Naomba msaada: Kupata mafao ya NSSF

Naomba msaada: Kupata mafao ya NSSF

Magobe T

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2008
Posts
5,602
Reaction score
3,845
1. Nilikuwa nimeajiriwa kwenye kampuni fulani ya Kitanzania tangu 2006 hadi 2010 na nilikuwa nakatwa mafao ya NSSF kila mwezi na nina salary slips zake na hata barua ya kuacha kazi na certificate of service.
2. Baada ya kuwa nimehama, nilienda kuangalia mafao yangu ya NSSF na kukuta hakuna makato ambayo yalikuwa yameshawasilishwa huko.
3. Nilienda NSSF wakaniambia wafanyakazi wa kampuni hiyo waliohama wana malalamiko kama yangu na wengine wamefungua kesi. Nawafahamu baadhi ya wanaodai pia lakini nao hawajui kinachoendelea wakiwemo wale ambao wamefungua kesi maana ni wengi na umepshapita muda mrefu - baadhi waliacha kabla yangu.
4. Nilishaenda kwenye hiyo kampuni na kuongea na HRM na akasema hakuna hela na kama zipo kipaumbele ni kulipa mishahara ya wafanyakazi. Alisema: "Kama unakuja kudai mafao ya NSSF, forget about it."
5. Sijui nifanye nini maana huu ni mwaka wangu wa 2 tangu niache kazi kwenye hiyo kampuni.
6. Naomba maoni/ushauri wa kisheria au ushauri wowote hata kama si wa sheria utakaonisaidia kupata haki yangu.
7. Natanguliza shukurani zangu.
 
Kwanza NSSF wanayo nguvu kisheria kuichukulia hatua hiyo kampuni na kama bado hawajafanya lolote pamoja na watu kuripoti hilo hiyo ni kashfa kwa NSSF!

Unaweza kudai mahakamani nafikiri wanasheria wanajua zaidi lakini nijuavyo NSSF wanapaswa kuchukua hatua kali kama wanavyofamya TRA.

Nashauri uende NSSF tawi lako na vielelezo wao wakaibane kisheria kampuni.

Nadhani ukipata mwanasheria mzuri mtavuna mapesa kibao kwa uzembe wa hiyo kampuni.

Wewe banana na NSSF tu kabla hujachukua hatua za kisheria
 
ingia website ya NSSF upate nakala ya sheria za NSSF ili ujue haki zako kama huna unaweza kuulizia NSSF penyewe wakupe nakala au wafanyakazi wa Audit firms

Upo tawi gani la NSSF ili kama kuna mtu namjua niku pm namba yake pengine anaweza kusaidia ku push kidogo.
 
ingia website ya NSSF upate nakala ya sheria za NSSF ili ujue haki zako kama huna unaweza kuulizia NSSF penyewe wakupe nakala au wafanyakazi wa Audit firms

Upo tawi gani la NSSF ili kama kuna mtu namjua niku pm namba yake pengine anaweza kusaidia ku push kidogo.

Asante. Nipo tawi la Ubungo.
 
Back
Top Bottom