mtu akikuuliza ''haujambo'' unajibu ''sijambo'' ukimaanisha hauna tatizo,je, ukiwa na tatizo utajibu vipi?namaanisha kinyume cha neno sijambo katika salamu.
Ninajambo? Hapana. Sijambo haimaaanishi kuwa ni kinyume cha nina jambo. Unazijua irregular verbs kwenye Kiingereza? Na-suspect hii ni mojawapo kwenye Kiswahili. So far, tatizo lililopo kwenye lugha ya Kiswahili, wataalamu wake hawajawahi kutuambia hata siku moja kama irregular verbs zina-exixst kwenye lugha hii au hapana. Hadi inanishangaza kuona kuwa kuna neno limejitokeza siku hizi, eti kivumishi cha ONA ni ONESHA, na si ONYESHA. Why not this one being an irregular type of verb in Swahili? Kwa sababu ukinambia kuwa kivumishi cha ONA ni ONESHA, nashindwa kupata picha vizuri kwa sababu mimi ninavyoelewa ONESHA maana yake ni kufanya kiungo/kitu kisichoona kione, kama vile kufunua jicho la kipofu lisiloweza kuona halafu likaona, hapo utakuwa umefanya kitendo cha kuonesha, yaani kuwezesha kile kisichoona kiweze kuona. Anyway mawazo yangu!
Nasalimia wanaJF; Furaha yangu kuungana mkono katika kutafuta uwepesi na msemiyati ya lugha......mtu akikuuliza ''haujambo'' unajibu ''sijambo'' ukimaanisha hauna tatizo,je, ukiwa na tatizo utajibu vipi?namaanisha kinyume cha neno sijambo katika salamu.
neno ONYESHA lnatokana na neno ONYA,
Unajibu hivi "Taabani"mtu akikuuliza ''haujambo'' unajibu ''sijambo'' ukimaanisha hauna tatizo,je, ukiwa na tatizo utajibu vipi?namaanisha kinyume cha neno sijambo katika salamu.
Unajibu hivi "Taabani"
Nasalimia wanaJF; Furaha yangu kuungana mkono katika kutafuta uwepesi na msemiyati ya lugha......
Nafikiri tukirudi nyuma tutapata maana ya maneno mengi...Rudia lugha mama. kiswahili ni mtoto wa lugha ya wazazi wawili huwezi kukimbia kiini cha msemiti.
mkuu nakutakia heri..nina maanisha msaada hupatikana ktk. References....life is short sijakuelewa mzee!?
Hydle Hapana, siyo kweli,hicho ndicho ninachokataa tangu mwanzo.
Mara ngapi umewahi kusikia mtu ametumia neno onyesha kwa maana ya kuonya? Chukua real life sitution na si kuangalia mnyumbulisho wa neno tu bila kujali maana yake katika uhalisia. Nisome vizuri katika post yangu ya kwanza. Una-fall for the obvious pasipo kuangalia maana halisi ya matumizi ya neno katika uhalisia. Yaani umerudia kile kile ambacho nilianza kwa kukipinga ili usjie ukakifanya, sasa na wewe tena unafanya hivyo hivyo ?
Ainisha viambishi vya maneno yafuatayo:
a. alionyesha
b. alionesha
a. alionyesha
a- Nafsi ya tatu umoja
me - njeo wakati uliopita
ony- mzizi wa neno
esh - kauli ya kutendesha
a - kaiambishi tamati
hali kadhalika kwenye neno alionesha mzizi utakua "on" ingawa viambishi vingine vitabaki kama vilivyo.
Kumbuka neno la kiswahili maana halisi inapatikana kwenye mzizi wake na si vinginevyo.
Nakushauri kama unapenda lugha ya kiswahili jizoeze kuizungumza na kuiandika bila kuchanga na lugha za kigeni kama unavyoofanya.
