Naomba mkopo wa tsh 20,000

Angekuwa na location, ningempelekea mkono kwa mkono. Kutuma kwa Mpesa una reveal identity yako.
 
Wee tulaumu tuu ,Sawa broo ila unasahau haraka sana.
Huna sababu weukijiskia kuomba unaomba tuu au sisi ni mashemegi zako acha kutuzoeya vibaya broo wewe hata usiku mda mwingi uko on bando unatoa wapi ?
@mods anajaza server huyu
 
Nimeomba mara nyingi kwa unyenyekevu, lakini badala ya kupata msaada, ninachokutana nacho ni maneno makali, dharau na hukumu. Ukweli ni kwamba kila mtu ana changamoto zake, na hakuna anayependa kujikuta katika hali ngumu. Sijamlazimisha mtu yeyote kunisaidia, nimeomba kwa sababu nina uhitaji. Kama hakuna mwenye uwezo wa kunisaidia, nitapokea hali hiyo kwa moyo wa subira. Naomba tu utu uzingatiwe, kwani maisha hubadilika na leo yangu inaweza kuwa kesho ya mwingine. Yote ni maisha tu, Mungu ndiye anayejua kesho yetu.
 
Moderator hawa wahuni wanaotumia Jukwa kutapeli watu mngekua mnawapiga ban aisee haiwezekani mtu ana Id kadhaa za kuombea tu na si kutaka kazi sio kweli..
Muhuni akiamka tu anaanza na 20K keshokutwa 25k ngoma za kizamani sana hizi.
 
Kwa kweli, ndani ya moyo wangu nimeumia sana. Si rahisi kupitia changamoto nyingi maishani, halafu badala ya kupata faraja, unakutana na dhihaka, kejeli na maneno ya kukudhalilisha. Nimeomba msaada mara nyingi, lakini sikuwahi kufikiria kwamba hali yangu ingenifanya nionekane mtu asiye na thamani mbele ya wengine. Mimi ni binadamu kama walivyo wengine, nina hisia na heshima yangu. Sina nia ya kujidhalilisha wala kuwasumbua watu, bali nimekuwa nikipambana na hali ngumu ya maisha. Naomba mtambue kwamba shida ni sehemu ya maisha, na leo ni mimi, kesho inaweza kuwa mwingine. Mungu anajua kila ninachopitia. 💔
 
Yaani nani apoteze muda wake kwa hiyo takataka!
 
Moderator hawa wahuni wanaotumia Jukwa kutapeli watu mngekua mnawapiga ban aisee haiwezekani mtu ana Id kadhaa za kuombea tu na si kutaka kazi sio kweli..
Muhuni akiamka tu anaanza na 20K keshokutwa 25k ngoma za kizamani sana hizi.
Ninaelewa hasira yako na hoja yako, lakini si kila mtu anayeomba msaada ni tapeli. Kuna watu wanapitia changamoto za kweli ambazo si rahisi kuzielezea. Mimi sijafungua ID nyingi kwa ajili ya kuomba msaada, wala sina nia ya kumtapeli mtu yeyote. Kama nimekukosea kwa namna yoyote, naomba radhi. Naomba tuheshimiane na tuepuke kuhukumu maisha ya mtu bila kujua ukweli wote. Shida ni ya muda, na kila mmoja ana mapambano yake. 🙏
 
😂😂😂 nimemfanyia ushawishi kwa nyie watu wema, mmeshindwa na kukataa katu katu kutoa msaada,

Sasa nikimpitisha njia zangu, sitaki kelele na mibwato yenu ya kinafiki.
😂😂😂
Ohooooo hizo njia zenu ni ngumu sana zinahitaji uwe umekunywa damu ya binadamu aliyekufa mwaka mmoja mbele ayaweze🥹🥹eishhhh hasa masharti ya shoga yako bichwa komwe yule mpumbavu sana mpaka Leo PM naichukia kuiangalia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…