Inaonesha pia hata maji hayatoshi , piga maji ya kutosha pia dawa za ukungu muhimu pia jua huwa likiwa kali sana kuna ugonjwa huwa unaitwa "Kanitangaze" vidudu fulani hivi vinakula ndani ya majani panabaki na tissue nyeupe hivi kama nailoni !!
Issue za Bustani napiga sana ila nyanya nilishaacha aseee yaani nyanya inabembelezwa kila stage ya ukuaji ukiharibu kidogo inazima ! Kuanzia unapanda miche , inavyokua kadri majani yanavyokua , ikianza maua mpaka matunda ! Ukichuma mchumo wa kwanza ,huduma zikapungua inayumba ! Nyanya ni kama unahudumia mwanamke walah ! Na bei yake sokoni inafluctuate sana mwaka mmoja hivi nililima hekari moja ya maana Nilitumia mbegu ya IMARA ikanikubali bhana huduma yan VIP yaani zile chupa za dawa nilizokua napulizia nikizikusanya sehemu ungeshangaa nyingi balaa !! Ilizaa vibaya sana ! Kuingia sokoni bei iko chini nakumbuka ndoo(huku kwetu linaitwa dumu) ilikua 3000/= watu wanachagua nyanya ya kununua hiyo bei ni kwa nyanya safi ile inayovutia ukienda na chenga ni buku ndoo !! Bahati yangu ni kwamba huo mwaka ilinikubali nilichuma michumo 7 niko on fire ! Bado mingine kama minne ilikua chenga. Ilichonikera nyanya inataka attention sana na haitaki hela za mawazo !!!
Nilishageuza majeshi kwa sasa nadeal na vitu ambavyo siwi roho juu juu Bilinganya , Pilipili hoho na Nyanya chungu !! Nyanya nikilima nafanya tu ili kujiongezea ubusy na siwezi zidisha Robo hekari !!