Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 11,129
- 7,321
Tatizo unalokumbana nalo ni kutaka kulazimisha sarufi ya kiswahili irandane na sarufi ya kingereza, ukilazimisha hivyo lazima ukumbane na ugumu kwani si kila kitu kitafanana. Kumbuka lugha yoyote ina sifa ya kukua ndio maana hata kingereza cha zamani si sawa na kingereza cha sasa. vivyo hivyo na kiswahili nacho cha msingi ni kuzingatia mzizi wa neno kulingana na sarufi ya kiswahili. Kumbuka sarufi ya kiswahili sio sawa na sarufi ya kingereza.
Root cause ya swali langu, je ni kwa nini hili neno tunalojadili hapa halikuwa siyo sahihi tangu mwanzo mpaka juzi tu? Ukuaji wa lugha si unaendana na kuongezeka kwa maneno mapya na si kuanzisha matumizi tofauti kwa neno ambalo limekuwepo siku zote, na wla si kulinyang'anya neno ile maana yake ya awali liliyokuwa likiitumikia siku zote?