naomba msaada hapa watu wa lugha.

naomba msaada hapa watu wa lugha.

hydle

Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
63
Reaction score
8
mtu akikuuliza ''haujambo'' unajibu ''sijambo'' ukimaanisha hauna tatizo,je, ukiwa na tatizo utajibu vipi?namaanisha kinyume cha neno sijambo katika salamu.
 
Ninajambo? Hapana. Sijambo haimaaanishi kuwa ni kinyume cha nina jambo. Unazijua irregular verbs kwenye Kiingereza? Na-suspect hii ni mojawapo kwenye Kiswahili. So far, tatizo lililopo kwenye lugha ya Kiswahili, wataalamu wake hawajawahi kutuambia hata siku moja kama irregular verbs zina-exixst kwenye lugha hii au hapana. Hadi inanishangaza kuona kuwa kuna neno limejitokeza siku hizi, eti kivumishi cha ONA ni ONESHA, na si ONYESHA. Why not this one being an irregular type of verb in Swahili? Kwa sababu ukinambia kuwa kivumishi cha ONA ni ONESHA, nashindwa kupata picha vizuri kwa sababu mimi ninavyoelewa ONESHA maana yake ni kufanya kiungo/kitu kisichoona kione, kama vile kufunua jicho la kipofu lisiloweza kuona halafu likaona, hapo utakuwa umefanya kitendo cha kuonesha, yaani kuwezesha kile kisichoona kiweze kuona. Anyway mawazo yangu!
 
neno ONYESHA lnatokana na neno ONYA,
 
mtu akikuuliza ''haujambo'' unajibu ''sijambo'' ukimaanisha hauna tatizo,je, ukiwa na tatizo utajibu vipi?namaanisha kinyume cha neno sijambo katika salamu.
Nasalimia wanaJF; Furaha yangu kuungana mkono katika kutafuta uwepesi na msemiyati ya lugha......
Nafikiri tukirudi nyuma tutapata maana ya maneno mengi...Rudia lugha mama. kiswahili ni mtoto wa lugha ya wazazi wawili huwezi kukimbia kiini cha msemiti.
 
neno ONYESHA lnatokana na neno ONYA,

Hydle Hapana, siyo kweli,hicho ndicho ninachokataa tangu mwanzo.
Mara ngapi umewahi kusikia mtu ametumia neno onyesha kwa maana ya kuonya? Chukua real life sitution na si kuangalia mnyumbulisho wa neno tu bila kujali maana yake katika uhalisia. Nisome vizuri katika post yangu ya kwanza. Una-fall for the obvious pasipo kuangalia maana halisi ya matumizi ya neno katika uhalisia. Yaani umerudia kile kile ambacho nilianza kwa kukipinga ili usjie ukakifanya, sasa na wewe tena unafanya hivyo hivyo ?
 
hujambo(huna jambo) sijambo (sina jambo). mfano hujambo? naumwa!. kuumwa ndo jambo.
siku hizi twasema "ni aje/nambie? shwari/poa. or nambie? ovyo mambo hayaeleweki. mia
 
Makanyaga salaam. Nimeogopa kuchangia kutokana na msimamo wako wa dhahiri kwamba unayo majumuisho/majibu tayari. Unachojaribu kufanya sasa ni kutafuta idadi ya watu utakaojibizana nao ilikuhalalisha yale uliyo nayo kama majibu. Sitaki kutumbukia katika mtego huo lakini nifanye masahihisho madogo kwenye uzi wako wa awali. Neno 'ONESHA' si kivumishi. Halijapata kuwa katika kategoria hiyo na wala halitawahi. Si kimuundo tu bali hata kisemantiki na kimuktadha.
 
Nasalimia wanaJF; Furaha yangu kuungana mkono katika kutafuta uwepesi na msemiyati ya lugha......
Nafikiri tukirudi nyuma tutapata maana ya maneno mengi...Rudia lugha mama. kiswahili ni mtoto wa lugha ya wazazi wawili huwezi kukimbia kiini cha msemiti.

life is short sijakuelewa mzee!?
 
Hydle Hapana, siyo kweli,hicho ndicho ninachokataa tangu mwanzo.
Mara ngapi umewahi kusikia mtu ametumia neno onyesha kwa maana ya kuonya? Chukua real life sitution na si kuangalia mnyumbulisho wa neno tu bila kujali maana yake katika uhalisia. Nisome vizuri katika post yangu ya kwanza. Una-fall for the obvious pasipo kuangalia maana halisi ya matumizi ya neno katika uhalisia. Yaani umerudia kile kile ambacho nilianza kwa kukipinga ili usjie ukakifanya, sasa na wewe tena unafanya hivyo hivyo ?

