Naomba msaada kutafsiriwa hizi dawa


Ndg ALOE VERA ndio SHUBIRI.
Iwe SHUBIRI MWITU au SHUBIRI zote ni ALOE VERA na zipo aina zaidi ya tano za shubiri
 

Ndg ALOE VERA ndio SHUBIRI.
Iwe SHUBIRI MWITU au SHUBIRI zote ni ALOE VERA na zipo aina zaidi ya tano za shubiri
 
Mkuu Yasini_waziri Mwambie mama atumie Dawa moja kati ya dawa hizi Zitamsaidia.


MARADHI YA KISUKARI:


TIBA 1:
Tafuta vijiko 10 vya chakula (10ml) vya unga wa habbat saudai,Vijiko 6 vya vya chakula (10ml) vya ubani mweupe,Gramu 50 za mvuje, Gramu 50 za shubiri,na gramu 100 za ukwaju.
Changanya dawa hizi na maji lita moja na nusu.Chemsha ibaki lita 1 ya dawa.
Tumia kikombe kimoja cha kahawa (50ml) kutwa mara tatu (1×3) mpaka itakapokwisha.

TIBA 2:

Tafuta ujazo wa sawa kwa sawa wa Habbat saudai,Ubani mweupe,Mvuje,Shubiri,Bakal had,Mani mani,Kuzbara,Kamun as-wad na Uwatu.
Matayarisho yake na matumizi ni kama tiba 1 ya Kisukari.

TIBA 3:
Kila siku kunywa kijiko kimoja (10ml) cha mafuta ya haba soda na ule kitunguu Saumu kimoja .Baada ya hapo kula mbegu za kabichi.

 
MziziMkavu asante sana pamoja mkuu maisha tu ukiona mtu anabisha nikumsamehe unenisaidia sana maana kunasiku nilikuwa nawaza sasa hizi dawa sizijui kwa kingereza nitazipate lakini naona umetusaidia sana nyingine tunazo majumbani mwetu haswa tunaotoka kijijini
 
angalieni pia majina mengine hayo hapo
Black pepper – pilipili manga
Cardamom – iliki
Caraway – Kisibiti
Cilantro – dania (majani ya giligilani)
Cinnamon – Mdalasini
Cloves – karafuu
Coriander seeds – giligilani /Kitimiri
Cumin – binzari ya pilau
curry – binzari
Ginger – Tangawizi
Lemon grass -mchaichai
Nutmeg – kungumanga
Saffron – zafarani
Sweet peppers – pilipili hoho
Turmeric – binzari manjano
 
Bibie Mwanaweja unaweza kututajia Dawa hii kwa kiingereza (Bakalhadi)?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu MziziMkavu usikasirike kwani kuemilisha inahitaji uvumilivu, upeo na uelewa kwa wanadamu unatofautiana, huenda aliponukuhuu ndipo penye makosa, endelea kutuemilisha hasa kwenye hili suala zima la tiba asilia.
 
Last edited by a moderator:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…