Naomba msaada kuhusu hedhi.

Ili kuuelewa mzunguko unahesabu hivi, siku anapopata bleed(damu inapotoka kwa mara ya kwanza) ndio unaihesabu ni siku ya kwanza. Ili kujua ana mzunguko wa siku ngapi unaendelea kuhesabu weeeee mpaka atakapopata tena bleed. Jumla ya hizo siku ndio mzunguko wake kwa hiyo kama hizo siku ni 21 tunasema ana mzunguko wa siku 21 kama ni 28 tunasema ana mzunguko wa siku 28 nk. Ili kujiridhisha kwamba mzunguko ni wa siku ngapi inabidi ufuatilie walau kwa miezi mitatu au zaidi kama ukipata idadi ya siku zinazofanana ndio unasema kwamba mzunguko ni wa siku 21au28au35. Kwa kawaida yai hupevuka katikati ya mzunguko hivyo baada ya kujua mzunguko ni wa siku ngapi then hizo siku ukigawanya kwa mbili ndio kipindi ambacho yai linakuwa tayari kwa kupokea mbegu. Kwa kuwa mbegu za kiume zinaweza kuishi siku tatu ukeni bila kufa kwa hiyo ukijamiiana siku tatu kabla ya siku ya yai kutolewa unaweza kupata ujauzito( ie siku za hatari zinaanzia siku 3 kabla ya hiyo siku ambayo ni ya katikati ya mzunguko) pia yai baada ya kupevuka pia linaweza kuishi kwa siku 3 hivyo siku 3 baada ya ile siku yetu ya katikati nazo ni za hatari. Kwa hiyo tuna jumla ya siku za hatari sita. Tatu kabla ya hiyo siku ya katikati na tatu baada.

Ukichukulia mfano mtu mwenye mzunguko wa siku 28, siku ya kwanza anapoanza kupata hedhi mpaka siku ya 10 zinakua sio siku za hatari siku ya 11,12,13 ni za hatari kwa kuwa zimekaribiana na siku ya kupevushwa yai ambayo ni siku ya 14. Baada ya yai nalo kupevushwa linaweza kukaa siku 3 kwa hiyo siku za hatari zinaendelea kuwa siku ya 14,15,16 na 17. Halafu inakua salama mpaka atakapo pata hedhi tena na kuanza mzunguko upya.
Angalizo hapa naongelea siku na wala sio tarehe za kalenda hedhi inaweza kuanza siku yeyote ile ila kwa kalenda ya hedhi ndio itahesabika siku ya kwanza.
Natumai nimeeleweka
 
Anyway...
Nisaidieni wangu anaingia bleed kila tar 27,28,29 tar 30 alimalizia kidogo sana
sasa naomba mnisaidie anamzunguko wa siku ngapi na tareh yake ya hatari.
watu8, Chocs na wengine embu weken maneno hapa

Mkuu nimeshapata kuelezea sana hili jambo hapa...
Kesho nikipata wasaa nitaweka link ya moja ya uzi niliopata kufafanua hili..
 
Last edited by a moderator:

Thank u very much. U are so great.
 

wakuu nimewaelewa vizur mpaka nimefurah! Nashukuru kama kuna hajaelewa basi naomba asome vizuri!
Ok mim nina maswali ma 2 kama ntaeleweka
1.kama mtu anatatzo pre-mature ejaculation inakuwaje?

2. Nimekuwa nikimchunguza wife wangu kwa mda kidogo wakati wa maandaliz nikiingiza kidole kunako kwa uke ndani kabisa mbona sioni tundu la uzazi?
Sasa hizo mbegu zinaingiaje au ni kwa wote huwa wapo hivi au ni mim sio kwamba sjawah kuwa na madem kabla ya wife wangu mpendwa bali sikuwa na tension ya kufatilia hii kitu kule tulikuwa tunatafuta raha tu!!
na kuongezea alishapima autra-sound na tukakuta hamna tatzo
msaada kwa hili plz
naongezea na huyu MziziMkavu na wengine





 
Last edited by a moderator:
Leo niko customer service najibu timely,
Kuhusu premature ejaculation mara nyingi inahesabiwa ni pale ambapo mtu unakojoa ndani ya dakika tatu za mwanzo baada ya kuanza tendo. Mara nyingi ni saikolojia tu ndio inasababisha hivyo na mara nyingi sio ya kudumu kama mtu ana tatizo hilo ni vema akaijulisha akili yake kwamba anatakiwa kulidhibiti tatizo hilo. Akishindwa aanze kwa kutumia desinsetizers kama lignocane (stud) au condoms huwa zinasaidia kwa wale ambao vichwa vya mboo zao ni sensitive sana.


Kuhusu tundu la kupitishia mbegu, kama mkeo ana kizazi basi tundu lipo sema sio lazima liwe moja kwa moja inatofautiana kutoka mtu mmoja kwenda mwingine. Usiende kulitafuta bwana kwani unalihitaji la nini aiseee?
 
