Mr Bakari Yusuph
Member
- May 19, 2024
- 10
- 7
Chanzo mtandaoni
UTANGULIZI
Ni watoto wetu ni tegemeo letu la Tanzania tuitakayo hawa ndio wasomi na madaktari wetu Hawa ndio wanajeshi na polisi wetu na hawa ndio wasanii wetu na wachezaji wetu wa miaka ya hivi karibuni .Kwa takribani Miongo kadhaa vyombo vya habari mbali mbali vimeripoti matukio juu ya watoto wakifanyiwa ukatili mkubwa na wakutisha Kubakwa,kulawitiwa,Kukatwa kwa viungo vyao ,Ndoa za utotoni, ukeketaji pamoja na ajira za utotoni imekuwa ikileta usalama mdogo kwa watoto wetu ambao ndio muhimili wa Taifa la nchi yetu hapo baadae je tutafika kweli ?
Mauji Kwa watoto wenye Ualibino
Tanzania na watanzania wameshuhudia visa na matukio mbali mbali juu ya mauji na ukataji wa viungo vya watoto wenye ulemavu wa ngozi katika maeneo mbali mbali jambo hili Lina tia mashaka kwa usalama wa watoto Hawa na wajui ni wapi wakimbilie.
Chanzo mtandaoni
Kulawitiwa na kubakwa kwa watoto
Kumekuwa na wimbi kubwa mno la watoto kuingiliwa kinyume na mbile na wengine kubakwa katika jamii Tena wanaofanyia hivyo wakiwa ni ndugu zao wa karibu wakiwemo Baba ,wajomba je Hawa watoto ambao ndio tegemeo letu nani wakuwalinda?
Chanzo mtandaoni
Ukeketqji wa Watoto wa Kike
Kumekuwa na ongezeko kubwa la ukeketaji katika mikoa ya Dodoma, Manyara, na Kanda ya ziwa Hali ambayo inapelekea vifo na maambukizi ya ukimwi pamoja na Watoto wa kike kukosala Usalama je ninani wa kuwalinda na waende wapi.
Chanzo mtandaoni
Ndoa za Utotoni
Ni Hali ya juu wa ukiukwaji wa haiki na katiba ya nchi kwa kuwa uzesha watoto wenye umri chini ya miaka 18 hali hii limekuwa janga la kitaifa linalooelekea watoto kukosa elimu na malezi Bora watoto wanteseka nani wakuwalinda.
Chanzo mtandaoni
Tutawalinda vipi watoto ambao ndio tegemeo la Taifa letu la baadae na wasilisha kwenu watanzania
NILINDE DATA BASE
Mfumo wa ukusanyaji wa taarifa za maendelea ya watoto katika kila kaya nchini ambapo hufanyika kila weekend ya mwisho wa mwezi kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18.
MIPANGO MKAKATI YA MFUMO
1.Kuundwa kwa bodi ya wataalam na uongozi wa kusimamia na kuendesha maisha ya mfumo ambapo kutakuwa na wajumbe mwenyekeki wakuu wa idara wataalam kama Wanasaikolojia, Maafisa maendelea ,wanasheria na waendesha mifumo.
2.Ukusanyaji wa Kazi data kwa Kila kaya juu ya maendeleo ya watoto:
Wanasaikolojia, Maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata adi mtaa kuukusanya taarifa za maendele ya watoto na kuziweka katika mfumo
3.Taarifa Hitajika kwa watoto
I Usalama wake
Ii Haki zake za msingi
iii Uchunguzwe juu ya Saikolojia yake
iv Apimwe mimba
V Apimwe afya ya maumbile ya haja kubwa
Uchambuzi wa Taarifa ufanyike na ubaini kaya zenye watoto walio katika Hatari
Kupitia taarifa zilizo kusanywa na wataalam na kuchambuliwa pamoja na vipimo vya madictor vibaini ni watoto na kaya zipi zipatiwe uangalifu yakinifu.
Kuundwe kwa chombo Cha kisheria cha kufuatilia kesi zote ambazo zimebainika:
Serikali kupitia mfumo huu iunde na utoe mamlaka wa kuwa na nguvu ya kuwakamata na kuwapeleka wahusika wa haki za watoto chombo hichi kiwe na wanasheria ,wanasaikolojia ,jeshi la polisi.
HII NDIO TANZANIA TUITAKAYO 2025
Attachments
Upvote
4