Naomba mnisaidie wingi wa Maneno haya

U
Kwanza ulimwengu ni mmoja tu so hauna wingi. Hakuna ulimwengu zaidi ya mmoja.
Pili
Uchumi wingi wake ni CHUMI.
MFANO. Uchumi wa nchi yetu unakuwa maradufu ukilinganisha na chumi za nchi nyingine Africa Mashariki
Ulimwengu si ndio universe?
Universe zipo nyingi Tu mbona
 
Ulimwengu(the universe) sidhani kama Kuna ulimwengu mwingine labda tumuulize doctor Stephen strange🤣
Ni kweli ila wakiwemo watu , wamiliki wa ulimwengu tunaita walimwengu, pia nasikia zipo universe nyingine bwashee šŸ˜‚
 
Asante,Niliuliza kwa sababu nilimsikia mwalimu fulanj wa neno la Mungu akisema kuna ulimwengu wa mwili na ulimwengu wa roho halafu akasema hizo ni 'nyulimwengu' tofauti

Kwahio niliuliza wingi kwakua alitumia ulimwengu kwa muktadha huo
 
Mimi nimewasikia wakenya mara kadhaa wakitumia neno Chumi kama wingi wa uchumi
Sawa,ila mpaka sasa sijajua neno sahihi ni lipi maana watu wamegawanyika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…