naomba msaada hapa watu wa lugha.

naomba msaada hapa watu wa lugha.

Tatizo unalokumbana nalo ni kutaka kulazimisha sarufi ya kiswahili irandane na sarufi ya kingereza, ukilazimisha hivyo lazima ukumbane na ugumu kwani si kila kitu kitafanana. Kumbuka lugha yoyote ina sifa ya kukua ndio maana hata kingereza cha zamani si sawa na kingereza cha sasa. vivyo hivyo na kiswahili nacho cha msingi ni kuzingatia mzizi wa neno kulingana na sarufi ya kiswahili. Kumbuka sarufi ya kiswahili sio sawa na sarufi ya kingereza.

Root cause ya swali langu, je ni kwa nini hili neno tunalojadili hapa halikuwa siyo sahihi tangu mwanzo mpaka juzi tu? Ukuaji wa lugha si unaendana na kuongezeka kwa maneno mapya na si kuanzisha matumizi tofauti kwa neno ambalo limekuwepo siku zote, na wla si kulinyang'anya neno ile maana yake ya awali liliyokuwa likiitumikia siku zote?
 
mtu akikuuliza ''haujambo'' unajibu ''sijambo'' ukimaanisha hauna tatizo,je, ukiwa na tatizo utajibu vipi?namaanisha kinyume cha neno sijambo katika salamu.
What about if you are asked 'good morning' wont your response be 'good morning?
Kiungwana mnapoonana kwa mara ya kwanza ni budi kwanza kusalimiana hata kama kuna msiba na baada ya kusalimiana ndipo mtu aanzapo kumueleza mwenzake aidha ya msiba, kuumwa nk.
 
Root cause ya swali langu, je ni kwa nini hili neno tunalojadili hapa halikuwa siyo sahihi tangu mwanzo mpaka juzi tu? Ukuaji wa lugha si unaendana na kuongezeka kwa maneno mapya na si kuanzisha matumizi tofauti kwa neno ambalo limekuwepo siku zote, na wla si kulinyang'anya neno ile maana yake ya awali liliyokuwa likiitumikia siku zote?

neno hilo lilikuwepo isipokuwa athari ya matamshi na maandishi ndilo lilisabababisha watu waandike tofauti na linavyostahili na kujikuta likipata mvumo ktk jamii kwa maana isiyostahiki. Kipindi cha nyuma hakukuwa na wataalam wengi wa lugha ya kiswahili hivyo watu wengi hawakuona tatizo la matumizi ya neno hilo tofauti na sasa ambapo kuna wataalamu wengi wa lugha ya kiswahili.
 
TUKI ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unaijua? Unajua ipo na wataalamu waliobobea kwenye Kiswahili tangu lini? Nipe hoja zenye tija ili niweze kukubaliana na wewe
 
TUKI ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unaijua? Unajua ipo na wataalamu waliobobea kwenye Kiswahili tangu lini? Nipe hoja zenye tija ili niweze kukubaliana na wewe

TUKI ina wataalamu waliobebea tangu kuanzishwa kwake ila idadi yao inaongezeka siku hadi siku, na ni hao hao ndio waliokuja na hii tafsiri na msisitizo. Rejea kamusi ya TUKI kuhusu maneno hayo:-

ony.a kt [ele] 1 warn, admonish. 2 forbid, prevent. (tde) onyea; (tdk) onyeka; (tdn) onyana; (tds) onyesha; (tdw) onywa.

on.a kt [ele] 1 see: Kusikia si ku~ hearing is not the same as seeing. 2 feel: Na~ njaa I am feeling hungry. (tde) onea; (tdk) oneka; (tdn) onana; (tds) onesha; (tdw) onwa.

[FONT=arial, helvetica, sans-serif]"Kamusi hii imetayarishwa na wataalamu wa leksikografia wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Aidha, imepitiwa na kuhakikiwa na wataalamu wa lugha na isimu kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya Tanzania na Kenya.Uandishi wa Kamusi hii ulianza rasmi mwaka 1997 na kukamilika mwaka 2000. Ina vitomeo (maneno yanayofafanuliwa) zaidi ya 30,000."[/FONT]
 
Ndiyo maana nikasema ukiangalia unyambulishaji pamoja na analysis ya vitenzi vyenyewe kama vilivyo, perfect 100% uko sawa. Lakini ukirudi katika uhalisia, au practically, ulishawahi kusikia mtu ametumia neno onyesha kwa maana ya ku-onya? Unataka kuniambia kuwa hii ni common mistake in Swahili? Tupeni irregular verbs kwenye Kiswahili kwanza tuzijue ndiyo tutakubaliana na huo unyumbulishaji, otherwise mimi nachukulia, ona na onya kama irregularities kwenye kiswahili, na ziko sahihi kana zilivyokuwa zinatumika hapo awali na si katika hii new invention ya kusema maonyesho yanakuwa maonesho, and I hate the idea, finish!

Mkuu kuona watu wengi kwa muda mrefu wanatumia neno isivyo sahihi inatosha kuhalalisha matumizi yake!? je itakuwa sahihi kuegemea kwenye mazoea ya watu na si uhalisia wa kimuundo wa maneno!?
 
Mkuu kuona watu wengi kwa muda mrefu wanatumia neno isivyo sahihi inatosha kuhalalisha matumizi yake!? je itakuwa sahihi kuegemea kwenye mazoea ya watu na si uhalisia wa kimuundo wa maneno!?

Kwenye mtihani nitafuata Kamusi, kwenye kuongea na mambo mengine ambayo hayako subject to examination, nitatumia neno lililozoeleka siku zote. So far sijawa convinced na hoja.
 
Maada kama hii ukiwawekea vijana wa sasa hawatakuelewa hata kidogo badala yake utawaskia[oya mwanangu sio ishu we potezea kama vipi kwani kesi?]
 
Kwenye mtihani nitafuata Kamusi, kwenye kuongea na mambo mengine ambayo hayako subject to examination, nitatumia neno lililozoeleka siku zote. So far sijawa convinced na hoja.

siku ukienda kuomba kazi kwa mzungu usiandike barua kwa kiswahili andika kwa kiingereza kwani hatokuelewa.mfano utasema ''nilikuwa naomba kazi'' atajua umeshapata.bora lugha yake kwasababu hata ukipindisha au ukikosea atakuelewa zaidi kwa lugha aliyozaliwa nayo kuliko aliyosoma.nadhani nimeeleweka?
 
Back
Top Bottom