Naomba msaada kuhusu nyanya

Naomba msaada kuhusu nyanya

hayolae

Senior Member
Joined
Sep 28, 2015
Posts
180
Reaction score
865
Ndungu zangu poleni na majukumu,Kwaa wale wataalamu wa nyanya naombeni msaada wa haraka juu ya hali hii inayoitesa nyanya yangu,ili angalau niweze kuiokoa.
1.Nyanya inanyauka majani kuanzia chini kwenda juu.
2.Maua yananyauka na kudondoka.
3.Maua yanakaa mda mrefu bila kutoa matunda.

aina ya mbengu ni asira, hali ya hewa iliyopo kwa sasa ni jua kali, vumbi sana na upepo mkali mda wote.
KIlimo ni chaumwagiliaji.

Natanguliza shukrani kwa yeyyote anaeweza nipatia ushauri au namna ninayoweza kuiokoa hii nyanya.
IMG_20230309_181334_682.jpg
IMG_20230309_181318_440.jpg
IMG_20230309_181255_142.jpg
IMG_20230309_181215_061.jpg
IMG_20230309_181147_632.jpg
IMG_20230302_174605_429.jpg
IMG_20230302_174754_783.jpg
IMG_20230302_174810_944.jpg
IMG_20230302_174546_239.jpg
 
Attachments

  • VID_20230221_183101.mp4
    11.1 MB
Inaonesha pia hata maji hayatoshi , piga maji ya kutosha pia dawa za ukungu muhimu pia jua huwa likiwa kali sana kuna ugonjwa huwa unaitwa "Kanitangaze" vidudu fulani hivi vinakula ndani ya majani panabaki na tissue nyeupe hivi kama nailoni !!

Issue za Bustani napiga sana ila nyanya nilishaacha aseee yaani nyanya inabembelezwa kila stage ya ukuaji ukiharibu kidogo inazima ! Kuanzia unapanda miche , inavyokua kadri majani yanavyokua , ikianza maua mpaka matunda ! Ukichuma mchumo wa kwanza ,huduma zikapungua inayumba ! Nyanya ni kama unahudumia mwanamke walah ! Na bei yake sokoni inafluctuate sana mwaka mmoja hivi nililima hekari moja ya maana Nilitumia mbegu ya IMARA ikanikubali bhana huduma yan VIP yaani zile chupa za dawa nilizokua napulizia nikizikusanya sehemu ungeshangaa nyingi balaa !! Ilizaa vibaya sana ! Kuingia sokoni bei iko chini nakumbuka ndoo(huku kwetu linaitwa dumu) ilikua 3000/= watu wanachagua nyanya ya kununua hiyo bei ni kwa nyanya safi ile inayovutia ukienda na chenga ni buku ndoo !! Bahati yangu ni kwamba huo mwaka ilinikubali nilichuma michumo 7 niko on fire ! Bado mingine kama minne ilikua chenga. Ilichonikera nyanya inataka attention sana na haitaki hela za mawazo !!!

Nilishageuza majeshi kwa sasa nadeal na vitu ambavyo siwi roho juu juu Bilinganya , Pilipili hoho na Nyanya chungu !! Nyanya nikilima nafanya tu ili kujiongezea ubusy na siwezi zidisha Robo hekari !!
 
Attachments

  • 69b18ddaedc30451bb8f8524d77ef13b.jpg
    69b18ddaedc30451bb8f8524d77ef13b.jpg
    253 KB · Views: 24
Mimea yako ni dhaifu kiafya, ukali wa jua na maji hayafiki chini kwenye mizizi, so inashindwa kuvumilia.
 
Inaonesha pia hata maji hayatoshi , piga maji ya kutosha pia dawa za ukungu muhimu pia jua huwa likiwa kali sana kuna ugonjwa huwa unaitwa "Kanitangaze" vidudu fulani hivi vinakula ndani ya majani panabaki na tissue nyeupe hivi kama nailoni !!

Issue za Bustani napiga sana ila nyanya nilishaacha aseee yaani nyanya inabembelezwa kila stage ya ukuaji ukiharibu kidogo inazima ! Kuanzia unapanda miche , inavyokua kadri majani yanavyokua , ikianza maua mpaka matunda ! Ukichuma mchumo wa kwanza ,huduma zikapungua inayumba ! Nyanya ni kama unahudumia mwanamke walah ! Na bei yake sokoni inafluctuate sana mwaka mmoja hivi nililima hekari moja ya maana Nilitumia mbegu ya IMARA ikanikubali bhana huduma yan VIP yaani zile chupa za dawa nilizokua napulizia nikizikusanya sehemu ungeshangaa nyingi balaa !! Ilizaa vibaya sana ! Kuingia sokoni bei iko chini nakumbuka ndoo(huku kwetu linaitwa dumu) ilikua 3000/= watu wanachagua nyanya ya kununua hiyo bei ni kwa nyanya safi ile inayovutia ukienda na chenga ni buku ndoo !! Bahati yangu ni kwamba huo mwaka ilinikubali nilichuma michumo 7 niko on fire ! Bado mingine kama minne ilikua chenga. Ilichonikera nyanya inataka attention sana na haitaki hela za mawazo !!!

Nilishageuza majeshi kwa sasa nadeal na vitu ambavyo siwi roho juu juu Bilinganya , Pilipili hoho na Nyanya chungu !! Nyanya nikilima nafanya tu ili kujiongezea ubusy na siwezi zidisha Robo hekari !!

Hapa ni wapi
 
Back
Top Bottom