:confused2:
Umewahi kuingia dukani then ghafla wateja wakajaa hat kama hujanunua bado unachaguachagua?Jambo hili lishanitokea mara kwa mara,na mwenye duka mmoja alilinote sijui au sijui alijuaje lakini kila nikipita lazima aniite na kunitaka ni ninunue chochote hata kwa kukopa kama sikopi basi ninywe hata soda kwa bili yake.Kwa kuwa ni mwanaume nilifikiria vingine,ila kila nilipoendelea kumchunguza sikuona dalili ya zaidi ya uteja.Siku moja nilipita akawa yupo mfanyakazi wake,nikamhoji kuhusu bosi wake kuniitaita kila mara.Ndio nikaujua ukweli,eti mm nikingia tu wateja wanajaa na mauzo yavuka wastani wa siku zote.Niliamua kubadili njia kwani nihisi sasa naweza kufanyiwa yaliyowakuta ndugu zetu maalbino.Ila nilipojifuatilia mimi binafsi,ni kweli nikiingia kwenye biashara ya mtu,iwe dukani,sokoni,mitumbani nk,watu wanajaa sana kwa ghafla.Hata sijielewi,na sijui niamini lipi wapendwa