1. Nilikuwa nimeajiriwa kwenye kampuni fulani ya Kitanzania tangu 2006 hadi 2010 na nilikuwa nakatwa mafao ya NSSF kila mwezi na nina salary slips zake na hata barua ya kuacha kazi na certificate of service.
2. Baada ya kuwa nimehama, nilienda kuangalia mafao yangu ya NSSF na kukuta hakuna makato ambayo yalikuwa yameshawasilishwa huko.
3. Nilienda NSSF wakaniambia wafanyakazi wa kampuni hiyo waliohama wana malalamiko kama yangu na wengine wamefungua kesi. Nawafahamu baadhi ya wanaodai pia lakini nao hawajui kinachoendelea wakiwemo wale ambao wamefungua kesi maana ni wengi na umepshapita muda mrefu - baadhi waliacha kabla yangu.
4. Nilishaenda kwenye hiyo kampuni na kuongea na HRM na akasema hakuna hela na kama zipo kipaumbele ni kulipa mishahara ya wafanyakazi. Alisema: "Kama unakuja kudai mafao ya NSSF, forget about it."
5. Sijui nifanye nini maana huu ni mwaka wangu wa 2 tangu niache kazi kwenye hiyo kampuni.
6. Naomba maoni/ushauri wa kisheria au ushauri wowote hata kama si wa sheria utakaonisaidia kupata haki yangu.
7. Natanguliza shukurani zangu.