Ndiyo maana nikasema ukiangalia unyambulishaji pamoja na analysis ya vitenzi vyenyewe kama vilivyo, perfect 100% uko sawa. Lakini ukirudi katika uhalisia, au practically, ulishawahi kusikia mtu ametumia neno onyesha kwa maana ya ku-onya? Unataka kuniambia kuwa hii ni common mistake in Swahili? Tupeni irregular verbs kwenye Kiswahili kwanza tuzijue ndiyo tutakubaliana na huo unyumbulishaji, otherwise mimi nachukulia, ona na onya kama irregularities kwenye kiswahili, na ziko sahihi kana zilivyokuwa zinatumika hapo awali na si katika hii new invention ya kusema maonyesho yanakuwa maonesho, and I hate the idea, finish!
Nimepata kusikia watu wakijibu: "sijambo kidogo/kiasi", "sijambojambo", "nasumbuliwa na [anataja tatizo, mf 'mafua', 'homa' nk]", "shida tupu" , "hivyo hivyo tu" nk nk. Usishangae pia vijana wa sasa wanaweza kuitikia kwa kusema "majanga tu".mtu akikuuliza ''haujambo'' unajibu ''sijambo'' ukimaanisha hauna tatizo,je, ukiwa na tatizo utajibu vipi?namaanisha kinyume cha neno sijambo katika salamu.
Ndiyo maana nikasema ukiangalia unyambulishaji pamoja na analysis ya vitenzi vyenyewe kama vilivyo, perfect 100% uko sawa. Lakini ukirudi katika uhalisia, au practically, ulishawahi kusikia mtu ametumia neno onyesha kwa maana ya ku-onya? Unataka kuniambia kuwa hii ni common mistake in Swahili? Tupeni irregular verbs kwenye Kiswahili kwanza tuzijue ndiyo tutakubaliana na huo unyumbulishaji, otherwise mimi nachukulia, ona na onya kama irregularities kwenye kiswahili, na ziko sahihi kana zilivyokuwa zinatumika hapo awali na si katika hii new invention ya kusema maonyesho yanakuwa maonesho, and I hate the idea, finish!
Kila lugha ina isimu yake ambayo hata kama katika matumizi ya kawaida watu hawaitumii lakini bado itaendelea kubaki hivyo. tofautisha mazoea hata kama ni makosa na isimu ya lugha. kuna misamiati mingi ya kiswahili ambayo watumiaji wengi wa kiswahili hawaijui au hawaitumii lakini hiyo haifanyi misamiati hiyo kuwa batili.
Ikiwa unakipenda kiswahili ungekuwa na desturi ya kukitumia bila kuchanganya na lugha nyingine, kwa kufanya hivyo labda ungefanya baadi ya watu waanze kudhani na wewe ni mmahiri wa kiswahili lakini kwa kuchangaya lugha mbili inaashiria hata unachodhani ni sahihi labda hata hujui ni kwa nini kiko hivyo.
Makanyaga salaam. Nimeogopa kuchangia kutokana na msimamo wako wa dhahiri kwamba unayo majumuisho/majibu tayari. Unachojaribu kufanya sasa ni kutafuta idadi ya watu utakaojibizana nao ilikuhalalisha yale uliyo nayo kama majibu. Sitaki kutumbukia katika mtego huo lakini nifanye masahihisho madogo kwenye uzi wako wa awali. Neno'ONESHA' si kivumishi. Halijapata kuwa katika kategoria hiyo na wala halitawahi. Si kimuundo tu bali hata kisemantiki na kimuktadha.
Wamogori;
Naomba nilulize swali moja kwa Kiingereza, na jingine kwa Kiswahili, halafu unijibu kwa Kiswahili, naogopa kuchanganya lugha mbili katika kuuliza swali hilo.
1. Where are the irregular verbs in swahili? Do they exist anyway? If not why? Do not you see the likelyhood that the swahili verbs ona and onya might fall in the category of such verbs?
2. Hayo matumizi siku zote miaka nenda rudi tumekuwa tukitumia neno maonyesho badala ya hilo mnalolipigia upatu sasa hivi la maonesho, ina maana siku zote hizo wataalamu wa Kiswahili walikuwa hawajaliona hilo?
Hii issue ya ni kitaaluma. Kwa nini iibuke ghafla tu namana hii kama ulivyoibuka mgogoro wa kuchinja nyama?