Naomba mbinu za kumuangamiza kenge

Naomba mbinu za kumuangamiza kenge

Okay
Broo mshana kuchapwa na mkia wa kenge ni story tu za kusadikika mimi imenitokea sana utotoni lakini mpaka sasa na utu uzima nilionao hakuna madhara yoyote nimepata kwa kuchapwa na mkia wa kenge

Jr[emoji769]
 
Chemsha mayai kadhaa kisha fanya timming umtegeshee hapo anapoingilia kuja kula.

Ujinga wa kenge huwa yai analibugia na kulivunjia kooni. Yai lililochemshwa halivunjiki so akibugia lazma lita clog njia ya hewa atabaki anatapa tapa mpaka kufa kwake.
Aiseeeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni heri ungeboresha banda lako pia maana kama kaweza kuingia kenge na nyoka watakuwa wanaingia.
 
Ngozi nyeusi bana, naona jamaa hapo kaweka picha kamuua kenge alafu anaona ni ufahari.

Kule Nchi za wenzetu a.k.a Mabeberu kuna idara za Wanyama na kama kuna kiumbe yupo Nyumbani kwako unawapigia wanakuja kumchukua.

Wenzetu hawazingatii sana kwenye kuwauwa viumbe, unless kama unafanya hivyo kuokoa maisha yako, tofauti kabisa na huku kwetu, kule Wananchi wenyewe wanajitahidi sana na kuhakikisha Kiumbe anachukuliwa akiwa hai.

Niliangaliaga hii clip, jamaa anavyohangaika kumtoa Nyoka nyumbani akiwa hai wala hakufikiria kumuua....nikajiuliza ni Mbongo gani atafanya hivi?

KWA MWENYE CHANGAMOTO YA BANDO, HIYO HAPO JUU INA DK 12, HII YA CHINI INA DK 1 TU.
 
Chemsha mayai kadhaa kisha fanya timming umtegeshee hapo anapoingilia kuja kula.

Ujinga wa kenge huwa yai analibugia na kulivunjia kooni. Yai lililochemshwa halivunjiki so akibugia lazma lita clog njia ya hewa atabaki anatapa tapa mpaka kufa kwake.
Ni ushauri mzuri, ila ugumu uko kwenye "timing", mayai yawezakaa mpaka yakapoa na kenge asitokee!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mikenge mikibwa aisee mayai ya kuku anameza hata lisipopasuka

Dawa nzuri nikulipiga yai sindano ya sumu kisha tega maeneo unahisi anapitaga
 
Ni ushauri mzuri, ila ugumu uko kwenye "timing", mayai yawezakaa mpaka yakapoa na kenge asitokee!

Sent using Jamii Forums mobile app
Yanatakiwa yawe katika normal temperature tu. Akigusa la moto si ataliacha kwa kuungua tu. Likishapoa ataona yako kawaida tu atabugia kilafi tu.
 
Chemsha mayai kadhaa kisha fanya timming umtegeshee hapo anapoingilia kuja kula.

Ujinga wa kenge huwa yai analibugia na kulivunjia kooni. Yai lililochemshwa halivunjiki so akibugia lazma lita clog njia ya hewa atabaki anatapa tapa mpaka kufa kwake.
Daaah...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naamini nimemshinda kenge kutafuna mayai kwa kuzungushia nyavu ya samaki yenye kipimo cha "ply 18" ambayo ina urefu wa mita 40 na dukani ni Tsh 18, 500.

Nimepigilia miti au fito nene meter 3 au zaidi kwa hatua kuzungushia eneo. Chini ya nyavu nimefukia ili asipenye kwa chini na juu ili nyavu ikae sawa nimeingizia kamba ya nylon inauzwa buku 2 utefu wa kutosha.

Nyavu yenyewe ni rangi ya blue. Siku moja nilimwona kenge ananyatia sikumfukuza ila alihangaika sana. Alijaribu kuitafuna alishindwa
Alijaribu kuingia kibabe ichanike akashindwa, akaamua kuondoka.

Hivyo dawa ya kenge ni hizo nyavu za kuvulia samaki zipo kariakoo. Kenge hawezi kuipanda

Clip ya Extrovet imenielimisha sana pia.
Kenge anataga mayai mengi utatega utachoka.

Toka nimeweka hiyo nyavu nina miezi 2 sijaona kenge kuingia.
 
Ngozi nyeusi bana, naona jamaa hapo kaweka picha kamuua kenge alafu anaona ni ufahari.

Kule Nchi za wenzetu a.k.a Mabeberu kuna idara za Wanyama na kama kuna kiumbe yupo Nyumbani kwako unawapigia wanakuja kumchukua.

Wenzetu hawazingatii sana kwenye kuwauwa viumbe, unless kama unafanya hivyo kuokoa maisha yako, tofauti kabisa na huku kwetu, kule Wananchi wenyewe wanajitahidi sana na kuhakikisha Kiumbe anachukuliwa akiwa hai.

Niliangaliaga hii clip, jamaa anavyohangaika kumtoa Nyoka nyumbani akiwa hai wala hakufikiria kumuua....nikajiuliza ni Mbongo gani atafanya hivi?

AU IPO HII YENYE DAKIKA 1 KWA MWENYE CHANGAMOTO YA BANDO, HIYO HAPO JUU INA DK 12.

Huyo angekula vitofa vya hela yote, akitoka hapo kapasuka kichwa na utumbo wote nje
 
Back
Top Bottom