Ainisha viambishi vya maneno yafuatayo:
a. alionyesha
b. alionesha

a. alionyesha
a- Nafsi ya tatu umoja
me - njeo wakati uliopita
ony- mzizi wa neno
esh - kauli ya kutendesha
a - kaiambishi tamati

hali kadhalika kwenye neno alionesha mzizi utakua "on" ingawa viambishi vingine vitabaki kama vilivyo.
Kumbuka neno la kiswahili maana halisi inapatikana kwenye mzizi wake na si vinginevyo.

Nakushauri kama unapenda lugha ya kiswahili jizoeze kuizungumza na kuiandika bila kuchanga na lugha za kigeni kama unavyoofanya.
 
Ndiyo maana nikasema ukiangalia unyambulishaji pamoja na analysis ya vitenzi vyenyewe kama vilivyo, perfect 100% uko sawa. Lakini ukirudi katika uhalisia, au practically, ulishawahi kusikia mtu ametumia neno onyesha kwa maana ya ku-onya? Unataka kuniambia kuwa hii ni common mistake in Swahili? Tupeni irregular verbs kwenye Kiswahili kwanza tuzijue ndiyo tutakubaliana na huo unyumbulishaji, otherwise mimi nachukulia, ona na onya kama irregularities kwenye kiswahili, na ziko sahihi kana zilivyokuwa zinatumika hapo awali na si katika hii new invention ya kusema maonyesho yanakuwa maonesho, and I hate the idea, finish!
 
neno HAUJAMBO ni utamkaji tu wa mazoea bali hutamkwa HUJAMBO=HUNA JAMBO na unajibu SIJAMBO= SINA JAMBO hapo muulizaji upita kwa kuwa hauna tatizo. Kama unatatizo basi ungetakiwa ujibu NIJAMBO= NINA JAMBO. kwa kuwa neno hilo halijazoeleka kimatamshi si rahisi kulitamka na kueleweka haraka. Watu wengi kwa sababu ya mazoea tu hata kama amepigwa akiulizwa HUJAMBO HUJIBU SIJAMBO bila kuelewa wakati jibu ni NIJAMBO.
 
Ndiyo maana nikasema ukiangalia unyambulishaji pamoja na analysis ya vitenzi vyenyewe kama vilivyo, perfect 100% uko sawa. Lakini ukirudi katika uhalisia, au practically, ulishawahi kusikia mtu ametumia neno onyesha kwa maana ya ku-onya? Unataka kuniambia kuwa hii ni common mistake in Swahili? Tupeni irregular verbs kwenye Kiswahili kwanza tuzijue ndiyo tutakubaliana na huo unyumbulishaji, otherwise mimi nachukulia, ona na onya kama irregularities kwenye kiswahili, na ziko sahihi kana zilivyokuwa zinatumika hapo awali na si katika hii new invention ya kusema maonyesho yanakuwa maonesho, and I hate the idea, finish!

Kila lugha ina isimu yake ambayo hata kama katika matumizi ya kawaida watu hawaitumii lakini bado itaendelea kubaki hivyo. tofautisha mazoea hata kama ni makosa na isimu ya lugha. kuna misamiati mingi ya kiswahili ambayo watumiaji wengi wa kiswahili hawaijui au hawaitumii lakini hiyo haifanyi misamiati hiyo kuwa batili.

Ikiwa unakipenda kiswahili ungekuwa na desturi ya kukitumia bila kuchanganya na lugha nyingine, kwa kufanya hivyo labda ungefanya baadi ya watu waanze kudhani na wewe ni mmahiri wa kiswahili lakini kwa kuchangaya lugha mbili inaashiria hata unachodhani ni sahihi labda hata hujui ni kwa nini kiko hivyo.
 
mtu akikuuliza ''haujambo'' unajibu ''sijambo'' ukimaanisha hauna tatizo,je, ukiwa na tatizo utajibu vipi?namaanisha kinyume cha neno sijambo katika salamu.
Nimepata kusikia watu wakijibu: "sijambo kidogo/kiasi", "sijambojambo", "nasumbuliwa na [anataja tatizo, mf 'mafua', 'homa' nk]", "shida tupu" , "hivyo hivyo tu" nk nk. Usishangae pia vijana wa sasa wanaweza kuitikia kwa kusema "majanga tu".
 
Ndiyo maana nikasema ukiangalia unyambulishaji pamoja na analysis ya vitenzi vyenyewe kama vilivyo, perfect 100% uko sawa. Lakini ukirudi katika uhalisia, au practically, ulishawahi kusikia mtu ametumia neno onyesha kwa maana ya ku-onya? Unataka kuniambia kuwa hii ni common mistake in Swahili? Tupeni irregular verbs kwenye Kiswahili kwanza tuzijue ndiyo tutakubaliana na huo unyumbulishaji, otherwise mimi nachukulia, ona na onya kama irregularities kwenye kiswahili, na ziko sahihi kana zilivyokuwa zinatumika hapo awali na si katika hii new invention ya kusema maonyesho yanakuwa maonesho, and I hate the idea, finish!

makanyaga,usichanganye kiswahili na kiingereza,mchanganyiko huo ndio huitwa lugha ya kihuni.mfano,ticha samahani,hii ni lugha ya kihuni
 
Kila lugha ina isimu yake ambayo hata kama katika matumizi ya kawaida watu hawaitumii lakini bado itaendelea kubaki hivyo. tofautisha mazoea hata kama ni makosa na isimu ya lugha. kuna misamiati mingi ya kiswahili ambayo watumiaji wengi wa kiswahili hawaijui au hawaitumii lakini hiyo haifanyi misamiati hiyo kuwa batili.