Mkuu swali la kwanza ( Pre-mature ejaculation) ukiwa na hilo tatizo unakuwa huwezi kulifurahia starehe yako ya ngono utakuwa wewe unamalizamapema kumwaga wakati mpenzi wako hajafika kileleni itakuwa wewe umemaliza lakini mwenzi wako hajamaliza kufika kileleni matokeo yake ndani ya ndoa ni ugomvi mtupu.

Na kuhusu swali lako la pili inakuwaje wewe umchunguze tundu yake Mke wako na umeona kuwa hana tundu kivipi? una wasiwasi hataweza kushika mimba? Unanishangaza hapo Je mke wako hajazaa bado?
 
Kuweka kumbukumbu sawa mzizi mkavu premature ejaculation haitegemei mke wako kufika, inategemea vitu viwili either unachovya mara ngapi mpaka kupiga bao au ni dkika ngapi zinakutosha kupata bao ndio maana kwenye post yangu nimetumia unit ya muda.
 
Asante sana ndugu zangu kwa elimu nzuri sana. Mbarikiwe sana.
 

ili niweke Mimba!
kwani kumchungza mkeo vibaya?



Yes bado hajazaa! Tulifanya vipimo hakuna tatzo! Kwan kumchunguza mkeo ni vibaya cha mcngi si muumizi au niulize hakuna aliyeambiwa kuwa kwa mwanamke kuna sehemu inaitwa G-spot inaleta msisimko asiende kuingiza kidole anchunguze wap hiyo kitu???
 
Ni matatizo wasipokuwa makin kwa maana mizunguko inabadilika 28,30,35 na bado kuna factor nyingne kama ugonjwa stress nk awe makin otherwise atamtundika mimba
 
mkuu samahan naomba urudie kidogo hapo uniacha
unamaana kuwa m/mke ana siku za kupata mimba mara 2??

1. Maelezo ya awali hayamaanishi kuwa binti anaweza kupata mimba mara mbili ila,
2. Je wajuwa? Binti anaweza kupata mimba mara mbili ndani ya mwezi mmoja au miwili pengine hata mitatu tangu mimba ya kwanza iingie. "HAPA HUZALIWA MAPACHA WASIOFANANA" Wanaoweza kuzidiana umri kati ya nusu saa hadi miezi mitatu hivi!
 

duh ndiyo hivi! Welldone presenters.
 
Siku zote ni salama kasoro siku ya 14 toka hedhi inaitwa fertile day or at risk day hata hivyo chukua tahadhari siku tatu nyuma na siku tatu mbele kwa ni sperm zinakaa hadi 72hrs kama pH medium za mwanamke na mwanamme zinalinga.

Kiongozi sasa unaniangusha, "We normally say fertile period" amabapo ni kipindi cha siku saba, yaani kuanzia siku ya 11 mpaka siku ya 18, ambayo hii imekuja kwa ukweli kwamba, uhai wa yai ni angalau masaa 36 na uhai wa mbegu angalau masaa 72 ongeza offset ya 48hours(24hours kabla ya kupopolewa/kuanguliwa yai na 24hours baada ya uhai wa yai .
 
Asante sana ndugu kwa shule yako nzuri. Kwa hyo una maana kuwa kwa mwezi unaofuata hataingia tarehe 08 kama mwezi huu bali ataanza kati ya tar 05 na 06?

Haswaaaaa! lakini kama ni mwezi Februari anaweza kuingia tarehe hiyo hiyo 8 ama tarehe 7.
 
Anyway...
Nisaidieni wangu anaingia bleed kila tar 27,28,29 tar 30 alimalizia kidogo sana
sasa naomba mnisaidie anamzunguko wa siku ngapi na tareh yake ya hatari.
watu8, Chocs na wengine embu weken maneno hapa
Mzunguko wake wa mwezi mzima ni siku ngapi...na sio siko ammbazo anakuwa menstrual


Yaani tarehe ya kwanza kuona mwezi jana ni tarehe ngapi mpaka tarehe ya mwezi huu ni tarehe ngapi? ili tuweze kuhesabu kuwa ana mzunguko wa siku ngapi ndani ya mwezi wake,sijui umenielewa gody
 
Last edited by a moderator:


no sory nilimaanisha kuwa mwanamke anaweza kuingia ktk Ovulation mara mbili kwa mwezi,
 


mwezi wa July-27, mwz Augst-27 na mwez sept -27 na ni siku tatu tatu kasoro
mwezi huu kaingia siku 4 lkn siku ya nne ilikuwa damu kidogo sana.
Sijui kama umenielewa.??
 
Last edited by a moderator:
no sory nilimaanisha kuwa mwanamke anaweza kuingia ktk Ovulation mara mbili kwa mwezi,

Haswaaaaaaa ndio msingi wa mapacha wasiofanana! Bado hujaelewa tu? Mbona maelezo yako wazi kaka.
 
Unajua watu wengi huwa hawajui kitu kimoja, kwamba yai la mwanamke laweza kuwahi au kuchelewa siku 2 kabla au baada ya siku 14 kwa wale wenye mzunguko wa siku 28. Kwa hiyo siku za hatari ni siku 11. Yaani kuanzia siku ya 9 hadi ya 19. Nafikiri umenielewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…