakuu salaam

Kuna ndugu yangu anataka kuanzisha biashara ya kununua FUSO zima la viazi vya chips / viazi ulaya/ viazi mviringo, Njombe na kuja kuuza Dodoma

Naomba Kwa mtu mwenye uzoefu au amewahi kufanya hii biashara atoe uzoefu wake

Hasa kwenye mambo ya soko kwenye kununua na kuuza
Kiongozi kama hutojali gharama ya kujaza fuso ya viazi huwa inafika kiasi gani kulingana na misimu?
 
Viazi vingi vinatoka njombe na vingne vinatoka mbeya kitu kingne Ni Kwamba Viaz Ni bidhaa inayoharibika haraka Sana so inahitaji soko la haraka vikikaa Sana utaishia kupata hasara

Wafanyabiashara wengi huchukua Viaz Kama tigo na cap na Obama hiv ndio hupendwa na wauza chips wengi coz havitumii mafuta mengi kuiva kwahyo itabid ununue aina hi ya viazi huko unakotaka kuchukua mzgo

Masokoni unakoenda kuuza Kuna madalali bila madalalsokoni huuzi mzgo wako utarud nao ulikotoka Kila ana wateja wake anaojuana nao so ukifika soon inabdi umpe dalali mzgo wako auze Yeye Kama wake ww unamwambia Kuna gunia Kama 100 unakaa zako pembeni baada ya siku 2 au 3 unapewa Pesa yako ukizubaa wengne wanakutapeli ukikutana na wasio waaminifu
 
Wakuu salaam

Kuna ndugu yangu anataka kuanzisha biashara ya kununua FUSO zima la viazi vya chips / viazi ulaya/ viazi mviringo, Njombe na kuja kuuza Dodoma

Naomba Kwa mtu mwenye uzoefu au amewahi kufanya hii biashara atoe uzoefu wake

Hasa kwenye mambo ya soko kwenye kununua na kuuza
Biashara ya viazi ni ngumu sana kwasababu kwanza inategemea na soko la siku hiyo pili usharp wa dalali wako na tatu ubora wa mzigo wako. Kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kwenda sokoni na kumpata dalali mwaminifu kitu cha pili nihuyo dalali kukupatia contact za wahusika kule viazi vinakotoka, hawa jamaa kule njombe ni waaminifu sana sijasikia hata siku moja wakimtapeli, ukitapeliwa ujue huyo siyo mfanya biashara wa viazi. kwa mara ya kwanza itabidi usafiri ili ufahamiane na mtu atakaye kufungia mzigo mnapatana naye gharama yakukufikishia mzigo mpaka kwenye gari, inamaana hapi yeye atasimamia, gharama za magunia, wachimbaji, wabebaji mpaka kwenye gari, pia huwa wanajuana na madalali wa magari kwahiyo hao hao wanakutafutia gari, pia inabidi ujue ujazo kutokana na sehemu unayopeleka mzigo wako la sivyo unaweza ukala hasara. Pua ujue gari unalochukua linabeba viroba vingapi na uhakikishe unakwenda kwenye mizani ya kulipia kuhakiki mzigo wako kwani mzigo ukizidi fine inakuwa yako wenye magari hawakubali kulipa fine.
 
Back
Top Bottom