Ikiwa unakipenda kiswahili ungekuwa na desturi ya kukitumia bila kuchanganya na lugha nyingine, kwa kufanya hivyo labda ungefanya baadi ya watu waanze kudhani na wewe ni mmahiri wa kiswahili lakini kwa kuchangaya lugha mbili inaashiria hata unachodhani ni sahihi labda hata hujui ni kwa nini kiko hivyo.

Wamogori;
Naomba nilulize swali moja kwa Kiingereza, na jingine kwa Kiswahili, halafu unijibu kwa Kiswahili, naogopa kuchanganya lugha mbili katika kuuliza swali hilo.

1. Where are the irregular verbs in swahili? Do they exist anyway? If not why? Do not you see the likelyhood that the swahili verbs ona and onya might fall in the category of such verbs?

2. Hayo matumizi siku zote miaka nenda rudi tumekuwa tukitumia neno maonyesho badala ya hilo mnalolipigia upatu sasa hivi la maonesho, ina maana siku zote hizo wataalamu wa Kiswahili walikuwa hawajaliona hilo?

Hii issue ya ni kitaaluma. Kwa nini iibuke ghafla tu namana hii kama ulivyoibuka mgogoro wa kuchinja nyama?
 
Makanyaga salaam. Nimeogopa kuchangia kutokana na msimamo wako wa dhahiri kwamba unayo majumuisho/majibu tayari. Unachojaribu kufanya sasa ni kutafuta idadi ya watu utakaojibizana nao ilikuhalalisha yale uliyo nayo kama majibu. Sitaki kutumbukia katika mtego huo lakini nifanye masahihisho madogo kwenye uzi wako wa awali. Neno'ONESHA' si kivumishi. Halijapata kuwa katika kategoria hiyo na wala halitawahi. Si kimuundo tu bali hata kisemantiki na kimuktadha.

Omonto;
Uko sawa. Ni aina fulani ya kitenzi ambacho sikumbuki jina lake, siyo kivumishi. Ahsante kwa taarifa. Nimeshachukua msimamo tayari kwa sababu ninataka ku-attract concrete reasoning ambayo itakuja kuni-prove kuwa niko wrong na nikaridhika kweli kwamba niko wrong, na si vinginevyo. Unajua tunataka kupelekwa sehemu ambayo hata leo mtu anaweza akaibuka akaema kuwa Kuku jina lake sahihi kwa Kiswahili ni Nyumbu na Nyumbu jina lake ni Paka, na watu tukafuata tu simply anayesema ni mtaalamu wa Kiswahili. Hii hapana, lazima tuhoji kwamba kama miaka yote hiyo nenda rudi tumekuwa tukijua kuwa mnyama so and so anaitwa Kuku na leo wewe unakuja kutueleza kuwa haitwi hivyo, hiyo miaka yote hapakuwa na wataalamu wa Kiswahili kuweza kutueleza hilo, miaka yote hiyo? Let's try to "lumbana" kwa hoja please!
 
Wamogori;
Naomba nilulize swali moja kwa Kiingereza, na jingine kwa Kiswahili, halafu unijibu kwa Kiswahili, naogopa kuchanganya lugha mbili katika kuuliza swali hilo.

1. Where are the irregular verbs in swahili? Do they exist anyway? If not why? Do not you see the likelyhood that the swahili verbs ona and onya might fall in the category of such verbs?

2. Hayo matumizi siku zote miaka nenda rudi tumekuwa tukitumia neno maonyesho badala ya hilo mnalolipigia upatu sasa hivi la maonesho, ina maana siku zote hizo wataalamu wa Kiswahili walikuwa hawajaliona hilo?

Hii issue ya ni kitaaluma. Kwa nini iibuke ghafla tu namana hii kama ulivyoibuka mgogoro wa kuchinja nyama?

Tatizo unalokumbana nalo ni kutaka kulazimisha sarufi ya kiswahili irandane na sarufi ya kingereza, ukilazimisha hivyo lazima ukumbane na ugumu kwani si kila kitu kitafanana. Kumbuka lugha yoyote ina sifa ya kukua ndio maana hata kingereza cha zamani si sawa na kingereza cha sasa. vivyo hivyo na kiswahili nacho cha msingi ni kuzingatia mzizi wa neno kulingana na sarufi ya kiswahili. Kumbuka sarufi ya kiswahili sio sawa na sarufi ya kingereza.
 
Back
Top Bottom