kijumbamshale
JF-Expert Member
- Apr 27, 2011
- 267
- 87
Ili kuuelewa mzunguko unahesabu hivi, siku anapopata bleed(damu inapotoka kwa mara ya kwanza) ndio unaihesabu ni siku ya kwanza. Ili kujua ana mzunguko wa siku ngapi unaendelea kuhesabu weeeee mpaka atakapopata tena bleed. Jumla ya hizo siku ndio mzunguko wake kwa hiyo kama hizo siku ni 21 tunasema ana mzunguko wa siku 21 kama ni 28 tunasema ana mzunguko wa siku 28 nk. Ili kujiridhisha kwamba mzunguko ni wa siku ngapi inabidi ufuatilie walau kwa miezi mitatu au zaidi kama ukipata idadi ya siku zinazofanana ndio unasema kwamba mzunguko ni wa siku 21au28au35. Kwa kawaida yai hupevuka katikati ya mzunguko hivyo baada ya kujua mzunguko ni wa siku ngapi then hizo siku ukigawanya kwa mbili ndio kipindi ambacho yai linakuwa tayari kwa kupokea mbegu. Kwa kuwa mbegu za kiume zinaweza kuishi siku tatu ukeni bila kufa kwa hiyo ukijamiiana siku tatu kabla ya siku ya yai kutolewa unaweza kupata ujauzito( ie siku za hatari zinaanzia siku 3 kabla ya hiyo siku ambayo ni ya katikati ya mzunguko) pia yai baada ya kupevuka pia linaweza kuishi kwa siku 3 hivyo siku 3 baada ya ile siku yetu ya katikati nazo ni za hatari. Kwa hiyo tuna jumla ya siku za hatari sita. Tatu kabla ya hiyo siku ya katikati na tatu baada.
Ukichukulia mfano mtu mwenye mzunguko wa siku 28, siku ya kwanza anapoanza kupata hedhi mpaka siku ya 10 zinakua sio siku za hatari siku ya 11,12,13 ni za hatari kwa kuwa zimekaribiana na siku ya kupevushwa yai ambayo ni siku ya 14. Baada ya yai nalo kupevushwa linaweza kukaa siku 3 kwa hiyo siku za hatari zinaendelea kuwa siku ya 14,15,16 na 17. Halafu inakua salama mpaka atakapo pata hedhi tena na kuanza mzunguko upya.
Angalizo hapa naongelea siku na wala sio tarehe za kalenda hedhi inaweza kuanza siku yeyote ile ila kwa kalenda ya hedhi ndio itahesabika siku ya kwanza.
Natumai nimeeleweka